Tuesday, September 4, 2018

DK.SHEIN AZINDUA OFISI MPYA ZA WILAYA-DUNGA NA UIMARISHAJI MFUMO WA WAKALA WA USAJILI MATUKIO YA KIJAMII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt.Hussein Khamis Shaaban (kulia) mara baada ya kuzindua Jengo la Ofisi mpya ya Wilaya- Dunga na Uimarishaji wa Mfumo wa Matukio ya Kijamii katika hafla iliyofanyika leo katika Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja,(kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Ofisi mpya za Wilaya -Dunga pamoja na uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii uliofanyika leo Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja,(kulia)Makamo wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idii,Mama Mwanamwema Shein na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri (kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua jengo la Ofisi mpya za Wilaya -Dunga pamoja na uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii uliofanyika leo katika Wilaya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt.Hussein Khamis Shaaban wakati wa uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii uliofanyika leo katika Ofisi mpya ya Wilaya Dunga Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi mpya ya Wilaya- Dunga na Uimarishaji wa Mfumo wa Matukio ya Kijamii katika hafla iliyofanyika leo katika Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt.Hussein Khamis Shaaban na (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo ya kifundi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt.Hussein Khamis Shaaban mara baada ya uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii na Jengo la Ofisi mpya ya Wilaya Dunga uliofanyika leo katika Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja,(kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Dunga wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi mpya ya Wilaya- Dunga na Uimarishaji wa Mfumo wa Matukio ya Kijamii katika hafla iliyofanyika leo katika Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi mpya ya Wilaya- Dunga na Uimarishaji wa Mfumo wa Matukio ya Kijamii katika hafla iliyofanyika leo katika Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani). Picha na Ikulu, ZANZIBAR.

Sunday, September 2, 2018

PINDA AFUNGUA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA UKONGA ASEMA WAITARA ANATOSHA KWA JIMBO HILO

 Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda akizungumza kabla ya kumpandisha Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Ukonga , Mwita Waitara wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo hilo
 Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia CCM, Mwita Waitara wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo.


Mbunge Mteule wa Chama Cha Mapinduzi anayegombea ubunge katika Jimbo la Ukonga , Mwita Waitara akiomba kura kwa wakazi wa jimbo hilo wakati wa uzinduzi wa kampeni za  uchaguzi mdogo katika Viwanja vya Kivule Shule
 Mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM, Makongoro Nyerere akimuombea kura Mgombea ubunge wa Chama hicho kwenye uzinduzi wa kampeni
 Mbunge wa Mtera , Lusinde Maharufu kama kibajaji akimuombea kura Mgombea wa CCM Mwita waitara wakati wa kufungua kampeni na kuwataka wakazi wa ukonga wasije fanya kosa kuchagua upinzani.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba akifungua Mkutano huo


Katibu wa CCM  Mkoa wa Dar es Salaam , Saad Kusilawe akizungumza kablaya kumkaribisha Mwenyekiti wa mkoa kufungua Mkutano huo.


Wakazi wa Ukonga na Viunga vyake waliofurika katika Mkutano huo wa kampeni.

Saturday, September 1, 2018

Matumizi ya ARV hupunguza maambukizi kwa mtu mwingine

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu  akiendelea na matembezi katika moja ya banda lililokuwa katika viwanja vya maji maji Songea mkoa wa Ruvuma wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu Mkoa wa Ruvuma.

Na WAMJW-SONGEA,RUVUMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa mtu akitumia ARV kwa usahihi na kikamilifu anapunguza ewezekano wa kuambukiza VVU kwa mtu mwingine  kwa takribani Asilimia 60.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo wakati akizindua Kampeni ya FURAHA YANGU, PIMA, JITAMBUE, ISHI katika  viwanja vya Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma. 

“Kwa mujibu wa Wataalamu wa Afya ikiwemo Wanasayansi imedhihirika kwamba mtu akianza mapema kutumia Dawa anapunguza uwezekano wa kupata magonjwa nyemelezi, pia anaongeza muda wa kuishi na anapunguza uwezekano wa kuwaambukiza watu wengine”  alisema Waziri Ummy Mwalimu.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu aliselebuka na kikundi cha Bendi cha JKT Mlale wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha Yangu mkoa wa Ruvuma katika viwanja vya maji maji Songea.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa mtu akigundulika kuwa na maambukizi ya VVU na UKIMWI ataanzishiwa dawa za kupunguza makali ya Ukimwi mara moja badala ya kusubiri hali yake kuwa mbaya zaidi. 

Waziri Ummy alisema kuwa wakati Takwimu za Kitaifa zikionesha maambukizi ya VVU yamepungua kutoka Asilimia 5.7 hadi Asilimia 4.7, bado maambukizi mapya yameendelea kuwepo, takribani vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 sawa na Asilimia 40 wanaambukizwa VVU.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa Asilimia 52 ya watu wanaoishi na maambukizi ya VVU wanajifahamu kuwa wana VVU,  katika kila watu 100 Watu 48 wenye maambukizi ya VVU hawajui kuwa wana VVU jambo ambalo ni hatari kwenye kaya zao na Taifa kwa ujumla .

Mbali ya yote Waziri Ummy aliwaagiza watoa huduma  kupitia Kampeni hiyo kwamba  watu wote wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU vizuri kwa kuzingatia masharti wapewe dawa za miezi mitatu badala ya mwezi mmoja kama inavyofanywa sasa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (wapili Kushoto) akiendelea na matembezi katika viwanja vya maji maji wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu mkoa wa Ruvuma.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme.

“Watu wote wanaotumia Dawa vizuri kwa kuzingatia masharti, wapewe dawa za miezi mitatu badala ya kila mwezi kwenda kuchukua dawa katika vituo vya kutoa huduma za afya, tunaamini kwamba hatua hii itachochea watu wengi zaidi kwenda kupima na kujiandikisha kupata huduma za dawa” alisema Waziri Ummy.

Pia, Waziri Ummy  amewaagiza Waganga Wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha kwamba  vituo vya Afya vyote nchi ambavyo vimesajiliwa na kutambulika na Wizara ya Afya  kutoa huduma za kupima VVU, kutoa ushauri nasaa na kutoa dawa

“Maelekezo ambayo tumetoa Serikali, hatuoni ni kwanini katika kila kituo cha Afya kisitoe huduma za kupima VVU, zakutoa Ushaurinasaa na kutoa huduma za dawa kama ameambukizwa” alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya maji maji katika kampeni ya Furaha yangu mkoa wa Ruvuma

Sambamba na hayo Waziri Ummy alisema kuwa  katika kila watoto 100 wanaozaliwa nchini Tanzania ,Watoto 11 walikuwa wanazaliwa na maambukizi ya VVU,  ndani ya mika miwili maambukizi ya VVU yamepungua kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hadi kuwa chini ya Asilimia 5 kutoka Asilimia 11.

Aliendelea kusema kuwa  katika kila watoto 11 wanaozaliwa na VVU ni takribani watoto 5 ndio wanazaliwa na maambukizi ya VVU, inawezekana kabisa kuwa na mtoto  asilimia 0 ambae anazaliwa na maambukizi ya VVU.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme alisema kuwa kwa upande wa 909090 hali ya hali ya Mkoa wa Ruvuma takwimu zinaonesha kuwa 90 ya kwanza imefikia Asilimia 71.3 sawa na watu 41,789 wanaokadiliwa kuishi na maambukizi ya VVU imefikiwa kati ya watu wanaokadiliwa 58,534 wanaishi na VVU katika MKoa wa Ruvuma, huku 90 ya pili Asilimia 78 ambayo ni sawa na watu 41,141 ya watu waliotambuliwa hali zao za maambukizi ya VVU na tayari wamekwisha anzishiwa dawa.

Aidha, Bi. Mndeme aliendelea kusema kuwa vituo vya kutolea huduma za upimaji wa VVU vimeongezeka mkoani Ruvuma kutoka vituo 240 kwa mwaka 2016 hadi kufikia vituo 293 kufikia mwezi juni 2018, Mkoa wa Ruvuma Tayari una vituo 303, huku vituo 293 vikiwa Tayari vimekwishafikiwa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akipata huduma ya kupima maambukizi ya VVU wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu katika viwanja vya maji maji Songea mkoa wa Ruvuma.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme akipata huduma ya kupima maambukizi ya VVU wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu katika viwanja vya maji maji Songea mkoa wa Ruvuma.
Picha ya pamoja ikiongonzwa na Waziri wa Afya, Mhe Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu mkoa wa Ruvuma katika viwanja vya maji maji Songea.

WADAU WA ELIMU WATAKIWA KUCHANGIA ILI UBORESHA VYUMBA VYA MADARASA RORYA

Diwani wa kata ya Baraki Mh Mwita Laurian akikabidhi vyeti kwa wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Erengo ambapo mahafari hayo yameambatana na harambee kwa lengo la kuboresha vyumba vya madarasa hayo.

Na Frankius Cleophace, Rorya.

Wadau wa elimu Wilayan Rorya Mkoni mara wametakiwa kuendelea kuchangia fedha kwa lengo la kuboresha Vyumba vya madarasa katika shule za msingi wilayani Rorya Mkoani Mara ili kuweza kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia ikiwemo shule ya Msingi Erengo ambayo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo pamoja na upungufu wa Madarasa.

Wananchi kwa kuliona hilo katika mahafari ya darasa la saba Shule ya Msingi Erengo  wanachangi fedha kupitia harambee ambapo wamechangia zaidi ya Millioni moja pamoja na vifaa vyenye thamani ya shilingi Millioni moja huku wakiomba serikali kuwaunga mkono ili kuendeleza jitihada hizo , Makutano Gijagida ni Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Erengo na Charles Maganya ni mratibu Elimu kata ya Baraki wanazungumzia changamoto za shule hiyo huku wakipingeza nguvu za wananchi haowaliojitoa kuchagia katika harambee iliyoandaliwa.
Wanafunzi wa darasa la saba awakitoa burudani ya nyimbo katika mahafari hayo.

Maganya amesema kuwa shule yake inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa vyumba vya madarasa hivyi amezidi kuomba wadau wa elimu na wazazi kuzidi kujitoa kwa wingi kwa lengo la kutatu changamoto hiyo.

“Mazuingira ya shule yakiwa mazuri wanafunzi watapenda kusoma pia walimu watkaa shuleni hivyo sasa wazazi na wadau wa elimu kwa mkoa wa Mara na nje ya mkoa tuendelee kujitoa” alisema Mwalimu mkuu.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Baraki Mh Mwita Laurian anasema kuwa shule ya Msingi Erengo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uchakavu wa majengo hivyo amesema kuwa kama diwani wa kata hiyo atazidi kuhimiza wananchi kuendelea kujenga vyumba vya madarasa ili serikili iweze kumalizia huku akitafuta wadau mbalimbali wa elimu ili kutatua changamoto za shule hiyo.
Wananchi wa kijiji cha Baraki pamoja na wazazi wakiwa katika mahafari hayo.

Aidha  Anipha Misapa ambaye ni afisa mtendaji wa kijiji cha Baraki anasema kuwa majengi yote yenye changamoto yanaenda kukarabaitiwa huku Mwenyekiti wa kijiji hicho Emmanuel Daud akizidi kusisitiza jamii kujitolea kwenye suala la Maendeleo hususani ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika shue za msingi na Sekondari.

Wananchi wa kijiji cha Baraki wameamua kufanya harambee kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Erengo iliyopo wilayani Rorya mkoani Maraambapo wamepata vifaa vya ujenzi vyenye thamani zaidi ya shilingi Millioni moja pamoja na fedha zaidi ya million moja zilizochangwa na wanachgi na wadau wa elimu katika mahafari hayo huku wengine wakiutoa ahadi mbalimbali lengo ni kuboresha shule hiyo.
Ni vyumba vya madarasa vinavyotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Erengo iliyopo wilayani Rorya Mkoani Mara ambavyo siyo rafiki kwani vimechakaa sana.

SOMA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 1,2018
















Friday, August 31, 2018

MAWAKILI WA SERIKALI KUWA NA CHAMA CHAO – AG

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akitoa mada kuhusu Nafasi na Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wakati wa mkutano unaoendelea wa Mawakili wa Serikali waliokatika utumishi wa umma. Pamoja na mambo mengine Dk. Kilangi amesema Mawakili wa Seriakali walio katika utumishi wa umma watakuwa na chama chao.
Sehemu ya mawakili wa serikali kutoka wizara mbalimbali, Idara na Taasisi zinazojitegema, Wakala na Serikali za Mitaa ambao wapo Jijini Dodoma kwa mkutano wao wa siku mbili.

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi amesema, anakusudia kuanzisha Chama cha Wanasheria walio katika utumishi wa Umma. Dk. Kilangi ameyaeleza hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu Nafasi na Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Mawakili wa Serikali walio katika utumishi wa umma wanaokutana katika mkutano wao wa siku mbili unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Mawakili hao wa Serikali wapatao mia tisa ( 900) wanatoka Wizara mbalimbali, Idara za Serikali, Taasisi na Mashirika yanayojitegemea, Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mkutano huo ambao ni wa pili kufanyikia ulifunguliwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amebainisha kwamba, kuanzishwa kwa Chama hicho ni kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Muswaada wa Sheria ya Marekebisho Mbalimbali ( Na.2) 2018 inayoeleza kuwa , “ Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaweza kuanzisha Chama cha Wanasheri katika Utumishi wa Umma”.

Amewaeleza Mawakili wa Serikali kwamba Chama hicho kitakuwa kinakutana mara moja kwa mwaka kwaajili ya kujadili masuala mbalimbali ya kisheria ikiwamo maendeleo ya taaluma hiyo. Dk. Kilangi amesema, pamoja na wanachama wa chama hicho kukutana mara moja kwa mwaka, Waziri mwenye dhamana na mambo ya sheria anaweza kuitisha mikutano ya wanasheria waliokatika utumishi wa umma kila anapoona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Amefafanua zaidi kwa kusema, ripoti ya mikutano ya chama hicho itawasilishwa kwa Waziri wa Katiba na Sheria na kwamba, Waziri atatunga Kanuni kuhusu usimamizi, uongozi, muundo na uendeshaji wa shughuli za chama. Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuanzishwa kwa chama cha Mawakili wa Serikali walio katika utumishi wa Umma hakutawanyima fursa mawakili hao ya kujiunga au kuwa wanachama wa vyama vingine vya kitaaluma kikiwamo Tanganyika law Society ( TLS).

Akizungumzia kuhusu kuanzishwa kwa daftari la mawakili wa serikali, Mwanasheria Mkuu amesema, daftari hili litaanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Muswaada wa Sheria ya Marekebisho mbalimbali ( Na. 2) 2018 unaotamka kwamba, “ Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataanzisha Daftari la Mawakili wa Serikali ( Roll of State Attorneys)”.

Amesema daftari hilo likuwa na majina ya mawakili wa serikali kwa kuzingatia ukuu ( seniority ) miongoni mwao na kusisitiza kwamba, hatua hiyo haitaathiri sifa au hadhi ambayo mtu alikuwa nayo kabla ya kuazishwa kwa daftari hilo.

Kuhusu mawakili hao sasa kutambulika kama wanasheria wa Serikali ( State Attonerys ) Mwanasheria Mkuu wa Serikali amelitolea ufafanuzi kwa kusema Kila Afisa Sheria aliyeteuliwa au kuajiriwa katika Wizara, Idara inayojitegemea, wakala au serikali za mitaa sasa anakuwa wakili wa serikali na kwa sababu hiyo yuko chini ya usimamizi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali isipokuwa kwa Wanasheria wa Serikali ambao wapo chini ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

“Hivyo Afisa huyo anachukuliwa kuwa anafanya kazi na kutekeleza majukumu na mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Wizara zao , Idara zinazojitegemea, wakala wa serikali na Serikali za mitaa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataweweza kutoa maelekezo ya jumla au maelekezo mahsusi kwa mawakili wa serikali walio katika utumishi wa umma kuhusu utekelezaji wa majukumu yao ya kisheria.

Akawahimiza wanasheria hao kila mmoja wao kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa bidii, maarifa na ujuzi wake huku akitanguliza maslahi ya taifa lake katika kila jambo analokishughulikia. Akahadharisha kwamba, hatasita kuchukua hatua dhidi ya mtumishi yeyote atakaye kiuka maadili ya Mawakili katika utumishi wake.

Awali akifungua Mkutano huo Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, amewataka Mawakili wa Serikali kutumia njia mbadala ya usuluhi katika baadhi kesi za madai pale inapobidi na kufikia usuluhishi nje ya Mahakama. Jaji Mkuu amesema , ikiwa njia ya usuluhishi nje ya mahakama utafanyika, basi utapunguza muda wa undeshaji kwa kesi hizo ambazo nyingine huchukua hadi miaka kumi bila kufikia muafaka.

“Niwaombe wanasheria wa Serikali katika kesi nyingine za madai pale inapobidi wajaribu sana kulenga kufikia usuluhishi wa nje ya mahakama badala ya kuendesha kesi kwa miaka hata kumi, kuanzia kesi inapoanza ngazi ya chini hadi kufikia Mahakama ya Rufani” amesema Jaji Mkuu na Akasisitiza kwamba, “ Kuna wakati wanasheria wa Serikali wanakiri kwa pembeni, kuwa kesi wanayoendesha haina nafasi ya kushinda au hata wakishinda gharama hadi kupata ushindi huyo ni kubwa. Wanapambana tu kwa sababu Mkuu wa Idara au Kitengo amesema hivyo”.

Akasisitiza kwa kusema. “Hapa ndipo ipo haja ya kujenga Imani ya Mawakili hawa ( wa Serikali) na kuwaruhusu wapate usuluhisho wa mashauri nje ya mahakama”.

Akitoa takwimu za Kituo cha Usuluhishi ( Mediation Centre) cha Mahakama Kuu Dar es Salaam kwa mwaka jana ( 2017) kinaonyesha kuwa jumla ya mashauri 41 yalisuluhishwa na kituo bila ya kufikishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa na kati ya hizo, ni 10 tu zilikuwa za taasisi ya Umma.