Sunday, August 31, 2014

RACHAEL CLAVERY ASHINDA TAJI LA MISS LAKE ZONE 2014. AONDOKA NA MKOKO WA MILIONI 10!

Mshindi wa Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Mary Emanuel( kulia) na Mshindi wa tatu Nikole Sarakikya ( kushoto). Rachael amejinyakulia zawadi nono ya Gari la millioni 10 CCM Kirumba Jijini Mwanza. Shindano hilo lililokuwa na Walimbwende 18 wote wakichuana vikali kila mmoja akitaka ashinde hatimaye usiku huu Rachael Clavery amewafunika wenzake na kuibuka na ushindi. Picha zote na Faustine Ruta wabukobasports.com
Kwenye picha ya pamoja
Kwenye picha ya pamoja washindi Mshindi wa Miss Lake Zone 2014, Rachael ClaveryDoreen Robert (kushoto) Aliyeshika nafasi ya nne akipata picha ya pamoja na wenzake.Gari aliloshinda Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery usiku huu...Mshindi wa kwanza alizawadiwa gari ya shilingi mil 10, mshindi wa pili alijibebea bajaji yenye thamani ya sh. mil 4 huku mshindi wa tatu alijipatiapatia pikipiki ya Tsh mil 1.8
Jaji Mkuu wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania akitangaza tano bora.Walioshika nafasi tano boraWakiulizwa maswali.Viongozi mbalimbaliWarembo wakiwa katika Vazi la UfukweniWarembo wakiendelea na Vazi la UfukweniDoreen Robert(kulia) akipita na mwenzake na Vazi la UfukweniWarembo hao walikuwa wamepiga kambi ya siku 10 katika Lenny Hotel ya Mkoani Geita na walichuana kuwania taji lililokuwa linashikiliwa na Ruth Charles.
Dada wakiwaangalia wadogo zaoWadau wakichukua kumbukumbu..Msanii wa Kizazi kipya Barnabas akitumbuiza mashabikiBarnabas akiimba wimbo wake live na kundi la Sky Light Band jukwaani.
Kundi zima la Skylight Band likishusha muziki mkali
Skylight Band wakifanya yao jukwaani..Meneja wa bendi ya Skylight, Anneth Kushaba a.k.a AK 47 akifanya yake jukwaani.Meneja wa bendi ya Skylight, Anneth Kushaba a.k.a AK 47 akizungusha zungusha huku akiweka mbwembwe juu ya jukwaa CCM Kirumba kwenye mashindano ya Miss Lake Zone 2014.
Mgeni rasmi Leonard Bugomola Mkurugenzi wa Lenny Hotel ambaye pia alikuwa mmoja wa wadhamini wa Shindano hilo akizungumza na Wakazi wa Mwanza waliojitokeza katika Uwanja wa CCM Kiumba juu ya swala zima la Miss Lake Zone 2014. 
Mratibu wa shindano la Miss Lake Zone 2014, Flora Lauwo (kushoto) akiwa na Mgeni rasmi Bw. Leonard Bugomola. Pia Mratibu aliongeza kuwa Wakiwa kambini wilayani Geita, warembo hao walifanya shughuli za kijamii ikiwemo kutoa msaada kituo cha Yatima cha Moyo wa Huruma na kutembelea mgodi wa GGM na Hospitali ya Geita na Hifadhi ya Lubondo na kufanya usafi.
Mratibu huyo ametoa pongezi kwa wadhamini wakuu, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Redd’s, Lenny Hotel, Crown Paint, Shule ya Rishor Pre & Primary English Medium na Benki ya CRDB ya Geita. Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Warembo wote 18 jukwaani
Vazi la ufunguzi..warembo wote 18 walipanda jukwaani
Warembo waliopanda jukwaani ni Mikoa yao kwenye mabano ni Moshy Shaban: Doreen Robert; Christina Jilulu (Mwanza): Nikole Sarakikya, Mary Emanuel na Rachael Julika (Shinyanga).
Wengine ni Faudhia Haruna, Jackline Kimambo na Christina John (Kagera), huku Nyangi Warioba: Cecilia Kibada na Everlyn Charles (Simiyu). Wamo pia Martina John: Elinaja Nnko, Winfrida Nashon (Mara)huku Rose Msuya, Rachael Clavery na Faridha Ramadhani wakiwakilisha mkoa wa Geita.

MSAMA AKAMATA CD FEKI ZA MIL 200 PAMOJA NA MASHINE YA KISASA YA KURUDUFU CD

Sehemu ya CD Feki zilizokamatwa.
Msama akionesha CD zilizokamatwa katika maeneo ya Kariakoo na Kimara Bonyokwa.
Baadhi ya vifaa vinavyotumika katika kutengeneza CD feki zikiwa Kituo cha Polisi Urafiki.
Hizi ni sehemu ya CD feki zilizokamatwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akionyesha mashine ya kisasa aina ya LG iliyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa kurudufu kazi za wasanii (CD FEKI) katika maeneo ya Kariakoo na Kimarta Bonyokwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akionesha mashine ya kisasa aina ya LG waliyokamatwa nayo watuhumiwa wa kurudufu CD feki za kazi za wasanii katika maeneo ya Kariakoo na Kimara Bonyokwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP, Denis Moyo. (Picha na Francis Dande)  

Msama akionyesha wino na vifaa vingine vinavyotumika katika kutengeneza CD feki za kazi za wasanii.
Msama akionesha mashine ya kuprint Cover za CD.
CD feki zilizokamatwa katika maeneo ya Kariakoo.
Msama akizungumza na waandishi wa habari leo.
Lundo la CD feki zilizokamatwa katika maeneo ya Kimara na Kariakoo.
Kasha la CD iliyokuwa na nyimbo za mwimbaji Bahati Bukuku ikiwa imewekea stika feki ya TRA.
Baadhi ya CD feki zilizokamatwa na Kampuni ya Msama Auoctions Mart.

NA FRANCIS DANDE

OPERESHENI ya kukamata watuhumiwa wa wizi wa kazi za wasanii, imeshika kasi baada ya Kampuni ya Msama Auction Mart kukamata mashine za kisasa za kurudufu kazi za wasanii na CD feki zenye thamani ya shs. milioni 200.
Huo ni mkakati wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo pamoja na Jeshi la Polisi katika vita ya kuwapigania wasanii waweze kunufaika na kazi zao.
Mbali ya wasanii, pia harakati hizo zinalenga kuiwezesha serikali kupata mapato yake kutoka kwa wasanii ambao siku zote wamebaki duni huku wajanja wachache wakivuna mamilioni ya fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama alisema operesheni hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika maeneo ya Kariaakoo na Kimara Bonyokwa  jijini Dar es Salaam.
 “ Ttumekamata vijana watano ambao wapo katika kituo cha Polisi cha Urafiki   na taratibu za kuwafikisha mahakamani zinafanyika,” alisema Msama.
Aidha, Msama amesema katika zoezi hilo wanamshikiria mmiliki wa nyumba moja ambayo baadhi ya watuhumiwa walikutwa wakifanya uharamia wa kudurufu kazi za wasanii, hivyo kuikosesha serikali mapato yake halali. 
“Kwa namna hii, serikali haiewezi kupata mapato na pia wasanii wataendelea kuwa ombaomba kutokana na kuibiwa kazi zao,” alisema Msama.
Msama alisema, zoezi hilo ni endelevu na litafanyika nchi nzima ambapo kampuni Msama kwa kushirikiana  na Polisi wa Kituo cha Urafiki, wameweza kuwakamata jumla ya watuhumiwa 20 ambao wanasubiri taratibu za kisheria ili kesi zao ziweze kufikishwa mahakamani.
Msama aliongeza, matunda ya operesheni hiyo, yameanza kuonekana kwani kwa kushirikiana na raia wema, wameweza kukamata mashine moja kubwa ya kisasa aina ya LG ambayo huweza kuzalisha CD feki zaidi ya ishirini kwa dakika tano. 
“Katika kipindi kicha wiki moja tumekamata mzigo mkubwa wa shs mil.200 katika maeneo ya Kimara Bonyokwa na Kariakoo na kazi bado inaenedelea,” alisma Msama.
Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini, amejitwika jukumu hilo zito katika kupigania maslahi ya wahusika ambao wameshindwa kupiga hatua kutokana na wiki wa kazi zao.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAJUMBE KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA (TCD) IKULU NDOGO DODOMA LEO

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo akiongea na Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. ABdulrahman Kinana na Mhe Isack Cheyo walipowasili Ikulu ndogo mjini Dodoma kukutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo. Nyuma yao ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mwenyekiti wa UPDP Mhe Fahmi Dovutwa leo.TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP.
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo , Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Isack Cheyo, Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mhe Fahmi Dovutwa wakielekea chumba cha mikutano Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo 
Wajumbe  wa TCD wakielekea chumba cha Mikutano
Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI Mhe Joseph Mbatia, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa wakiwasili Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na wakiwasili Ikulu ndogo mjini Dodoma leo
Wajumbe wa TCD wakielekea chumba cha Mikutano Ikulu ndogo mjini Dodoma leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiagana na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiagana nna wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
Rais Kikwete akiagana na mjumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania na Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustune Lyatonga Mrema Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo. PICHA NA IKULU