Sunday, August 31, 2014

MSAMA AKAMATA CD FEKI ZA MIL 200 PAMOJA NA MASHINE YA KISASA YA KURUDUFU CD

Sehemu ya CD Feki zilizokamatwa.
Msama akionesha CD zilizokamatwa katika maeneo ya Kariakoo na Kimara Bonyokwa.
Baadhi ya vifaa vinavyotumika katika kutengeneza CD feki zikiwa Kituo cha Polisi Urafiki.
Hizi ni sehemu ya CD feki zilizokamatwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akionyesha mashine ya kisasa aina ya LG iliyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa kurudufu kazi za wasanii (CD FEKI) katika maeneo ya Kariakoo na Kimarta Bonyokwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akionesha mashine ya kisasa aina ya LG waliyokamatwa nayo watuhumiwa wa kurudufu CD feki za kazi za wasanii katika maeneo ya Kariakoo na Kimara Bonyokwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP, Denis Moyo. (Picha na Francis Dande)  

Msama akionyesha wino na vifaa vingine vinavyotumika katika kutengeneza CD feki za kazi za wasanii.
Msama akionesha mashine ya kuprint Cover za CD.
CD feki zilizokamatwa katika maeneo ya Kariakoo.
Msama akizungumza na waandishi wa habari leo.
Lundo la CD feki zilizokamatwa katika maeneo ya Kimara na Kariakoo.
Kasha la CD iliyokuwa na nyimbo za mwimbaji Bahati Bukuku ikiwa imewekea stika feki ya TRA.
Baadhi ya CD feki zilizokamatwa na Kampuni ya Msama Auoctions Mart.

NA FRANCIS DANDE

OPERESHENI ya kukamata watuhumiwa wa wizi wa kazi za wasanii, imeshika kasi baada ya Kampuni ya Msama Auction Mart kukamata mashine za kisasa za kurudufu kazi za wasanii na CD feki zenye thamani ya shs. milioni 200.
Huo ni mkakati wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo pamoja na Jeshi la Polisi katika vita ya kuwapigania wasanii waweze kunufaika na kazi zao.
Mbali ya wasanii, pia harakati hizo zinalenga kuiwezesha serikali kupata mapato yake kutoka kwa wasanii ambao siku zote wamebaki duni huku wajanja wachache wakivuna mamilioni ya fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama alisema operesheni hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika maeneo ya Kariaakoo na Kimara Bonyokwa  jijini Dar es Salaam.
 “ Ttumekamata vijana watano ambao wapo katika kituo cha Polisi cha Urafiki   na taratibu za kuwafikisha mahakamani zinafanyika,” alisema Msama.
Aidha, Msama amesema katika zoezi hilo wanamshikiria mmiliki wa nyumba moja ambayo baadhi ya watuhumiwa walikutwa wakifanya uharamia wa kudurufu kazi za wasanii, hivyo kuikosesha serikali mapato yake halali. 
“Kwa namna hii, serikali haiewezi kupata mapato na pia wasanii wataendelea kuwa ombaomba kutokana na kuibiwa kazi zao,” alisema Msama.
Msama alisema, zoezi hilo ni endelevu na litafanyika nchi nzima ambapo kampuni Msama kwa kushirikiana  na Polisi wa Kituo cha Urafiki, wameweza kuwakamata jumla ya watuhumiwa 20 ambao wanasubiri taratibu za kisheria ili kesi zao ziweze kufikishwa mahakamani.
Msama aliongeza, matunda ya operesheni hiyo, yameanza kuonekana kwani kwa kushirikiana na raia wema, wameweza kukamata mashine moja kubwa ya kisasa aina ya LG ambayo huweza kuzalisha CD feki zaidi ya ishirini kwa dakika tano. 
“Katika kipindi kicha wiki moja tumekamata mzigo mkubwa wa shs mil.200 katika maeneo ya Kimara Bonyokwa na Kariakoo na kazi bado inaenedelea,” alisma Msama.
Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini, amejitwika jukumu hilo zito katika kupigania maslahi ya wahusika ambao wameshindwa kupiga hatua kutokana na wiki wa kazi zao.

No comments: