Mshindi wa Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Mary Emanuel( kulia) na Mshindi wa tatu Nikole Sarakikya ( kushoto). Rachael amejinyakulia zawadi nono ya Gari la millioni 10 CCM Kirumba Jijini Mwanza. Shindano hilo lililokuwa na Walimbwende 18 wote wakichuana vikali kila mmoja akitaka ashinde hatimaye usiku huu Rachael Clavery amewafunika wenzake na kuibuka na ushindi. Picha zote na Faustine Ruta wabukobasports.com
Kwenye picha ya pamoja
Kwenye picha ya pamoja washindi Mshindi wa Miss Lake Zone 2014, Rachael ClaveryDoreen Robert (kushoto) Aliyeshika nafasi ya nne akipata picha ya pamoja na wenzake.Gari aliloshinda Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery usiku huu...Mshindi wa kwanza alizawadiwa gari ya shilingi mil 10, mshindi wa pili alijibebea bajaji yenye thamani ya sh. mil 4 huku mshindi wa tatu alijipatiapatia pikipiki ya Tsh mil 1.8
Jaji Mkuu wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania akitangaza tano bora.Walioshika nafasi tano boraWakiulizwa maswali.Viongozi mbalimbaliWarembo wakiwa katika Vazi la UfukweniWarembo wakiendelea na Vazi la UfukweniDoreen Robert(kulia) akipita na mwenzake na Vazi la UfukweniWarembo hao walikuwa wamepiga kambi ya siku 10 katika Lenny Hotel ya Mkoani Geita na walichuana kuwania taji lililokuwa linashikiliwa na Ruth Charles.
Dada wakiwaangalia wadogo zaoWadau wakichukua kumbukumbu..Msanii wa Kizazi kipya Barnabas akitumbuiza mashabikiBarnabas akiimba wimbo wake live na kundi la Sky Light Band jukwaani.
Kundi zima la Skylight Band likishusha muziki mkali
Skylight Band wakifanya yao jukwaani..Meneja wa bendi ya Skylight, Anneth Kushaba a.k.a AK 47 akifanya yake jukwaani.Meneja wa bendi ya Skylight, Anneth Kushaba a.k.a AK 47 akizungusha zungusha huku akiweka mbwembwe juu ya jukwaa CCM Kirumba kwenye mashindano ya Miss Lake Zone 2014.
Mgeni rasmi Leonard Bugomola Mkurugenzi wa Lenny Hotel ambaye pia alikuwa mmoja wa wadhamini wa Shindano hilo akizungumza na Wakazi wa Mwanza waliojitokeza katika Uwanja wa CCM Kiumba juu ya swala zima la Miss Lake Zone 2014.
Mratibu wa shindano la Miss Lake Zone 2014, Flora Lauwo (kushoto) akiwa na Mgeni rasmi Bw. Leonard Bugomola. Pia Mratibu aliongeza kuwa Wakiwa kambini wilayani Geita, warembo hao walifanya shughuli za kijamii ikiwemo kutoa msaada kituo cha Yatima cha Moyo wa Huruma na kutembelea mgodi wa GGM na Hospitali ya Geita na Hifadhi ya Lubondo na kufanya usafi.
Mratibu huyo ametoa pongezi kwa wadhamini wakuu, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Redd’s, Lenny Hotel, Crown Paint, Shule ya Rishor Pre & Primary English Medium na Benki ya CRDB ya Geita. Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Vazi la ufunguzi..warembo wote 18 walipanda jukwaani
Warembo waliopanda jukwaani ni Mikoa yao kwenye mabano ni Moshy Shaban: Doreen Robert; Christina Jilulu (Mwanza): Nikole Sarakikya, Mary Emanuel na Rachael Julika (Shinyanga).
Wengine ni Faudhia Haruna, Jackline Kimambo na Christina John (Kagera), huku Nyangi Warioba: Cecilia Kibada na Everlyn Charles (Simiyu). Wamo pia Martina John: Elinaja Nnko, Winfrida Nashon (Mara)huku Rose Msuya, Rachael Clavery na Faridha Ramadhani wakiwakilisha mkoa wa Geita.
No comments:
Post a Comment