Tuesday, October 2, 2018

Rais Magufuli atekeleza ahadi ya kutoka Milioni 20 kwa wavuvi na Mama Janeth Magufuli Milioni 5 za mama ntilie eneo la feri jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Oktoba, 2018 ametekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi Milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Magufuli alitoa ahadi hiyo jana alipokutana na wajasiriamali hao wakati akifanya mazoezi ya jioni pamoja na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli ambaye pia ametekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi Milioni 5 kwa akina Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.
Fedha hizo zimekabidhiwa na Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike kwa Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga, na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Tulusubisya Kamalama.
Kabla ya kukabidhi fedha hizo Bw. Ngusa amesema pamoja na kutoa fedha hizo Mhe. Rais Magufuli ameagiza Manispaa ya Ilala impelekee taarifa ya mapato na matumizi ya soko la samaki la Feri haraka iwezekanavyo na amemuagiza Mkuu wa Wilaya na Manispaa ya Ilala kushughulikia kero za wavuvi na wajasiriamali wa eneo hilo ikiwemo ushuru wenye kero na tatizo la vyoo.
Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina mama wajasiriamali wa Feri Bi. Bi Ashura Seif Nanjonga wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwasaidia fedha hizo na kwa kuwajali wao pamoja na Watanzania wengine hasa wanyonge.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutembelea soko la Feri na kuwasaidia wajasiriamali wa soko hilo na amesema yeye na timu yake ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala wataanza mara moja kushughulikia kero za wajasiriamali hao.

.
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike (tai Nyekundu) akikaribishwa kwenye  ofisi ya muda ya Umoja Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike (tai Nyekundu) akiongea na Wajasiriamali waliojikusanya kushuhudia utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsikiliza Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kabla ya kumkabidhi shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo
 Wajasiriamali wakishuhudia utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, pamoja na na mkewe Mama Janeth Magufuli aliyeahidi kutoa shilingi Milioni 5 kwa akina Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.
 Wajasiriamali wakishuhudia utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike (tai Nyekundu) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiongea na Wajasiriamali waliojikusanya kushuhudia utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiongozwa kuangalia sehemu itapojengwa ofisi  na Wajasiriamali waliojikusanya kushuhudia utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na  Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani   wakielekea sehemu itapojengwa ofisi zao katika utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na  Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani   sehemu itapojengwa ofisi  na Wajasiriamali waliojikusanya kushuhudia utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwaangalia Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga wakiweka sahihi katika hati za makabidhiano ya fedha taslimu kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli huku wakishuhudiwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Tulusubisya Kamalama na mshauri wa Rais Masuala ya sheria Bw. Dunstan Kiobya (kushoto)
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi shilingi milioni 5 kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga kutoka kwa mke wa Rais Mama Janeth Magufuli alizoahidi kuwasaidia Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi shilingi milioni 20 Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo
 Wajasiriamali wakishangilia kwa furaha utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) na ya Mama Janeth Magufuli ya kutoa msaada wa shilingi milioni 5 kwa kia na mama waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
 Wajasiriamali wakishangilia kwa furaha utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) na ya Mama Janeth Magufuli ya kutoa msaada wa shilingi milioni 5 kwa kia na mama waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
 Wajasiriamali wakishangilia kwa furaha utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) na ya Mama Janeth Magufuli ya kutoa msaada wa shilingi milioni 5 kwa kia na mama waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
 Wajasiriamali wakishangilia kwa furaha utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) na ya Mama Janeth Magufuli ya kutoa msaada wa shilingi milioni 5 kwa kia na mama waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam

  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike kiongozi wa akimsikiliza kiongozi wa Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga akishukuru baaada ya kupokea shilingi milioni 5 kutoka kwa mke wa Rais Mama Janeth Magufuli alizoahidi kuwasaidia Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsikiliza Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam akishukuru kwa msaada wa shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo
 Wajasiriamali wakishuhudia utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, pamoja na na mkewe Mama Janeth Magufuli aliyeahidi kutoa shilingi Milioni 5 kwa akina Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akipewa mikoni na wajasiriamali wenye furaha baada ya  kukabidhi shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) na shilingi milioni 5 toka kwa Mama Janeth Magufuli kwa kinamama waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA

Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro kabla ya kuikabidhi taarifa hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (kulia). Wengine katika picha Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda (wa pili kushoto) na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Bi. Merry Mwanjelwa.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro pamoja na watendaji wa Wilaya ya Kilosa wakati wa kukabidhi taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. kulia ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Wengine katika picha wa pili kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Bi. Merry Mwanjelwa.

Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. Kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda.

aadhi ya viongozi wa halmashauri za vijiji saba wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa kuwapa taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.

Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi wa halmashauri za vijiji saba kuhusu taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.
 
 

Na Munir Shemweta, Morogoro 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekabidhi taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji saba vya wilaya hiyo na mpango wa utekelezaji wake na kuagiza wote waliohusika kupotosha mipaka ya eneo hilo akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Lukuvi alitoa agizo hilo leo mkoani Morogoro wakati akikabidhi taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Jaji wa Mahakama Kuu ambaye sasa ni jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacob Mwambegele kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe kuhusiana na mgogoro wa mipaka ya kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani vya Mambegwa, Mbigiri, Dumila, Matongolo na Mfulu vilivyopo Wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. 

“Wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika process yote ambayo kwa kiasi fulani imeigharimu serikali fedha nyingi na kuipa maumivu serikali katika suala hilo ni lazima wachukuliwe hatua kali” alisema Lukuvi. 

Taarifa ya uchunguzi ilibaini chanzo cha mgogoro ni kukosekana ushirikishwaji wa vijiji jirani katika kuainisha na kuweka mipaka ya kijiji cha Mabwegere jambo lililosababisha kijiji kiwe na eneo la ukubwa wa hekta 10, 234 kuliko hata kijiji mama cha Mfulu chenye hekta 1,717 jambo lililothibitishwa na ukweli kwamba mipaka ya kijiji hicho imeingia ndani ya mipaka ya kata tatu za Mbigiri, Msowero, na Kitete ingawa kiutawala kijiji cha Mabwegere kinaratibiwa na kata ya Kitete. 

Hata hivyo, Waziri wa Ardhi alisema wizara haijakifuta kijiji cha Mabwegere bali itaanza kutekeleza mapendekezo ya uchunguzi ya kufuta mipaka ya kijiji hicho ambapo sasa TAMISEMI kwa kushirikiana na wilaya ya Kilosa itatakiwa kuanza mchakato wa kuandaa upya mipaka ya vijiji hivyo kwa njia shirikishi. 

Katika taarifa yake, Jaji Jacob Mwambegere alipendekeza kwa nia ya kuboresha utendaji kazi, weledi, maadili na umakini na uwezo wa kulinda na kutunza kumbukumbu katika idara ya Upimaji na Ramani na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi hatua za kinidhamu zichukuliwe ili kuzuia migogoro ya ardhi. Kwa mujibu wa Lukuvi, Wizara ya Ardhi ilikosea katika zoezi la upimaji wa kijiji cha Mabwegere lakini wilaya ya Kilosa itakuwa na jukumu la kuanza mchakato upya wa uanzishaji wa kijiji hicho. 

Alisema, kwa kuwa serikali inaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani ni jukumu la Tamisemi kwa kushirikiana na wilaya ya Kilosa kuhakikisha mipaka inaandaliwa upya kwa ajili ya kuanzishwa kijiji upya.
Waziri wa Ardhi alisisitiza kuwa shughuli za binadamu kama vile ufugaji na kilimo hazihusiani na masuala ya mipaka, hivyo wilaya ya Kilosa pamoja na kushughulikia suala la mipaka lazima iandae mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuanza kupendekeza maeneo ya ufugaji kwa vijiji vyote saba na kusisitiza kuwa ni lazima busara itumike katika kushughulikia jambo hilo. 

Kwa upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda alisema uanzishwaji kijiji cha Mabwegere haukufuata sheria na kuwataka wataalamu kuacha kuwa na nidhamu ya woga na kuzingatia kanuni na sheria katika kutekeleza majukumu yao. Aidha, amemuelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI kuunda timu itakayochunguza mchakato mzima wa kuanzisha kijiji hicho, na kila atakaebainika kuhusika na uanzishaji wa kijiji hicho kinyume na sheria achukuliwe hatua. 

Naye naibu Waziri wa Kilimo Merry Mwanjelwa alisisitiza hatua kuchukuliwa kwa wote waliohusika na kusema katika serikali hii ya awamu ya tano ni lazima kufufua makaburi kwa minajili ya kubaini wote waliohusika kuidanganya serikali. 

Taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa mipaka kati ya kijiji cha Mabwegere chenye jumla ya hekta 10,234 na mifugo takriban 24,146 na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa àmbao mara kadhaa ulisababisha vifo vya watu tangu mwaka 2008 lifanyika kwa muda wa siku sitini ambapo uchunguzi wake ulizingatia uanzishwaji, upimaji, utolewaji hati miliki kwa kijiji cha Mabwegere, maeneo yenye mgogoro na hatua zilizokwishachukuliwa juu ya mgogoro huo, uwiano wa ardhi, mifugo na mahitaji mengine ya ardhi pamoja na vyanzo vingine tofauti vya mgogoro. 

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiambatana na Manaibu waziri Tamisemi Joseph Kakunda na Kilimo Merry Mwanjelwa amekutana na viongozi wa Halmashauri za vijiji hivyo saba na kuwasomea taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani. 

Lukuvi amewaeleza wananchi hao kuwa ameikubali taarifa nzima ya uchunguzi kwa kuwa sheria inampa nafasi ya kuikubali au kuikataa taarifa hiyo, hivyo kuikubali kwake ni mwanzo wa utekelezaji wa mapendekezo ya uchunguzi na ndiyo maana aliamua kwenda kuwaeleza ukweli wa suala hilo. 


Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi viongozi wa wizara nne za Ardhi, Tamisemi, Kilimo pamoja na wizara ya Uvuvi na Mifugo walikaa pamoja na na kupanga mpango wa utekelezaji uchunguzi huo na namna ya kushughulikia mgogoro baina ya kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 2,2018


 tanzanite-dondoshA mtanzania-DONDOSHA-front mwananchi-dondosha-magazeti raia-mwema-dondosha-front tanzania-daima-dondosha-magazeti tanzanite-dondosha-magazeti tanzania-daima-dondosha-magazeti-michezo raia-mwema-dondosha-michezo jamvi-la-habari-dondosha-michezo mwananchi-michezo-dondosha-magazeti mtanzania-DONDOSHA bingwa-dondosha-magazeti bingwa-michezo-dondosha-magazeti

Monday, October 1, 2018

INTERNATIONAL YOUNG FASHION DESIGNERS SHOWCASE TOUR IN TANZANIA


Group photo from left: Ms Angel Hon, Curator of International Young Fashion Designers Showcase Tour, Ambassador Ramadhani Mwinyi, Deputy Permanent Secretary Ministry of Foreign Affairs, MrsPinda, Dr Annie Wu, Honorary Consul of the United Republic of Tanzania to Hong Kong and Macau, Hon MizengoPinda, Former Prime Minister of Tanzania Ms Devotha Mdachi, Managing Director of Tanzania Tourist BoardHon Angela Kairuki, Minister of Minerals, United Republic of Tanzania, Mr Joseph Kahama, Secretary General of Tanzania China Friendship Promotion Association and Mr Matindi, CEO of Air Tanzania.
Opening speech by Ms Devotha Mdachi, Managing Director of Tanzania Tourist Board.
Speech by Dr. Annie Wu, initiator of the showcase tour, Honorary Consul of the United Republic of Tanzania to Hong Kong Administrative Region.
Speech by Honorable Mizengo Peter Pinda, Former Prime Minister and Member of International Panel of Advisors on Belt and Road Initiative


Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Kenny Li from Hong Kong
Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Mountain Yam from Hong Kong
Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Mary Yu from Hong Kong
Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Veronica Angel from Panama
Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Tony Vergara from Panama.
Group photo of all attended designers and models.


*Talented Young Fashion Designers Gathered in Enchanting Africa

After the shows in Iceland and Panama, “International Young Fashion Designers Showcase Tour” set off her journey to Dar es Salaam as its third stop. A gala fashion show held at Hyatt Regency of Dar es Salaam on Sept 28 featuring the collections of the participating international young fashion designers.

To support the Belt and Road Initiative (BRI) launched by the Chinese Government to promote trade, infrastructure and networking strategy among countries, the “International Young Fashion Designers Showcase Tour” is organized aims to provide a platform for the young fashion designers to showcase their works globally.

This project is initiated by Dr. Annie Wu, SBS, JP, initiator of the showcase tour and the Honorary Consul of the United Republic of Tanzania to Hong Kong and Macau, to boost her relationship between China and Africa.

It is honored that Hon. Mizengo Peter Pinda, Former Prime Minister of Tanzania was present as the Guest of Honour. He officiated the catwalk show together with Dr Annie Wu and Ms Devotha Mdachi, Managing Director of Tanzania Tourist Board. They were joined by Mrs Pinda, Hon Angela Kairuki, Minister of Minerals, United Republic of Tanzania, Ambassador Ramadhani Mwinyi, Deputy Permanent Secretary Ministry of Foreign Affairs, Mr Joseph Kahama, Secretary General of Tanzania China Friendship Promotion Association, Ms Angel Hon, Curator of “Belt and Road International Young Fashion Designers Showcase Tour”, Mr Xu Chen, Minister Councellor of the Embassy of China in Tanzania and Mr Matindi, CEO of Air Tanzania.

“Dar es Salaam is an amazing and vibrant city filled with exotic and vivacious fashion, and I am incredibly thrilled to see the young fashion designers to be present here with positive energy and attitude, sharing their lively collections with the public. Getting inspired by this resourceful and ample city, the designers continue to express their enthusiasm of fashion with designers from various countries,” Dr. Annie Wu said.

The catwalk show presented the work of 11 designers from various countries including Tony Vergara and Veronica Angel from Panama, Hildur Yeoman from Iceland, Kemi Kalikawe from Tanzania, Junne Liu, Jarel Zhang from China, including the Trio-designer team, Lina, Yingzi, and Yuzhu from Kanoe, and Mary Yu, Kenny Li, Singchin Lo and Mountain Yam from Hong Kong.

Apart from their own outfits, the specially produced "Belt & Road" collection will be featured by selected African and Asian models.To enhance the blending of African and Chinese culture, special performances were arranged. The fashion show was opened by a local DJ and an African drummer, mixing African drums with the modern electro-acoustic. In addition, Anna Chau, the first female face-changing master from Hong Kong, gave a special Face Changing performance, blending the unique elements from the Chinese and African cultures and accompanied by brand new music arrangement and choreography. Prior to the show, Lee Wai Woo, a calligrapher from Hong Kong, offered the guests a fan with Chinese calligraphy, aiming to promote Chinese culture to the world.

“International Young Fashion Designers Showcase Tour” is initiated by Dr. Annie Wu, organized by “Belt and Road International Young Artist Development Centre”, curated by Ms. Angel Hon and coordinated by PR Network. After the inaugural show in Reykjavik in Iceland and second is Panama City, then Dar es Salaam in Tanzania and finally .


The event in Tanzania is co-sponsored by the Tanzania Tourist Board and Tanzania China Friendship Promotion Association.

KITUO CHA SANAA CHA URUSI NA TANZANIA WAMKUMBUKA ALIYEKUWA MCHORAJI NGULI MSAGULA

Na Agness Francis,globu ya Jamii

Kituo cha utamaduni cha Urusi na Tanzania wanaadhimisha wiki ya kumbu kumbu ya aliyekuwa mchoraji nguli hapa nchini Boniface Msagula.

Msagula aliyezaliwa 1939 kijiji cha ndanda wilayani masasi mkoa wa Lindi na kufariki 2005 anakumbukwa na kituo hicho kwa kuonyesha sanaa ya michoro yake ya aina ya tinga tinga alichora enzi ya uhai wake.

Akizungunza jijini Dar es Salaam aliyekuwa Mkurugenzi wa kituo hicho Rifat Pateev amesema maonesho hayo yameana jana katika hicho na kilele chake itakuwa Oktoba 6 mwaka huu.Amefafanua muda wa kuanza kwa maonesho hayo ni saa nne asubuhi na kumalizika saa 10 jioni na hakuna kiingilio,na watu waliokuwa wakijishuhulisha na Sanaa hapa jijini Dar es Salaam hasa Rifat Pateev aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha utamaduni cha Urusi na Tanzania. 

Akifafanua zaidi Rifat alisema alivutiwa Sana na viwango na uasili wa kazi za Sanaa za Msagula."Miongoni mwa wasanii wa kitanzania ambao nimezishuhudia kazi zao ni Damian Msagula ana michoro ya kipekee,rangi katika michoro na picha zake zilikuwa zikiendana vizuri na kwa uhakika,hiki kilikuwa ni kipaji muhimu kwake"amesema Rifat Pateev. 

Pia ametaja baadhi ya Maonyesho ya picha michoro na Sanaa aliyowahi kufanya Msagula katika sehemu mbali mbali ni mwaka 1976 New Africa hotel Dar es salaam, mwaka 1992 Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, mwaka 1993 Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, mwaka 1995 Telelom building Bonn, mwaka 1996 Dunia ya mizimu ya Msagula kituo cha utamaduni cha urusi na Dar es Salaam.Pia mwaka 1998 simulizi za Msagula kituo cha utamaduni cha urusi na Dar es Salaam,mwaka 1999 Tinga tinga na 2000 Msagula-Solo Exhibition. 

Akimzungumzia Mchoraji huyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Elias Jengo amesema Msagula akiwa na miaka 15 kabla ya kuanza kufanya kazi ya sanaa yake ya kuchora alikuwa mwanamuziki na kuanzisha bendi kadhaa.Amezitaja bendi hizo ni Uhuru Jazz,The black hammer boxing na Skylarks.Pia ilipofika mwaka 1972 alijishughulisha na uuzaji wa matunda kutoka mkoani Tanga kwenye eneo la duka la Morogoro Stores ambapo ndio alikutana na wasanii wa michoro ya Tinga tinga.

Profesa Jengo amesema msanii huyo ambaye hakuwahi kuwa na familia wala kuwa na watoto alikuwa na urafiki wa muda mrefu na watu waliokuwa wakijishughulisha na sanaa katika Jiji la Dar es Salaam hasa Rifat Pateev aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Urusi na Tanzania.

ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smitha Bhalia akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa kwa mkazi wa Kigamboni wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani ambapo Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) walifanya upimaji bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni. Katika upimaji huo makampuni mbalimbali ya dawa za binadamu yaligawa dawa bure kwa watu waliokutwa na matatizo yaliyohitaji kutumia dawa.


Na Genofeva Matemu – JKCI


1/10/2018 Zaidi ya watu 300 wamefanyiwa upimaji wa magonjwa ya moyo pamoja na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya ya moyo katika maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni.

Katika upimaji huo uliofanywa na madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) jumla ya watu 169 wakiwemo watoto walipimwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram ECHO) na 135 ambao ni watu wazima walipima kipimo cha kuangalia jinsi umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography-ECG).


Akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Rweyemamu alisema kwa upande wa watoto waliwaona 34 sita kati yao walikutwa na matatizo ya moyo na watu wazima 10 walikutwa na matatizo wote hao wamepewa rufaa ya moja kwa moja ya kwenda kutibiwa JKCI.

“Wananchi wengi tuliowaona na kuwafanyia vipimo wamekutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu ambapo tumewapa dawa za kwenda kutumia pamoja na ushauri na wachache kati yao tumewapa dawa za ugonjwa wa kisukari”, alisema Dkt. Rweyemamu.

Wananchi hao walifanyiwa vipimo hivyo wakati Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Tanzania walipokuwa wakiadhimisha siku ya moyo duniani iliyofanyika hivi karibuni katika hospitali ya Vijibweni iliyopo Wilaya ya Kigamboni na kutoa dawa za moyo kwa asilimia 80 ya wananchi waliopimwa na wengine wachache kupewa dawa za kisukari

Akizungumza na wananchi wa Kigamboni waliohudhuria upimaji huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile aliwataka wananchi hao kutoishia kufanya upimaji kwenye siku za maadhimisho tu bali kujitokeza mara kwa mara kupima afya zao na kutunza mioyo yao kwa kula milo yenye lishe bora, kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ya mara kwa mara, pamoja na kupunguza matumizi ya pombe na sigara.

“Wataalamu wa magonjwa ya afya tunaamini kwamba tiba sahihi za magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kuyakinga; serikali imejipanga kuanzisha mpango wa taifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ili tuweze kuzishusha huduma za magonjwa hayo hadi katika ngazi za kata katika vituo vyetu vya afya” alisema Mhe. Dkt. Ndungulile.

“Naipongeza sana Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya kwani imekua ikitumika kama shamba darasa kwa kutoa elimu kwa madaktari wengine waliopo mikoani lakini pia kutoa madaktari bingwa wa taasisi kwenda kwenye jamii kutoa huduma ya afya”, alisema Mhe. Dkt. Ndungulile

Siku ya moyo duniani huazimishwa Duniani kote kila mwaka tarehe 29 Septemba ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni , “kwa moyo wangu, kwa moyo wako, sote pamoja kwa mioyo yetu , tunatimiza ahadi”

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUKUZA UELEWA WA SHUGHULI ZA JUMUIYA HIYO KWA WANANCHI WAKE

Zamaradi Kawawa, MAELEZO, Windhoek, Namibia 

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC zinatakiwa kukuza uelewa wa shughuli za SADC kwa wananchi wake kwa kufundisha mashuleni historia ya ukombozi wa nchi hizo pamoja na kutumia wimbo wa SADC na bendera yake kwenye shughuli za kitaifa na kimataifa.

Baraza la SADC la Mawaziri wa nchi wanachama wanaoshughulikia sekta za Mawasiliano, Habari, Ujenzi na Uchukuzi walikubaliana hayo katika kikao kilichofanyika Septemba 27,2018 Windhoek, Namibia baada ya kufunguliwa na Waziri wa Madini na Nishati wa Namibia Mheshimiwa Tom Alweendo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo.

Kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kilisema wananchi wa SADC wanatakiwa kuelimishwa kuhusu SADC kwa kufahamu historia yake na ukombozi wa nchi wanachama, alama za SADC zikiwemo bendera, nembo, wimbo na itifaki yake kwa kuhusisha elimu hiyo kwenye mtaala wa elimu kwa nchi wanachama.

Akifungua kikao hicho, Waziri wa Madini na Nishati wa Namibia Mheshimiwa Alweendo alisema kuna taarifa nyingi nzuri za kuwaeleza wananchi wa nchi wanachama kuhusu SADC hivyo ni jukumu la Serikali za nchi za SADC kuelimisha na kuwaeleza wananchi wake wakati chombo hicho kkiendelea kujiimarisha.

Kikao hicho cha siku moja kilichokutana kwa lengo la kupitia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya nchi wanachama kwenye maeneo ya sekta za Mawasiliano, Habari, Ujenzi na uchukuzi kilisimama kwa dakika moja kabla ya kuanza ili kuonyesha masikitiko yao kwa vifo vya watanzania zaidi ya 200 vilivyotokana na ajali ya MV Nyerere Ziwa Victoria, Mwanza.

Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bi. Susan Mlawi kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambaye kwa niaba ya Serikali alipokea salamu za pole kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo kufuatia vifo vya watanzania zaidi ya 200 vilivyotokana na ajali ya MV Nyerere kwenye Ziwa Victoria mkoani Mwanza hivi karibuni.

Aidha, Kikao hicho kiliipongeza Tanzania kwa kupata tuzo ya dunia ya usalama wa anga baada ya kufaulu kwa kukidhi vigezo vilivyowekwa na Baraza la usafiri wa anga duniani vinavyohusu uhakika wa usalama wa anga.Wakati wa kikao hicho cha baraza la SADC la Mawaziri wa sekta za Mawasiliano, Habari, Ujenzi na Uchukuzi, Bi Mlawi alieleza nia ya Tanzania ya kupeleka mgombea kwenye nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na kuomba ushirikiano wa nchi wanachama wa SADC wakati wa uchaguzi ukifika.

Alimtaja mgombea huyo kuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr Agnes Kijazi, mwanamke msomi wa ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD) mwenye uzoefu wa miaka 30 kwenye masuala ya hali ya hewa kutoka nchi za SADC.Mheshimiwa Alweendo kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho alisema nchi wanachama wa SADC zimepiga hatua kubwa kwenye masuala ya hali ya hewa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya satellite iliyoimarisha kwa kiasi kikubwa matokeo ya utabiri wa hali ya hewa hivyo kuwezesha nchi kukabiliana na majanga ya ukame, mafuriko na moto yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr. Agnes Kijazi ambaye pia alitambulishwa katika kiako hicho aliiambia Idara ya Habari-MAELEZO kuwa Tanzania inajipanga kutekeleza miradi miwili mikubwa ya SADC ikiwemo uboreshaji wa chuo cha yaifa cha hali ya hewa kilichopo Kigoma pamoja na uwekaji wa miundo mbinu ya kisasa ya utabiri wa hali ya hewa itakayoimarisha huduma za utabiri wa hali ya hewa kwa nchi ili kupunguza umaskini. 

Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC ina nchi wanachama 16 zikiwemo Namibia ambaye ni mwenyekiti na Tanzania ni Makamu mwenyekiti wa Jumuiya hiyo. Nchi nyingine ni Zimbabwe, Zambia, Malawi, Afrika Kusini, Botswana, Angola, Msumbiji, Eswati, Lesotho, DRC, Mauritius, Comoro, Seychelles na Moroco. 

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 1, 2018