Wednesday, May 2, 2018
Tuesday, May 1, 2018
RAIS MAGUFULI AHUTUBIA SHEREHE SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI ZILIZOFANYIKA KITAIFA MKOANI IRINGA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
Wafanyakazi mbalimbali wakipita kwa maandamano katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
Sehemu ya Wafanyakazi waliohudhuria katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi mara baada ya kuhutubia mamia ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na wasanii wa kizazi kipya kutoka mkoani Iringa waliotumbuiza katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
Sehemu ya Walimu waliohudhuria katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa wakipiga makofi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiwa na Chifu wa Wahehe, Mtwa Adam Mkwawa II ambaye alihudhuria katika katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiondoka katika uwanja wa CCM wa Samora mkoani Iringa mara baada ya kuhutubia katika shere za Mei Mosi.
PICHA NA IKULU
BALOZI MASILINGI AMVALISHA CHEO BRIGEDIA JENERALI AP MUTTA MWAMBATA WA JESHI UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI NA CANADA
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta (hayupo pichani) kwenye hafla fupi ya kuvikwa cheo cha Brigedia Jenerali iliyofanyika siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22, Washington, DC.Balozi Wilson Masilingi alimwagia sifa kwa kazi nzuri anayofanya kwa nidhamu ya hali ya juu, kujituma kwake na kushirikiana ndio chachu ya mafanikio yake.
Wambata wengine waliovikwa vyeo vya Brigedia Jenerali ni Brig Gen AS Nwamy- Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini India, Brig Gen AM Alphonce Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Brig Gen JJ Mwaseba- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na Brig Gen RC Ng'umbi- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini China. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production kwa hisani ya Kilimanjaro Studio.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akitoa hotuba fupi ya kumpongeza Brigedia Jenerali Adolph Mutta kwa Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akiondoa cheo cha Colonel na kumvisha cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Brigedia Jenerali AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbu wa mkutano a Nyerere hall uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimvua kofia ya cheo cha Colonel na kumvisha kofia ya cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbi wa mkutano wa Nyerere Hall.uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta akipongzwa na mkewe Agnes Mutta.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta akitoa shukurani kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkuu wa majeshi Tanzania Luteni Jenerali Venance Mabeyo. Katika hotuba yake ya shukurani alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumfikisha pale alipo na kushukuru familia yake hasa mke wake. Brigedia Jenerali AP Mutta aliwashukuri Balozi mstaafu Mhe. Liberata Mulamula na Mhe. Balozi Wilson Masilingi wakiwemo Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ushirikiano wanaompa na akaahidi ataendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha wanaiwakilisha vyema nchi yetu nchini Marekani.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi (watatu toka kushoto) na wengine toka kushoto ni EdgarMutta (mtoto wa Brigedia Jenerali Mutta), Bi. Agnes Mutta (Mke wa Birigedia Jenerali Mutta),Bi Marystela Masilingi (mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi) na kulia ni Judy Mutta (mtoto wa Brigedia Jenerali Mutta)
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto waliokaa) wengine waliokaa toka kushoto ni aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula, Bi. Agnes Mutta, mke wa Brigedia Jenerali AP Mutta na Kulia na Bi. Marystela Masilibgi mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi. Wengine waliosimama ni Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto waliokaa) wengine waliokaa toka kushoto ni aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula, Bi. Agnes Mutta, mke wa Brigedia Jenerali AP Mutta na Kulia na Bi. Marystela Masilingi mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi. Wengine waliosimama ni Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na familia yake kutoka kushoto ni Edgar Mutta, mkewe Bi. Agnes Mutta na kulia ni Judy Mutta.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na mkewe Bi. Agnes Mutta.
SPIKA NDUGAI ATEMBELEA KIWANDA CHA ASASI KILICHOPO MKOANI IRINGA
MNEC wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoani Iringa na mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS Bw.Salim Abri akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai wakati alipowasili kiwandani hapo na kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho mjini Iringa leo.
MNEC wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoani Iringa na mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS Bw.Fuad Abri akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai wakati alipowasili kiwandani hapo na kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho mjini Iringa leo katikati ni MNEC wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akizungumza na Ahmed Salim Mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha ASAS wakati alipowasili kiwandani hapo na kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho mjini Iringa leo katikati ni .MNEC wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka Mkoani Iringa na mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS Bw.Salim Abri.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akiendelea na ziara yake kiwandani hapo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimsikiliza Bw. Fuad Abri Mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS wakati akitoa maelezo alipokembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo leo mjini Iringa katikati ni MNEC wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri na wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo la Kilolo Mh. Venance Mwamoto.
Fuad Abri Mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha Asas akitoa maelezo wa kwa Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai wakati alipokembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo leo Mjini Iringa , Ahmed Salim mmoja wa wakurugenzi wa ASAS na Mbunge wa jimbo la Kilolo Mh. Venance Mwamoto.
ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiendelea na kazi.
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai wakati akitembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo leo
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai wakati akionyeshwa moja ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha ASAS wakati alipokembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo leo wa pili kutoka kushoto ni MNEC wa CCM Mkoa wa Iringa na anayefuatia ni Ahmed Salim Mmoja wa wakurugenzi wa ASAS.
MNEC wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri akizungumza na Spika wa Bunge ofisini kwake wakati Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai alipotembelea kiwanda cha Maziwa cha ASAS leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akizungumza jambo huku MNEC wa CCM Mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri akimsikiliza wakati alipotembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS mkoani Iringa leo
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa cha ASAS Bw. Fuad Abri wakati akitoa ripoti ya kiwanda hicho wakati alipokitembelea na kukagua uzalishaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)