Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta (hayupo pichani) kwenye hafla fupi ya kuvikwa cheo cha Brigedia Jenerali iliyofanyika siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22, Washington, DC.Balozi Wilson Masilingi alimwagia sifa kwa kazi nzuri anayofanya kwa nidhamu ya hali ya juu, kujituma kwake na kushirikiana ndio chachu ya mafanikio yake.
Wambata wengine waliovikwa vyeo vya Brigedia Jenerali ni Brig Gen AS Nwamy- Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini India, Brig Gen AM Alphonce Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Brig Gen JJ Mwaseba- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na Brig Gen RC Ng'umbi- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini China. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production kwa hisani ya Kilimanjaro Studio.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akitoa hotuba fupi ya kumpongeza Brigedia Jenerali Adolph Mutta kwa Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akiondoa cheo cha Colonel na kumvisha cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Brigedia Jenerali AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbu wa mkutano a Nyerere hall uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimvua kofia ya cheo cha Colonel na kumvisha kofia ya cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbi wa mkutano wa Nyerere Hall.uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta akipongzwa na mkewe Agnes Mutta.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta akitoa shukurani kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkuu wa majeshi Tanzania Luteni Jenerali Venance Mabeyo. Katika hotuba yake ya shukurani alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumfikisha pale alipo na kushukuru familia yake hasa mke wake. Brigedia Jenerali AP Mutta aliwashukuri Balozi mstaafu Mhe. Liberata Mulamula na Mhe. Balozi Wilson Masilingi wakiwemo Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ushirikiano wanaompa na akaahidi ataendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha wanaiwakilisha vyema nchi yetu nchini Marekani.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi (watatu toka kushoto) na wengine toka kushoto ni EdgarMutta (mtoto wa Brigedia Jenerali Mutta), Bi. Agnes Mutta (Mke wa Birigedia Jenerali Mutta),Bi Marystela Masilingi (mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi) na kulia ni Judy Mutta (mtoto wa Brigedia Jenerali Mutta)
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto waliokaa) wengine waliokaa toka kushoto ni aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula, Bi. Agnes Mutta, mke wa Brigedia Jenerali AP Mutta na Kulia na Bi. Marystela Masilibgi mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi. Wengine waliosimama ni Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto waliokaa) wengine waliokaa toka kushoto ni aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula, Bi. Agnes Mutta, mke wa Brigedia Jenerali AP Mutta na Kulia na Bi. Marystela Masilingi mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi. Wengine waliosimama ni Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na familia yake kutoka kushoto ni Edgar Mutta, mkewe Bi. Agnes Mutta na kulia ni Judy Mutta.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na mkewe Bi. Agnes Mutta.
No comments:
Post a Comment