Friday, February 2, 2018
Thursday, February 1, 2018
Tatu Mzuka yazindua kampeni ya Valentine, ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’
• Zaidi ya milioni 300 kutolewa katika msimu huu wa Valentine
Kampuni ya mchezo wa bahati nasibu, Tatu Mzuka, leo wamezindua kampeni mpya ya Valentine, ambayo inaanza rasmi leo hadi tarehe 18 ya mwezi wa pili.
Kampeni hiyo yenye kauli mbiu, ‘Ukishinda, Unayempenda Naye Anashinda’ imelenga kuhakiksha inashamirisha msimu wa Valentine kwa watanzania kupata fursa ya kujishindia mamilioni lakini pia wawapendao pia kupata fursa ya kushinda.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, bwana Sebastian Maganga, alisema Tatu Mzuka imekuwa na utaratibu wa kuwa na kampeni zinazoendana na misimu ya sherehe za kitanzania.
‘Kwa msimu huu wa Valentine peke yake, zaidi ya shilingi MILIONI 300 zitatolewa kwa washindi wetu watakaocheza kuanzia tarehe 1 hadi 18 ya mwezi huu’ alisema Maganga.
Kama sehemu ya kampeni hiyo pia, Maganga alisema pia KILA SIKU kwa siku 18 kiasi cha MILIONI 10 zitakuwa zinatolewa, ambapo MILIONI 5 itakuwa ya mshindi na MILIONI 5 itakuwa ya mtu ambaye mshindi atamchagua.
‘Lakini pia kubwa kuliko, ukicheza kuanzia leo hadi tarehe 18 utapata pia fursa ya bure kuingia kwenye Valentine SUPA MZUKA Jackpot, ambapo mamilioni yatatolewa kwa washindi, ambapo pia mamilioni ya ziada yatakwenda kwa wanaowapenda’ alisema Maganga.
Kwa upande mwingine, Maganga aliwatambulisha Aslay na Nandy kama mabalozi wa kampeni hii, ambao pia watakuwa na matamasha makubwa katika msimu huu wa Valentine ambayo yatafanyika katika mikoa ya Tanga, Arusha na Dar.
‘Tunaomba mashabiki wetu wacheze Tatu Mzuka katika kipindi hiki, kwani wakishinda pia watapata fursa ya kuhudhuria matamasha yetu pamoja na kukaa sehemu ya watu maalumu pia watapata fursa ya kupiga picha na sisi na mambo mengine kibao’ alisema Aslay.
Akizungumza katika uzinduzi huo, msanii Nandy alisema anaamini kila mtu ana mtu anayempenda na ndio maana amefurahia kampeni hii kwani inawakumbusha watannzia misingi yetu ya upendo.
Namna ya kucheza Tatu Mzuka kipindi hiki cha Valentine ni rahisi kwa kutuma shilingi 500 hadi 30,000 kwenda namba ya kampuni 555111, na kumbukumbu namba ni namba zako tatu za bahati zikufuatiwa na neno PENDA, na hiyo itakupa fursa za kushinda kila saa, kila siku na pia kuingia kwenye SUPA MZUKA JACKPOT pamoja na kupata fursa ya kuhudhuria matamasha ya Nandy na Aslay.
Mkuu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga,akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu kampuni hiyo kuzindua kampeni mpya ya Valentine ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’ , ambayo inaanza rasmi leo hadi februari 18,2018.Pichani kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwae Nandy pamoja na Aslay (kushoto) ambao wamechaguliwa kuwa mabalozi wa kampeni hiyo
Msanii mahiri wa Muziki wa Kizazi kipya Aslay akighani moja ya wimbo walioimba pamoja na msanii mwenzake aitwaye Nandy 'subah lakheri' kama sehemu ya kionjo kwa wanahabari walioshiriki mkutano huo mapema leo jijini Dar.
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano huo
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Aslay na Nandy kwa pamoja wakiimba wimbo wao wa 'subah lakheri'mbele ya wanahabari waliofika kwenye mkutano huo mapema leo jijini Dar
Picha ya pamoja
KUMBILAMOTO AKABIDHI KIFAA CHA KUPIMIA PUMU ZAHANATI YA VINGUNGUTI
Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto akizungumza kabla ya kukabidhi kifaa cha kupimia pumu kwa watoto na watu wazima na Vifaa vya Kujifungulia katika Zahanati ya Vingunguti , ambayo Wanawake hufika hapo bila ya kuwa na Vifaa vya kujifungilia, hivyo vitaweza kuwasaidia wale ambao hawatakuwa na uwezo.
Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, akizungumza kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara baada ya kupokea Vifaa hivyo na kuvikabidhi katika Zahanati ya Vingunguti
Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto akikabidhi kifaa cha kupimia Pumu kwa Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, kwa ajili ya Zahanati ya Vingunguti.
Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto akikabidhi Vifaa vya Kujifungulia wajawazito kwa Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, kwa ajili ya Zahanati ya Vingunguti.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vingunguti, Sharif Mbulu akizungumza na kushukuru mara baada ya kupokea Vifaa kwa ajili ya Hospitali ya Vingunguti
Naibu Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamaoto na Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, wakikabidhi Mbuzi kwa ajili ya Madkatari na wauguzi wa Zahanati ya Vingunguti.
HALMASHAURI MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akivaa viatu vilivyotengenezwa katika Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za Ngozi kilichopo Senani Wilayani Maswa wakati wa Ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa pamoja na viongozi wakuu wa Wilaya ya Maswa wakielekea katika Kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa Ngozi katika Kijiji cha Senani kata ya Senani wakati wa ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akifuatilia hatua mbalimbali za utengenzaji wa viatu vya ngozi kwenye kiwanda cha kutengeneza bidhaa ngozi kilichopo Kijiji cha Senani kata ya Senani wakati wa ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Njiapanda wilayani Maswa, wakati alipotembelea eneo ambalo kitajengwa kiwanda kidogo cha kutengeneza ungalishe kitakachomikiwa na shule za Msingi 30 za Maswa,wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda vidogo wilayani humo.
………………….
Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imeshauriwa kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi ikiwemo viatu, mikoba na mikanda kinachomilikiwa na kikundi cha Usindikaji Ngozi Senani kilicho kata ya Senani wilayani Maswa, ili kuongeza thamani ya ngozi zitokanazo na mifugo.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda vidogo katika wilaya MASWA.
Mtaka amesema katika kutekeleza Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda , Halmashauri ya Maswa inapaswa kuwekeza katika viwanda vinavyoanzishwa na vikundi ili kuviwezesha katika upatikanaji wa malighafi ya kutosha, kuongeza thamani ya mazao ya mifugo pamoja na kilimo ili viwanda hivyo viweze kuzalisha kwa tija.
“Tungehitaji kuwa mkoa ambao utawekeza sana katika viwanda vidogo na ndiyo maana tulianza dhana ya Wilaya moja bidhaa moja kiwanda kimoja na sasa tunakwenda kwenye Kijiji Kimoja Bidhaa Moja Kiwanda kimoja; tunataka kupunguza uagizwaji wa bidhaa kutoka nje ya Mkoa” alisema Mtaka.Aidha, ameitaka Halmashauri hiyo kuwasaidia wanakikundi kuweka mifumo mizuri ya kutengeneza soko la bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kuuza katika minada yote ya wilaya hiyo na kuimarisha soko la nje.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko amesema Halmashauri itahakikisha kiwanda hicho kinapata malighafi ya kutosha ambapo amebainisha kuwa Halmashauri imeingia mkataba na Chuo cha DIT Mwanza kuhakikisha kuwa inazalisha malighafi(ngozi) kwa wakati kwa ajili ya kiwanda hicho.
Akiwa Malampaka ambapo alitembelea Mradi wa Ghala na Mashine ya kukoboa mpunga na kupanga madaraja, Mtaka amekipongeza Chama cha Ushirika Bumala AMCOS kwa kuanzisha kiwanda, huku akiwataka wananchi wa eneo hilo kujiandaa kiushindani katika biashara, kwa kuwa hivi karibuni Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa bandari ya nchi kavu itakayoenda sambamba na ujenzi wa Reli ya Kisasa(Standard Gauge).
“Ni lazima mjiandae kiushindani katika biashara, miaka mitatu ijayo katika Mipango ya Serikali Malampaka haitakuwa kama ilivyo, hapa ni mahali ambapo Standard Gauge ikianza bidhaa zitakuwa zikisafirishwa kwa wingi; nimeshaongea na Mkurugenzi kuwa eneo hili lipimwe na Halmashauri imiliki eneo la uwekezaji” alisisitiza Mtaka.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka alitembelea eneo la ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza ungalishe katika Kijiji cha Njiapanda, ambacho kitamilikiwa na shule 30 za Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, kinachoanzishwa kwa lengo la kuongeza kipato cha shule na halmashauri, kutoa ajira kwa wananchi na kuboresha lishe za watu.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Maswa, Mwl. Mabeyo Bujimu amesema shule za msingi 30 wilayani humo zitanufaika kwa kulima viazi lishe na kukiuzia kiwanda hicho kama malighafi pamoja na kuuza bidhaa zitakazozalishwa na kiwanda.
Huu ni mwanzo wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ambayo amepanga kutembelea viwanda vidogo vilivyopo katika wilaya zote za mkoa huo.
Klabu za Fema Hip zasema "Ukatili wa kijinsia sasa Basi"
Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akikabidhi zawadi kwa mwalimu Kahwa Mpunami wa Misungwi High ambao wameshinda (BEST FEMA CLUB OF THE YEAR 2017) Klabu Bora ya mwaka 2017 kutoka shule ya sekondari ya Myunzi Korogwe Tanga baada ya kutangazwa mshindi katika kipengele hicho katika kongamano la kujadili namna ya kupunguza ukatili wa Kijinsia kwa watoto wa kike likiwa na kauli mbiu ya "Ukatili wa Kijinsia sasa BASI" na kushirikisha Klabu mbalimbali za FEMA kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania , Kongamano limemalizika leo na lilikuwa likifanyika kwenye hoteli ya Seascape Mbezi Beach jijini Dar es salaam kwa siku nne mfurulizo, Kongamano hilo limehusisha pia mafunzo ya mambo mbalimbali. , Katika picha anayeshuhudia ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akikabidhi zawadi kwa Mayombo Lutego ambaye ameshinda (BEST FEMA CLUB MENTOR OF THE YEAR 2017) .kutoka shule ya Sekondari ya Misungwi mkoani Mwanza baada ya kutangazwa mshindi katika kipengele hicho katika anayeshuhudia ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
Upendo Abisai kutokamwanachama wa Youth For Change Project uliopo chini ya Plan International Tanzania akitoa mada katika kongamano hilo kutoka kushoto ni watoa mada wengine Lydia Charles Mtangazaji wa Kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show, Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig, Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Femina Hip na Koshuma Mtengeti Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Childrens Dignity Forum (CDF)
Koshuma Mtengeti Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Childrens Dignity Forum (CDF) akitoa mada katika kongamano hilo kutoka kulia ni Lydia Charles Mtangazaji wa Kipindi cha FEMA TV SHOW, Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig na Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Femina Hip.
Nicodemus Nangale kutoka shule ya sekondari Minaki kulia na Patrick Okilindi kutoka Shule ya Sekondari Arusha wakisoma habari iliyomhusu mmoja wa vijana kutoka Mkoa wa Mara aliyebadilisha maisha yake baada ya kumnyanayasa mke wake kwa kumpiga mara kwa mara.
Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Femina Hip akichangia mada katika kongamano hilo.
Halima Shariff Mjumbe wa Bodi ya Femina Hip akijadiliana jambo na Lydia Charles Mtangazaji wa kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show katika kongamano hilo kushoto ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
Lydia Charles Mtangazaji wa kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show na Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig wakijadili jambo katika kongamano hilo kutoka kushoto ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania na Halima Shariff Mjumbe wa Bodi ya Femina Hip.
mmoja wa wanachama wa Klabu za Fema Hip akiuliza swali kwa watoa mada wakati kongamano hilo lilikendelea.
Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Fema Hip akifafanua jambo katika kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi shule mbalimbali za sekondari nchini kutoka klabu za Fema Hip wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
Lydia Charles Mtangazaji wa kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show akihitimisha mjadala katika kongamano hilo kabla ya kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali.
Baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka klabu za Fema Hip zilizopo katika shule za sekondari hapa nchini wakiwa katika kongamano hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Femina Hip wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akizungumza na vijana mbalimbali wananchama wa klabu za Fema Hip wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Femina Hip wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
Picha mbalimbali hapa chini zikionyesha baadhi ya wafanyakazi na wanafunzi wanachama wa klabu za Femina Hip wakiwa katika picha za pamoja.
...........................................................................
Kongamano la kumi la Fema Clubs kutoka kote nchini limemalizika leo jijini Dar es Salaam likiwa limekutanisha wanafunzi zaidi ya mia moja pamoja na walimu wao. Hawa ni wawakilishi kutoka mikoa yote ya Tanzania.
Hili ni tukio ambalo shirika la Femina Hip hulifanya kila mwaka kama sehemu ya kuwaongezea uwezo vijana wanachama wa Clubs za Fema na pia walimu wao walezi, katika kutekeleza azma ya kuleta mabadiliko ya tabia na kujenga kizazi kinachozingatia mitindo bora ya maisha.
Kila mwaka kongamano huongozwa na mada maalum, na kwa mwaka huu kauli mbiu ni Ukatili wa Kijinsia Sasa Basi. Kauli mbiu hii inaakisi mkazo unaowekwa na shirika pamoja na wadau wake kupambana na matukio na tabia ambazo huwaumiza watu kwa sababu ya jinsi zao. Toleo jipya la jarida la Fema limesheheni simulizi za kweli na uzoefu wa watu ambao ama walifanya ukatili au walifanyiwa, lakini sasa wanasimama na kutuhimiza sote kuukataa ukatili wa kijinsia. Toleo hili lilizalishwa pamoja na wadau mbalimbali ikiwemo UNICEF, CDF na Plan International, na kama anavyosema Mkurugenzi Mkuu wa Femina Hip, Dr Minou Fuglesang, “Juhudi zetu hizi ni sambamba na juhudi za serikali kutokomeza ukatili dhidi ya wananawake na watoto kama zilivyoainishwa katika mpango wa kitaifa uliozinduliwa mwaka jana.”
Mafunzo na mijadala ambayo ilifanyika wakati wa kongamano hili ililenga kuwaandaa wana Fema Club kuwa vinara wa mabadiliko, kuongoza mchakato muhimu wa kuelimisha jamii zao na kuhamasisha tabia zinazopingana na ukatili huu.
Femina Hip inaamini katika usawa, usawa wa kijinsia na kwamba hakuna mwenye haki ya kumbagua au kumuumiza mtu mwingine kwa sababu ya jinsi yake, rangi au kwa kuwa ana ulemavu.
“Tunaamini katika mabadiliko, mitazamo chanya na mabadiliko ya tabia. Ni jukumu la Femina Hip kuwawezesha vijana kupata taarifa zinazoweza kuwahamasisha kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao, wakahoji mila zenye madhara na wakajenga kizazi chenye usawa na ustawi wa sasa na baadae,” anasema Amabilis Batamula, mmoja wa wawezeshaji.
Baada ya siku tatu za mafunzo na mijadala, siku ya nne ya kongamano ni siku ya kusherehekea mafanikio na kuwapongeza wale ambao walifanya vizuri zaidi mwaka jana, 2017. Tunzo zilitolewa kwa Club bora kitaifa, mwalimu mlezi bora wa club kitaifa, mtandao bora wa Club za Fema, mlezi bora wa mtandao wa Club za Fema na Club bora kwa kila mkoa.
Washindi na vipengele vilivyowapa ushindi ni kama ifuatavyo BEST FEMA CLUB OF THE YEAR 2017 ilijishindia Klabu ya MISUNGWI HIGH FEMA CLUB, MWANZA Katika kipengele cha BEST FEMA CLUB MENTOR OF THE YEAR 2017 amejishindia Bw. MAYOMBO CHARLES LUTEGO wa MNYUZI SECONDARY SCHOOL, TANGA na katika kipengele cha BEST FEMA CLUBS NETWORK imejishindia klabu ya KILIMANJARO FEMA CLUBS NETWORK na mwisho ilikuwa ni kipengele cha BEST FEMA CLUBS NETWORK MENTOR ambapo amejishindia Bw.RENATUS SANGI wa MARA NETWORK
Subscribe to:
Posts (Atom)



































