Tuesday, November 1, 2016

MATOKEO YA IKUNGI HALF MARATHON 2016 ILIYOFANYIKA TAREHE 29 OKTOBA, 2016

Washiriki wa Ikungi Half Marathon 2016 wakitimua mbio kutafuta ushindi.

WANAUME KM. 21

NA.
JINA KAMILI
UMRI
MUDA
TARAFA
KATA
BIBS NAMBA
1.
PAULO ITAMBU
25
1:08:55
MUNGAA
MUNGAA
396
2.
SAMWEL SHABANI
20
1:09:06
MUNGAA
MUNGAA
356
3.
JONAS JOHN
22
1:09:25
MUNGAA
MUNGAA
366
4.
ELIBARIKI SAIMON
29
1:10:57
IHANJA
ISEKE
338
5.
JAFARI RAJABU
26
1:11:06
IHANJA
KITUNTU
369
6.
HAMISI ATHUMANI
25
1:12:02
IHANJA
ISEKE
343
7.
SAMSON LYIMO
23
1:12:37
MUNGAA
MAKIUNGU
357
8.
MUSA JUMANNE
26
1:13:53
MUNGAA
MUNGAA
346
9.
JOHN SIMBA
23
1:15:07
IHANJA
PUMA
340
10.
EMANUEL NJOGHOMI
30
1:15:34
IHANJA
KITUNTU
339
11.
ABEDNEGO WILSON
18
1:15:46
IHANJA
MUHINTIRI
345
12.
MORIS JOSEPH
21
1:15:50
MUNGAA
NTUNTU
368
13.
ANTHON ALFONCE
27
1:15:51
IKUNGI
UNYAHATI
352
14.
JUMA NKITO
28
1:16:15
IHANJA
IHANJA
342
15.
JOSEPH CHIMA
26
1:16:18
IHANJA
MUHINTIRI
341
16.
HASHIMU HAMISI
23
1:16:19
IHANJA
KITUNTU
344
17.
HAMISI SAIDI
45
1:16:59
MUNGAA
MAKIUNGU
354
18.
LYANGA MANASE
23
1:17:07
IKUNGI
MANG’ONYI
365
19.
TELESPORI MARCO
20
1:17:18
MUNGAA
NTUNTU
367
20.
DAVID JUMA
20
1:17:58
IKUNGI
IKUNGI
397
21.
SAIDI SHABANI
21
1:18:50
SEPUKA
SEPUKA
349
22.
LEONARD PAULO
20
1:20:43
MUNGAA
MAKIUNGU
355
23.
JOSEPHATH MWAYA
28
1:21:49
IKUNGI
DUNG’UNYI
360
24.
IDD SHABANI
23
1:21:50
IHANJA
KITUNTU
370
25.
JAMES NG’WII
27
1:24:03
IKUNGI
MANG’ONYI
359
26.
ELISHA RUBENI
25
1:25:21
IKUNGI
IKUNGI
364
27.
HAJI ATHUMANI
24
1:25:44
SEPUKA
SEPUKA
350
28.
RAJABU OMARI RAMADHANI
18
1:28:42
SEPUKA
SEPUKA
348
29.
JOHN JOSEPHATH
22
1:28:47
IKUNGI
MKIWA
353
30.
OMARI MWELA
25
1:29:07
SEPUKA
SEPUKA
351
31.
ZUBERI RAJABU
19
1:29:17
SEPUKA
MTUNDURU
1682
32.
HASSANI SAIDI
23
1:29:29
SEPUKA
SEPUKA
347
33.
PHILIMON BASILI
23
1:35:59
IKUNGI
MANG’ONYI
358
34.
CHIMA GHULIKO
24
1:46:27
IKUNGI
IKUNGI
363



WANAWAKE KM 21
NA.
JINA KAMILI
UMRI
MUDA
TARAFA
KATA
BIBS NAMBA
1.
CELINA MBUA
22
1:21:45
MUNGAA
SIUYU

2.
JULIANA ALFONCE
18
1:28:19
IHANJA
IHANJA
84
3.
WITNES MUHINJO
17
1:46:20
IHANJA
IHANJA
98
4.
ZAINABU RAMADHANI
47
1;46:27
MUNGAA
MAKIUNGU
65
5.
MWANAISHA IDDI
18
1:50:04
IKUNGI
DUNG’UNYI
1228


MITA 100

WAVULANA/WANAUME                       HEAT I
NA.
JINA KAMILI
UMRI
MUDA
TARAFA
KATA
1.
FAHADI JUMA
20
12:22:01
MUNGAA
MAKIUNGU
2.
MOHAMEDI IDDI
17
12:23:57
SEPUKA
SEPUKA
3.
TUMAIN SEIF
24
12:23:68
IHANJA
PUMA

MITA 100

WANAWAKE                      HEAT I
NA.
JINA KAMILI
UMRI
MUDA
TARAFA
KATA
1.
NEEMA SAIDI
19
15:50:21
IHANJA
KITUNTU
2.
JENIFA JUMANNE
16
15:50:36
IHANJA
ISEKE
3.
ASUMAYA JUMA
18
15;50:47
IHANJA
KITUNTU



MITA 400 WANAUME – FINAL
NA.
JINA KAMILI
UMRI
MUDA
TARAFA
KATA
1.
FREDRICK DANIEL
23
1:03:10
MUNGAA
NTUNTU
2.
SAMWEL YOHANA
22
1:03:43
IHANJA
IHANJA
3.
HAMISI RAMADHANI
30

SEPUKA
SEPUKA

MITA 400 WANAWAKE FINAL
NA.
JINA KAMILI
UMRI
MUDA
TARAFA
KATA
1.
ROSEMERY BONIFACE
16
1:19:41
IHANJA
PUMA
2.
VALENTINA MICHAEL
15
1:21:50
MUNGA
LIGHWA
3.
HABIBA JUMANNE
15

IKUNGI
ISSUNA


MITA 800 WANAUME – FINAL
NA.
JINA KAMILI
UMRI
MUDA
TARAFA
KATA
1.
EMMANUEL KIEMI
25
2:29:05
MUNGAA
LIGHWA
2.
PETRO JOSEPH
24
2:29:30
MUNGAA
MUNGAA
3.
RAJABU OMARI RAMDHANI
25
2:29:47
SEPUKA
MTUNDURU

MITA 800 WANAWAKE FINAL


NA.
JINA KAMILI
UMRI
MUDA
TARAFA
KATA
1.
ELIZABETH BOMIFACE
14
2:54:44
MUNGAA
LIGHWA
2.
ROSEMARY BONIFACE
16
3:03:22
IHANJA
PUMA
3.
EVADIA GABRIEL
15

IKUNGI
UNYAHATI

WADAU WA HABARI WALIVYOSHIRIKI KUTOA MAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA ZA HABARI.


Jovina Bujulu.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatarajia kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari. Muswada huu utatoa mwelekeo na dira ya tasnia ya Habari katika utendaji kazi wake.

Kabla ya kuwasilisha muswada huu Bungeni Serikali ilipokea maoni kutoka kwa wadau wa habari, vyama visivyokuwa vya Kiserikali (NGO’s) na taasisi mbali mbali kuhusu namna na jinsi wanavyotaka muswada wa habari uwe mwongozo wa tasnia ya habari.Miongoni mwa wadau ambao walifikisha maoni Serikalini ni pamoja na Baraza la Habari Tanzania ( MCT), Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB), Tanganyika Law Society, Sikika pamoja na Nation Organization for Legal Assistance (NOLA).

Wadau wengine ni Jukwaa la Wahariri (TEF), Kituo cha Haki za Binadamu (LHCR), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Tanzania Human Rights Defenders (THRDs), Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na Taasisi ya Wanahabari Nchi za Kusini Mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN).

Baadhi ya mambo yaliyowasilishwa Serikalini na wadau hao mnamo Machi, 31, 2016 ni pamoja na kuimarisha utendaji wa vyombo vya habari nchini, kuendeleza weledi katika taaluma ya habari na kulinda usalama wa wanahabari.

Mapendekezo yao kwa kiasi kikubwa ndiyo yaliyopo katika muswada wa sheria inayopendekezwa ambao umewasilishwa ili ujadiliwe katika kamati ya Bunge na Huduma za Jamii. Kamati hii na wadau inakutana mjini Dodoma kwa sasa.Baadhi ya mambo yaliyomo katika muswada huu ni pamoja na kuunda Bodi ya Ithibati, ambayo itatoa ithibati na vitambulisho kwa wanahabari,kusimamia kanunu za maadili ya wanahabari na kuishauri Serikali katika suala la elimu na mafunzo kwa wanahabari.

Kwa kuangalia baadhi ya maoni yaliyopendekezwa na wadau, na masuala yaliyomo katika muswada huu wa sheria inayopendekezwa, yote yameegemea katika kuipa tasnia hadhi kwa kuzingatia vigezo vya weledi, maadili na elimu kwa wanahabari.Aidha, wadau waliwasilisha kuwa uwepo uhuru wa vyombo vya habari na kwamba wanahabari wawe huru kutafuta, kuchunguza na kuchapisha habari bila kuingiliwa.

Suala hili lipo katika muswada wa sheria inayopendekezwa na kwamba hakuna mwandishi ayekatazwa kutafuta na kuchapisha habari ila muswada lakini uhuru huo sio kigezo cha kuingilia sheria nyingine.Wadau hao pia walipendekeza sheria ijayo itoe fursa kwa Serikali kuendelea kusajili vyombo vya habari bila kuweka masharti , jambo ambalo lipo pia katika sheria inayopendekezwa kwamba Serikali itaendelea kusajili kwa kuzingatia kanunu, sheria na taratibu zilizopo.

Kuhusu suala la ulinzi na usalama wa waandishi , wadau walipendekeza kuwa wamiliki wa vyombo vya habari wawe na wajibu wa kuzingatia usalama wa wanahabari wanapokuwa kazini ,suala ambalo limo katika muswada wa sheria inayopendekezwa ambapo inamtaka kila mwajiri kuweka Bima na hifadhi ya jamii kwa kila mtu aliyeajiriwa katika chombo cha habari husika.

Kutokana na tasnia ya habari kukosa taasisi inayosimamia wanahabari na vyombo vya habari, muswada wa sheria hii umekuja wakati muafaka kwani endapo itapitishwa itakuwa mkombozi wa wanahabari na tasnia yenyewe. Aidha sheria hii itawapa wanahabari mwelekeo wa kazi na kujua ni mahali gani wanakosea na jinsi ya kujisahihisha. Hii ni kutokana na kuwepo kwa Baraza Huru la Habari ambalo litaandaa na kuidhinisha kanuni za maadili ya wanahabari.

Kwa wadau wa habari, ambao kwa muda mrefu wamekuwa na kiu ya kupata chombo ambacho kitaelekeza na kuongoza tasnia hii, huu ni wakati muafaka kwao kuiunga mkono muswada wa sheria hii ili upitishwe kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.Tumeona manufaa mengi ya elimu na weledi kwa wanahabari,kwa kuwepo kwa mfuko wa mafunzo ya habari, usalama wao kwa kuwataka waajiri wao kuwawekea bima. Kwa kupitisha sheria hii wanahabari watatekeleza wajibu wao kwa weledi na ufanisi zaidi.

Utaratibu wa ajira kwa watanzania wanaofanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati kuangaliwa upya

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Watanzania 5600 wanakadiriwa kufanya kazi katika kada za madaktari, walimu, wauguzi, wahadhiri, wapishi, wahudumu wa mashambani na bustani na watumishi wa nyumbani, na kati ya hao karibu watanzania 200 ndio wanaofanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati.

Kada inayofanya kazi za ndani ndio inayopata changamoto nyingi huko ugenini ikiwemo ujira mdogo na vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji. Jambo hili halipaswi kufumbiwa macho. Hata hivyo zipo jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimefanyika kupunguza ama kuondoa hali hii.

Kufanya kazi nje ya nchi bila mateso au manyanyaso ni haki ya binadamu kama inavyoainishwa katika mikataba ya kimataifa. Katika makala hii utaweza kuona baadhi ya vipengele vya mikataba hiyo.

Mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa wa mwaka 1966, unataja haki mbalimbali za kiraia zinazolindwa na mkataba huo ikiwa ni pamoja na haki ya kutopewa mateso au kufanyiwa ukatili au vitendo vya kikatili na udhalilishaji ikiwemo hukumu za kikatili katika ibara ya 7. Uhuru wa mtu na usalama wake katika ibara ya 9 na uhuru wa mtu kwenda atakako na kuchagua mahala pa kuishi katika ibara 12.

Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 17 Kifungu cha (1) kinampa haki raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kwenda kokote ndani na nje ya nchi bila kuvunja sheria za nchi. Kwa misingi hiyo watanzania wanapata fursa za kwenda nje ya nchi, hususani nchi za kiarabu kwa lengo la kufanya kazi za ndani ili kujiongezea kipato na kuweza kuinua uchumi wa familia zao na pamoja na taifa kwa ujumla.

Lakini jambo linalovutia idadi kubwa ya watanzania kwenda kufanya kazi katika nchi za Mashariki ya Kati ambazo ni Omani, Saudi Arabia, Qatar, Bahrain, Kuwait, Lebanon, Syria, Iran, Iraq na Yemen pamoja na nchi zinazounda Falme za kiarabu ambazo ni Abu dhabi, Dubai, Ajman, Al Ain, Fujuirah, Ras al Khaimah na Sharjah ni uhusiano wa karibu sana ambao ni wa kihistoria na kidamu, ambapo nusu ya familia za Oman asili yake ni Tanzania na hivyo kufanya kuwa na mwingiliano wa karibu.

Lakini pia, nchi hizi kwa kiasi kikubwa ni tegemezi ya nguvu kazi kutoka nje ya eneo hilo na hivyo kusababisha soko kubwa la ajira katika maeneo mbalimbali kama vile madaktari, wauguzi, madereva, wapishi, wahudumu wa saluni, watumishi wa shambani na hasa watumishi wa nyumbani(house maids).

Asha Abdallah (si jina halisi) mwenye umri wa miaka 25, aliacha familia yake ya mume na mtoto mmoja, na kwenda kufanyakazi za ndani nchini Omani akiamini kuwa atapata kipato kitakachosaidia kuitunza familia yake nchini Tanzania.Hata hivyo, maisha yake ya nchini Omani yameififisha ndoto yake, kwa vile imemlazimu kurudi nchini Tanzania kwa visa vilivyomkumba nchini humo.

“Nilinyanyasika mno, kazi zilikua nyingi sana, sikuwa napata muda wa kupumzika, hata chakula nilikula kwa uoga, nilipoona siwezi kuvumilia zaidi baada ya kukaa mwaka mmoja ilinilazimu kusema nimefiwa na muwe wangu ili mradi nirudi nchini Tanzania”, anasema Asha. Hadi kufikia Januari mwaka huu karibu watanzania 200 wameajiriwa katika kazi za utumishi wa nyumbani nchini Omani.

Naye, mwanamke mmoja mwenye asili ya Tanzania (jina limehifadhiwa) aliyekuwa akifanya kazi ya uwakala wa kusafirisha wasichana kutoka Tanzania kwenda kufanya kazi za ndani nchini Omani, anasema ni kweli kumekuwepo na changamoto nyingi katika kazi hiyo, na wakati mwingine changamoto hizo si za kweli ama zinakuzwa.

“Nilifanyakazi hii kwa miaka 10, nimeacha hivi karibuni baada ya kuona inakabiliwa na changamoto nyingi, baadhi ya wasichana wanasafirishwa hadi Omani na wanapofika huku wanakua hawako tayari kufanya kazi kulingana na makubaliano ya kazi yenyewe”.

Anaongeza kuwa,“Wengine wanajisahau kama huku si Tanzania na hivyo lazima waendane na maisha ya huku, hata hivyo naishauri Serikali ya Tanzania na Omani kupatia ufumbuzi changamoto zenye ukweli kwa vile hivi karibuni kumekuwepo na visa vingi kuhusu wasichana wa kazi hapa Omani”, anasema wakala huyo.

Licha ya kuwa ni kazi inayowapatia kipato watanzania hao, kumekuwepo na  malalamiko kadhaa ikiwemo mazingira magumu ya kufanyia kazi, kufanyakazi masaa mengi, kukosa mapumziko, mshahara mdogo, kufanyishwa kazi za ziada ya makubaliano pamoja na kunyanyaswa kijinsia.

Katika kupambana na hali hii Serikali imeandelea na utaratibu wake wa kawaida pamoja na kuanzisha utaratibu mpya ambao utasaidia kudhibiti changamoto mbalimbali zinazowakumba watanzania wanaokwenda kufanyakazi za utumishi wa ndani nchini Omani pamoja na nchi nyingine za Mashariki ya Kati.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima anasema Ubalozi kwa kushirikiana na wadau wengine kama Uhamiaji, Wizara ya Kazi, Wakala wa huduma za ajira Tanzania (TAESA), Kamisheni ya kazi Zanzibar, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Jeshi la Polisi pamoja na Idara ya Usalama wa Taifa wamekua wakifanya kazi kwa karibu ya kufuatilia watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi na hasa nchini Omani.

“Watanzania wanatakiwa kufahamu na kufuata utaratibu ambao unamtaka raia wa Omani mwenye nia ya kumwajiri mtanzania kuwa anatakiwa kwenda katika Ubalozi wa Tanzania na kujaza fomu ya maombi ya kumwajiri mtanzania na baada ya fomu yake kuridhiwa na Ubalozi, basi atapewa mkataba ambao atajaza na kuurudisha Ubalozi”, anasema Balozi Kilima.

Balozi Kilima anaongeza kuwa, “Mhusika anaporudisha fomu hiyo anatakiwa kuambatisha nakala ya kitambulisho cha utaifa, uthibitisho wa makazi, nakala ya pasi ya kusafiria ya mfanyakazi, hati ya kiapo na dhamana ya fedha za Omani kiasi cha rial 100”.

Baada ya Ubalozi kuridhika na vielelezo vyake, ubalozi utapitisha mkataba wa kumtaka mwajiri husika kuuwasilisha nchini Tanzania kwa mtumishi husika ambae atauwasilisha TAESA au Kamisheni ya kazi ambao nao watamhoji mhusika pamoja na kujidhihirisha kama ameuelewa mkataba na kazi atakayofanya na baada ya hapo mwajiri huyo wa kitanzania ataruhusiwa kwa kupewa kibali ambacho ni barua ya kumuomba Kamishna wa Uhamiaji kutoa ruhusa ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi baada ya kufuata utaratibu uliowekwa.

Aidha, Serikali imeweka mkazo katika hatua kadhaa katika kutatua tatizo hili, ambapo imeanza kutumia wakala rasmi wa ajira ambao wameandikishwa na mamlaka husika.Kutumia mkataba wa ajira na kuhakikisha kila Ubalozi wa Tanzania katika nchi za Mashariki ya Kati unandaa mikataba ya kazi kutokana na muongozo uliokubaliwa na wadau wote.

Vilevile, Serikali inaandaa mtaala wa kuongeza ustadi na ujuzi kwa watanzania wanaofanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati.Aidha, Balozi huyo amesisitiza kuwa nia ya Serikali ya kuanzisha mtaala huo ni katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba nazo watanzania wanaofanyakazi za ndani nchini Omani.

“Serikali imeazimia kutumia Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ili kuwa na mtaala utakaosaidia kutoa mafunzo mbalimbali ikiwemo utaratibu na utamaduni wa nchi mbalimbali wanazokwenda kufanya kazi, ili kusaidia watanzania kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu kazi husika na changamoto zake kabla ya kukubali kufanya kazi hizo,” anasema Balozi Kilima

Sambamba na hilo, Serikali imeendelea kuwataka watanzania kufuata utaratibu kabla ya kwenda kufanya kazi katika nchi hizo kwa kutumia wakala rasmi wa ajira walioandikishwa na mamlaka husika pamoja na kuwepo mkataba wa ajira unaotambuliwa na Mamlaka za nchi wanazookwenda ili kuepuka usumbufu na changamoto wanazoweza kuzipata ikiwemo kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili.




Balozi Kilima ameongoza kuwa katika kupata suluhisho la kudumu katika kuwasaidia watanzania kupata fursa za ajira nje ya nchi,Wizara kwa kushirikiana na wadau imeendelea kufanya jitihada za kusaini Mikataba ya Ushirikiano katika Sekta ya ajira na kazi baina ya Serikali ya Tanzania na nchi mbalimbali.

MWAKA MMOJA WA JPM, TRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA MAPATO.


 YAKUSANYA WASTANI WA TRILIONI 1.1 KILA MWEZI
Na JOVINA BUJULU- MAELEZO.


Novemba Tano mwaka huu ni mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi hii.

Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake, Watanzania wameshuhudia  mafanikio makubwa katika katika sekta ya ukusanyaji kodi kupitia vyanzo mbali mbali vya mapato. Hatua hii inatokana na kuwa Rais Magufuli alipoingia madarakani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna mfanyabiashara anayekwepa ulipaji kodi na kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanadai risiti kwa kila bidhaa au huduma wanayolipia.

Hivyo Serikali hii tangu ianze kazi rasmi imekuwa ikitilia mkazo ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kubuni vyanzo vipya ili kuongeza makusanyo ya Serikali.Juhudi hizi za Rais Magufuli za kuongeza mapato na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali zimejionyesha katika mikutano yake mingi ambapo mara nyingi amekuwa akisema “Ukinunua bidhaa dai risiti na ukiuza bidhaa toa risiti”.

Jitihada hizo za wa ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya kuongeza mapato ya Serikali kwa manufaa zitatekelezwa na uongozi wa Rais Magufuli zinaunga mkono wosia aliwahi kuutoa Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo alisema kuwa “Serikali yeyote isiyokusanya kodi ni “corrupt”.

Hatua hiyo ya kutoa na kudai risiti ina mchango mkubwa kwa serikali katika  kukusanya kodi ambazo zitasaidia katika kuboresha huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji, umeme, usafirishaji, ujenzi na uendeshaji wa serikali kwa ujumla kutokana na mapato yanayopatikana.

Hapa nchini, Mamlaka ya Mapato (TRA) ndicho chombo chenye jukumu la kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Taifa na imekuwa ikitimiza lengo hilo kwa kutekeleza mikakati mbalimbali kama ilivyoainishwa katika mpango mkuu wa miaka mitano.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo, katika kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wa Rais Magufuli kumekuwepo na ongezeko la makusanyo ya mapato ya serikali yatokanayo na kodi.

Anasema kuwa katika kipindi hiki, TRA inakusanya wastani wa trillion 1.1 kila mwezi kuanzia mwezi Novemba, 2015 hadi Septemba 2016.
“Hili ni ongezeko la asilimia 28.1 kutoka kwenye kukusanya wastani wa shilingi bilioni 867 kwa mwezi katika kipindi cha mwezi Novemba, 2014 hadi Septemba 2015” anasema Bw. Kayombo.

Makusanyo ya mapato katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli kuanzia mwezi Novemba 2015 yamekuwa yakiongezeka ikilinganishwa na miaka iliyotangulia kwa mfano mwaka wa fedha 2015/2016 mapato yaliyokusanywa yalikuwa shillingi trilioni 12.5 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.4 ya makusanyo ya mwaka 2014/2015. Aidha TRA imekwisha kusanya kodi kiasi cha shilingi trilioni 3.5 kufikia mwezi Septemba 2016, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.4 ikilinganishwa na kipindi kama hiki cha robo mwaka 2015/16.

Bw. Kayombo anaongeza kuwa kwa sasa TRA inatekeleza mpango mkakati wa nne wa ukusanyaji kodi wenye dhamira ya kuongeza makusanyo ya kodi za ndani kwa kuongeza ulipaji kodi wa hiari.

“Jitihada mojawapo zinazofanywa na TRA ni pamoja na kuboresha mifumo ya makusanyo inayoendana na mazingira ya sasa ya ukuaji wa teknolojia ili kuhakikisha walipa kodi wanalipa kwa urahisi kama ilivyo dhamira yake ya kurahisisha ulipaji kodi na kufanya mazingira yawe bora” anasema Bw. Kayombo. Katika kipindi cha mwaka mmoja ambao Rais Magufuli amekuwa madarakani, juhudi mbalimbali zimefanyika ili kuhakikisha matarajio ya Rais ya kuimarisha makusanyo ya kodi na kudhibiti mianya ya rushwa yanafanikiwa.

Mafanikio hayo yatamuwezesha Rais Magufuli kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni zikiwemo kuboresha afya, upatikanaji wa maji, umeme, kutoa elimu bure, ujenzi wa miundombinu kama vile viwanja vya ndege, reli na barabara. Aidha makusanyo hayo yatawezesha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa wananchi na serikali kuweza kujitegemea na hivyo kupunguza utegemezi wa misaada kutoka kwa wafadhili.

Bw.Kayombo anataja kiini cha ongezeko la kukusanya kodi kuwa ni matumizi ya mashine za kielektroniki (EFD) ambazo zinatumika zaidi badala ya stakabadhi zinazoandikwa kwa mkono. “Matumizi ya stakabadhi zinazoandikwa kwa mkono hayakuwa na ubora mzuri wa kukusanya na kuongeza mapato na kutunza kumbukumbu sahihi ambayo yaliifanya serikali ipoteze mapato mengi” anaongeza.

Katika hatua nyingine TRA ilitoa mashine za EFDs 130 bure kwa makatibu wakuu wa Wizara mbali mbali kwa ajili ya taasisi za serikali ambazo zinakusanya maduhuli ya serikali kwa nia ya kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali.


Katika kuhakikisha makusanyo ya kodi yanaongezeka TRA imeendelea kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi, kufichua wakwepa kodi, kupambana na rushwa na kupanua wigo wa kodi kwa kusajili wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa sambamba na kuendesha zoezi la kuhakiki namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) linaloendelea jijini Dar es Salaam kwa sasa ili kuboresha daftari la walipa kodi.

Pamoja na mafanikio hayo Kayombo alizitaja changamoto wanazokutana nazo katika ukusanyaji kodi kuwa ni pamoja na taarifa za kodi kutowafikia wananchi wote ili kujenga uhiari wa kulipa kodi na uwepo wa ukanda mrefu wa Pwani unaosababisha kuwepo mianya mingi ya ukwepaji kodi ambapo bidhaa huingizwa nchini kwa njia za panya.

Pamoja na changamoto hizo, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeendelea kubuni mikakati mbali mbali ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo “HAPA KAZI TU” ili kutimiza na kuvuka lengo la kukusanya shilingi trilioni 15.1 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17.

Airtel FURSA yawafungulia masoko mapya wajasiliamali wadogo wadogo jijini Dar

Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Mh Aly Hapi akikagua na kujionea bidhaa za mjasiliamali aliyewezeshwa na Airtel FURSA Bi Betty Mngulwi mwisho mwa wiki ambapo Airtel iliwakutanisha baadhi ya wajasiliamali jijini Dar es salaam katika maonyesho maalum ya ‘Airtel FURSA Wajasiliamali Bazaar’ nje ya ofisi kuu ya Airtel Morocco kwa lengo la kuwakutanisha wajasiliamali hao na wateja mbalimbali ili kuwatanua masoko yao na kuuza bidhaa zao. pamoja nae ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano wakwanza kulia.
Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Mh Ally Hapi akipokea zawadi ya keki toka kwa mjasiliamali aliyewezeshwa na Airtel FURSA Bi Diana Moshi mwishoni mwa wiki mara baada ya kutembelea banda la mjasiliamali huyo wakati wa maonyesho ya bidhaa za wajasiliamali katika maonyesho ya ‘Airtel FURSA Wajasiliamali Bazaar’ nje ya ofisi kuu ya Airtel Morocco yaliyoandaliwa na Airtel kwa lengo la kuwakutanisha wajasiliamali hao na wateja wa airtel ili kuwatanua masoko yao na kuuza bidhaa zao. pamoja nae ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano wakwanza kulia.
Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Mh Ally Hapi akiangalia picha ya mapambo ya Afrika dansi iliyochorwa na mjasiliamali aliyewezeshwa na Airtel FURSA Bi Theresia Mariatabu wakati alipotembelea banda la mjasiliamali huyo katika maonyesho ya ‘Airtel FURSA Wajasiliamali Bazaar’ nje ya ofisi kuu ya Airtel Morocco yaliyoandaliwa na Airtel kwa lengo la kuwakutanisha wajasiliamali hao na wateja wa airtel ili kuwatanua masoko yao na kuuza bidhaa zao. pamoja nae ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano na mkurugenzi Rasilimali watu wa Airtel Bw, Patrick Foya kulia.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya akizungumza katika hafla hiyo.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA mwisho mwa wiki imewakutanisha baadhi ya wajasiliamali jijini Dar es salaam katika maonyesho maalum ya ‘Airtel FURSA Wajasiliamali Bazaar’ yaliyoandaliwa nje ya kiwanja cha ofisi kuu ya Airtel vilivyoko Morocco kwa leongo la kuwakutanisha wajasilimali hao na wateja mbalimbali kwa lengo la kuwawezesha kutanua masoko yao na kuuza bidhaa zao.

Baadhi ya wajasiriamali walionufaika na mradi wao wa kijamii wa Airtel FURSA  nao walipata nafasi za kuhudhuria na kuonyesha bidhaa zao huku wakiipongeza Airtel kwa kuendelea kuwasaidia kuboresha biashara zao.

“Airtel leo wametusaidia sana sisi kukutana na wajasiliamal wenzetu tukabadilishana ujuzi pamoja na kubadilishana mawasiliano ili tuweze kusaidiana kupeana masoko, vilevile hapa katika jengo tumejipatia wateja wengi sana, hatujaamini kabisa kama tungeweza kuuza hivi, mimi nauza keki nimepata wateja hata wa baadae, kunawenzangu wanaouza Kuku, Mayai, Picha za mapambo ya nyumabani, Mito ya mapambo, Ubuyu, Matunda na Sabuni za kufanyia usafi nyumbani nimefurahi kuona kila mtu ameuza na amejitengenezea wateja wa baadae” alieleza mnufaika wa Airtel FURSA Bi Diana Mushi

Tunawashukuru sana Airtel kwa kutupatia jukwaa hili la kuonyesha bidhaa na huduma zetu kwa wadau mbalimbali na kutuongezea wigo wa soko letu. Alisisitiza Bi Diana

Akitembelea maonyesho hayo  mkuu wa wilaya ya kinondoni alieleza kufurahishwa kwake na vijana hao huku akiwahimiza vijana wengine kuanziasha biashara ndogo ndogo ili na kuzisimamia vyema ili kutengeneza ajira kwa vijana wengine wengi nchini 

“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi sana ikiwa ni pamoja na ardhi yenye rutuba, wanyama na rasilimali nyingine nyingi na bado vijana wengi wanakabiliwa na janga la kukosa ajira ambalo uwiano  wa ukosefu wa ajira kwa vijana unakua kwa kasi kila mwaka. Napenda kuwapongeza sana vijana mlioamua kujikita kwenye ujasiriamali bila kujali changamoto zilizoko katika biashara, nawatia moyo vijana wengine kuiga mfano na kujiajiri wenyewe na kukuza maendeleo ya jamii zetu” alisema Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mh Ally Hapi.

Akionge kuhusu mradi wa  Airtel FURSA Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya  alisisitiza  dhamira ya kampuni yake  kuendelea kuwawezesha vijana wajasiriamali nchini kwani wanatambua ndio chachu kubwa ya kuinua maendeleo ya jamii

“Airtel FURSA imejipanga kuendelea kuwawezesha vijana ka ili kuweza kuzikamata fursa zitakazowawezesha kufikia ndoto zao kama ilivyofanya leo kupitia maonyesho haya  ya ndani ya biashara  ya Airtel FURSA wajasiliamali Bazaar” alisema Bi Singano

Bi Singano alimalizia kusema kuwa “Airtel tunaona fahari kwa kufanikiwa kwa mradi huu ambapo mpaka sasa vijana zaidi ya 5000 wamenufaika na elimu ya ujasiriamali na kati yao zaidi ya vijana 100 waliopo katika makundi na binafsi wamewezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi ili kuongeza uzalisjhaji wenye thamani”.

Mradi wa Airtel FURSA ulianzishwa mwaka jana mwezi wa tano kwa lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali kuweza kukuza biashara zao na kuchochea vijana wengi kujikita kwenye ujasirimali kwa lengo la kuinua uchumi wao na jamii inayowazunguka, pia mradi umelenga kutoa katika elimu ya ujasiriamali kwa vijana ili kuwawezesha kujua jinsi ya kuendesha biashara na namna ya kutatua changamoto za kibiashara na kupata faida zaidi.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOV 1 2016