Thursday, January 1, 2015

TUWAKUMBUKE WAZEE WASIOJIWEZA -LULU MTEMVU

Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu, katika picha ya pamoja , Desemba 31, 2014 na baadhi ya wazee wasiojiweza wa Kambi ya Funga Funga iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu, akimkabidhi zawadi ya vyakula na mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya 2015 kwa Wazee wasiojiweza wa Kambi ya Funga Funga iliyopo Manispaa ya Morogoro, mnamo Desemba 31, 2014, zawadi hiyo ilipokelewa na Mwenyekiti wao Joseph Kaniki. ( Picha na John Nditi).

Na John Nditi, Morogoro

VIJANA wa chama cha Mapinduzi UVCCM wameshauriwa kujenga tabia ya kusaidi wazee wasiojiweza, kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwa lengo la kuwapa faraja badala ya kuachia jukumu hilo kwa serikali pekee kama  ilivyo sasa.

Kauli hiyo ilitolewa Desemba 31, 2014  na Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu,wakati alipotembelea kituo cha kuwatunza wazee wasiojiweza cha Fungafunga cha Kichangani Manispaa ya Morogoro.

Lulu  ambaye pia ni mtoto wa mbunge wa jimbo la Temeke , Abbas Mtemvu, alisema ametoa msaada wa mchele, mbuzi,sukari na sabuni za kufuria kwa wazee hao zenye thamni ya sh  milioni moja.

‘’ Pamoja na kuwa mimi ni mwanafunzi  lakini nilijikusanya kwa muda mrefu ,kwaajili ya kutoa zawadi hii ya sikukuu kwa wazee hawa ili nao waweze kufurahia katika sikuu ya mwaka mpya’’ alisema.

Hivyo alitoa wito kwa vijana nchini kujenga tabia ya kusadia wazee, wajane na watoto yatima ili kuwawezesha kuishi kwa matumaini na faraja, na kuona jamii inawathamini.

‘’ Tukumbuke pia sisi ni wazee watarajiwa, hivyo tuone ni jukumu la jamii nzima hususani viojana kusadia makundi hayo maalumu ambayo kwa hakika yanahitaji msaada’’ alisema.

Kwa upande wao wazee hao wa Funga funga walisema wamepata faraja kuona vijana  kama hao wanaona umuhimu wa kuwasaidia ili nao waweze kupata chakula hasa katika sikukuu kama hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wa kituo hicho, Mwenyekiti wao ,Josefu Kaniki, alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwapatia zawadi ya mchele Kg 400, mafuta ya kura na mbuzi.

‘’ Tunapenda kutuma salamu zetu kwa  Rais wetu Kikwete kwa kutukumbuka sisi wazee, tunamhakikishia msaada umetufikia na tumefurahia  na tunamwombe dua ili aweze kutuongoza vema kwa hekima na busara katika kipindi chake hiki" alisema Mwenyekiti  wa wazee  kituo hicho.

Pamoja na kutoa shukrani hizo, aliiomba  Serikali kuangalia uwezekeano wa kuwalipia bili ya umeme, kwani kwa sasa wamekatiwa umeme kutokana na kituo hicho kudaiwa deni la sh milioni nne.

‘’ Kwa kweli tunakula tunashiba, lakini ikishafika jioni saa 12 , wazee wote tunakosa amani, hatuna muda tena hata wa kuzungumza kama ilivyokuwa zamani" alisema na kuongeza kuwa.

" ...Inatulazima kila mmoja awahi kitandani mwake kulala na hata kwenda chooni ni  shida hasa kwa wazee wasioweza kutembea’’ alibainisha.

Kituo hicho cha Fungafunga kilichopo katika eneo la Kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro lina milikiwa na Idara ya Ustawi wa Jamii chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kina jumla ya wakazi 50, wakiwemo wazee, wajane na watoto  wasiojiweza.

DKT. SHEIN AONGOZA SIKU YA KILELE CHA MAZOEZI KITAIFA,ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza matembezi ya Siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa akiwa na Viongozi wengine yaliyoanzia katika Uwanja wa Tumbaku hadi Uwanja wa Amaan Studium leo asubuhi ambapo yamejumuisha Vikundi mbali mbali vya Unguja na Pemba.
Miongoni mwa vikundi vilivyoshiriki katika matembezi ya Siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa ni kikundi cha KVZ Fitness Group kikiwa katika hali ya ukakamavu na nidhamu ya juu wakipita katika barabara Kariakoo kuelekea Komba wapya ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyaongoza matembezi hayo leo asubuhi.
Kundi la Mazoezi Zoni C wakiwa na bango lao linalosomeka "Siku ya Mazoezi Kitaifa 01Jan 2015 Mazoezi ni Tiba Mbadala",kama wanavyoonekanwa wakiwa katika matembezi ya Siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa leo yaliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipunga mkono kama ishara ya kuyapokea matembezi ya Vijana wa Vikundi vya mazoezi katika kilele cha Siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo asubuhi (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Zabesa Mohamed Suleiman Zidi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Vikosi vya Ulinzi wakiwa katika jukwaa wakiangalia harakati za mazoezi yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium wakati wa Siku ya KIlele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Vijana wa makundi mbali mbali wakiwa katika mazoezi ya jumla leo katika Kilele cha siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Vijana wa makundi mbali mbali wakiwa katika mazoezi ya jumla leo katika Kilele cha siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika Kilele cha Siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Cheti cha Heshima kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Zabesa Mohamed Suleiman Zidi, katika Kilele cha Siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk akimkabidhi kombe la Ushindi kwa Saidi Mchande wa Zoni A ambapo imekuwa ni washindi kwa mwaka huu katika siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa sherehe zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi cheti Ahmed Ali Zoni A yenye maeneo ya Maisra-Ngazi mia katika siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa katika hafla iliyofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi cheti Zuhura Issa Khamis wa Zoni B Mwenge kwa ushiriki wao katika siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa katika hafla iliyofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi cheti Sande Kichumvi wa Kikundi cha mazoezi cha wakali kutoka Dar es Salaam kwa ushiriki wao katika siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa katika hafla iliyofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]

MBUNGE WA MOROGORO MJINI ATOA WIKI MBILI KWA MTENDAJI WA KATA KURUDISHA FEDHA ZA WANANCHI

 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiongea Kwa Msisistizo Akimtaka Mtendaji wa Kata ya Luhungo Iliyopo Mzee Makame Kai Kurudisha Fedha za Wananchi wa Kata Hiyo Shilingi Milioni 1.4 Ndani ya Muda wa Wiki Mbili lasivyo atangulie Polisi.Mh Mbunge Ametoa Kauli Hiyo katiaka ziara yake aliyoifanya kata ya Luhungo Kwajili ya Kusikiliza Kero za wananchi na Ndipo wakazi wa Kata Hiyo walipotoa Malalamiko kwa Mbunge wao Kuhusu Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata Hiyo Aliyefahamika kwa Jina la Mzee Makame Kai. Wananchi walimweleza Mbunge kuwa Mtendaji huyo amechukua fedha za Maendeleo ya Kata Hiyo Kinyume na Utaratibu na Alipotakiwa kuzirudisha amekuwa na Maneno Mengi Bila Kuzirudisha ia Kufuja Pembejeo za wakulima Ndipo Mbunge Abood Alipotoa kauli ya Kumshugulikia kwa Kumpa wiki mbili fedha za Wananchi ziwe zimerudi.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiwasikiliza viongozi wa Watendaji wa kata ya Luhungo Iliyoo Manispaa ya Morogoro mara baada ya Kukagua eneo la Ujenzi wa Shule ya Awali Ambapo Mh Mbunge Amechangia Jumla ya Shilingi Milioni 2
 Wakazi wa Kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro waliojitokeza Kumsikiliza Mbunge wao Mh Abood aliowatembelea Kusikiliza Kero zao Ambapo wakazi hao walilamikia Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata hiyo Mzee Makame Kaialiyefuja Fedha za Miradi ya Maendeleo Pamoja na Kuuza pembejeo za wakulima.

  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akipokea Taarifa za Chama Kutoka kwa Katimu wa CCM Kata ya Luhungo
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akisikiliza kwa makini Kero Mbalimbali zinazowasumbua wakazi wa kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro sambamba akiwa na Diwani wa Kata hiyo kushoto Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lugala Kulia.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akipokea Taarifa za Maendeleo kata ya Luhungo Kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa Kata Hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikagua Kivuko Kinachounganisaha Mtaa wa Majengo na Mshikamano Eneo la Lukobe Kata Ya Kihonda Manispaa ya Morogoro wakati wa Mfululizo wa Ziara zake ya Kutembelea Kata Zinazounda Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Mbunge aliahidi Kujenga Kivuko Hicho mara baad ya Kutembelea Eneo Hilo na Ndipo wakati wa Eneo Hilo walipomwomba Mbunge wao Kuwatatulia Kero ya eneo hilo muhimu inayowaunganisha wakazi wa Mitaa hiyo
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Ujenzi wa Kivuko hicho ambapo Mpaka ujenzi utakapokamilika Utagarimu jumla ya Shilingi Million 6.

SIKU YA PILI ILIVYOKUWA KWA MABALOZI WAKATI WAKIPANDA MLIMA KILIMANJARO

Majira ya saa moja asubuhi katika kituo cha Mandara ikiwa ni siku ya pili ya safari ya Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro maandalizi ya muendelezo wa safari hiyo yanaanza.
Balozi wa Tanzania katika falme za nchi za kiarabu,Mbarouk N. Mbarouk akiongoza msafara wa Mabalozi kuelekea kituo cha Horombo.
Safari inaendelea.
Balozi Adadi Rajab anayeiakilisha Tanzania nchini  Zimbabwe na Mauritius akitafakari safari ya kuelekea kituo cha Horombo.
Mabalozi Patrick Tsere (Malawi) na Balozi Batilda Burian wakivuta pumzi kwanza kabla ya kuendelea na safari.
Balozi Grace Mujuma (Zambia) akiongozana na Balozi Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Balozi Charles Sanga wakienda na mwendo wa Mdogo mdogo.
Muongoza watalii mkuu msaidizi wa kampuni ya Zara Tour,Theofiri(mwenye miwani) akiwaongoza mabalozi kuelekea kituo cha Horombo.
Mabalozi ,Waandishi pamoja na waongoza watalii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembea kwa umbali mrefu kueleka Horombo.
Safari ya kuelekea kituo cha Horombo ikaendelea kwa pamoja bila ya kuacahana.
Mahala pengine Mabalozi walilazimika kutumia fimbo maalumu kupanda maeneo ambayo yalkuwa na vipando vikali.
Mabalozi ,Shamim Nyanduga( Msumbiji) na Radhia Msuya (Afrika Kusini) walilazimika kupaka mafuta mgando katika nyuso zao ili kuzuia kubabuka na jua.
Balozo Tsere akipatiwa huduma ya kwanza ya kuchuwa mguu wake ili aweze kuendelea na safari ,kulia ni balozi Batilida Buriani.
Balozi Mwinyi aliamua kupoza koo huku akitafakari safari hiyo.
Kila mmoja aliamua kupumzika ili kuvuta nguvu ya kumalizia kipande kilichokuwa kimebakia.
Maeneo mengine mabalozi walifanya mazungumzo na wageni waliokuwa wakishuka toka kileleni.
Hatimaye Mabalozi wakafika eneo la nusu njia kuelekea Horombo na kupata chakula .
Wale waliokuwa wamepungukiwa maji waliongezewa kwa kuwa ndio dawa pekee ili kufanikisha kuwez kupanda Mlima Kilimanjaro.
Safari ikaendelea.
Hataimaye kituo cha Horombo kikaonekana kwa mbali na mabalozi walitembea na kupumzika hapo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini aliyekuwa katika msafara wa Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro.