Monday, December 2, 2013

TASWIRA MBALIMBLI ZA MCHUANO WA MISS TANZANIA USA PAGEANT ULIVYOKUA MKALI

 Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera katika picha ya pamoja na Miss Sierra Leone.
 Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera katika picha ya pamoja na aliyekua Miss District Of Columbia.
Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera katika picha ya pamoja na mchumba wake.
washindi watano wa Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi
Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera katika picha ya pamoja na familia yake.
Majaji kutoka kushoto ni Miss Sierra Leone,  Peter Walden na aliyekua Miss District of Columbia 2012.
Hellena Nyerere akikabidhiwa cheti na Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey
kwa picha zaidi zikiwemo mchuano mkali wa Mamiss Tanzania USA Pageant ulivyokuwa bofya soma zaidi ujionee mwenyewe

Aisha Kamara
Namala Elias
Doreen Rumaya
Sham Manka
Faith Kashaa
Joy Kalemera
Alice Mhina
Julia Nyerere
Hellena Nyerere
Posted: 01 Dec 2013 10:51 AM PST
 Mlimbwende Joy Kalemera akipungia mashabiki baada ya kushinda mashindano ya Miss Tanzania USA Pageant yaliyofanyika usiku wa Jumamosi Novemba 30, 2013 kwenye ukumbi wa Hollywood Ballroom uliopo Silver Spring , Maryland na Mhe. Balozi Liberata Mulamula ndiye aliyekua mgeni rasmi. Joy Kalemera alipohojiwa na Vijimambo alikua na haya ya kusema.
 Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalamera akipewa maua na aliyekua Miss District of Columbia baada ya kutangazwa mshindi kwenye Miss Tanzania USA Pageant ambapo mashindano haya ya kumtafuta Miss Tanzania USA Pageant ndiyo ya kwanza kufanyika kwenye ardhi ya Marekani. 
 Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera akiwa mwenye furaha baada ya kutangazwa mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant.
 Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akimvisha taji Joy Kalemera baada ya kutangazwa mshindi wa Miss Tanzania Pageant
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa mwenye furaha baada ya shindano hili kufana sana na kuandika historia iliyobeba ukurasa mpya wa kutangaza Tanzania kwenye mashindano haya ya Miss Afrika USA Pageant ambayo Tanzania ilikua na mshiriki wa kwanza mwaka huu ambae ushiriki wake haukupitia ngazi hii.
Joy Kalemera akipongezwa na washiriki wenzake waliokua nae kwenye kinyang'anyiro hiki kilichoanzia miezi miwili iliyopita.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa kwanza katika historia ya Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera kulia ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey.
 Joy Kalemera katika picha ya pamoja na majaji pamoja na mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant, Lady Kate (kulia)
 Kutoka kushoto ni Faith Kashaa kutoka Alabama ambaye ndiye mshindi wa tatu, Doreen Rumaya kutoka Pennsylvania mshindi wa pili, Joy Kalemera kutoka New Jersey Miss Tanzania USA Pageant, Julia Nyerere mshindi wa Tano na Namala Elias mshindi wa nne wakiwa kwenye picha ya pamoja
 Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na washiriki wenzake.
picha zingine baadae
Posted: 01 Dec 2013 09:40 AM PST
KATUUNI HII IMELETWA KWENU KWA IDHINI YA MDAU WETU MARCO TIBASIMA
Posted: 01 Dec 2013 09:25 AM PST
 Mwanamuziki Adele Clarice kutoka Cameroon akiimba nyimbo za Taifa za Marekani na Tanzania na baadae kuimba singo zake mpya alishangiliwa sana na umati wa watu alipokua kiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kwa stadi bila kupindisha kiswahili utafikiri anatoka Tegeta, Dar es Salaam.
 Mwanamuziki toka Ethiopia Betty G akitamba kwenye ukijimwaya mwaya ukumbini
 Betty G
Mwanamuzi kutoka Cameroon Naomi Achu naye akifanya vitu vyake.
Mwanamuziki na mcheza sinema kutoka Ghana Kobi Maxwell akifunga pazia la makamuzi,
 Kobi Maxwell akikamua na Adele Clarice
 Dogo Al kutoka Delaware akikamua Azonto kisawa sawa na kunogesha usiku wa Miss Tanzania USA Pageant

KINANA AKUTANA NA JAMII YA WAFUGAJI WILAYANI CHUNYA LEO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano na Jamii ya Wafugaji katika kitongoji cha Mteka, Kijiji cha Kapalala, Jimbo la Songwe, Chunya Mbeya, alipokwenda kukagua mradi wa maji kwa ajili ya mifugo na jamii hiyo. Mradi huo uliojengwa kwa fedha za Halmashauri ya Chunya  umeleta manufaa makubwa kwa jamii hiyo.
 Kinana akiwa na jamii ya wafugaji kabila la wasukuma alipowasili katika kitongoji hicho kukagua mradi wa maji wakati ziara ya kuimarisha uhuai wa CCM na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya zote za Mkoa wa Mbeya.
 Kinana akimtwisha maji mmoja wa akina mama wa jamii ya wafugaji, baada ya kuyateka kwenye bomba lililojengwa katika kitongoji hicho kilichotengwa kwa ajili ya jamii hiyo.
 Kinana akiangalia sehemu ya bomba iliyotengwa kwa ajili ya maji ya kunyweshea mifugo katika Kijiji cha Mteka, wilayani cChunya leo.
 Katibu wa NEC wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro, (katikati), akisaidia kazi ya ujenzi katika jengo la Soko la Mulugo la Mwambani, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, wilayani Chunya, Mbeya. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye abaye naye anasaidia kazi hiyo.
 Kinana akikagua bweni la wasichana la Shul ya Sekondari ya Maweni wilayani Chunya leo.
 Kinana akifitisha mlngo katika nyumba ya kuishi watumishi wa  wa Hospitali na walimu katika Kijiji cha Saza, wilayani Chunya leo.
 Mbunge wa Jimbo la Songwe, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (kushoto) akiahidi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati)kuwasaidia wasaidia wachimbaji madini  wadogo wadoko katika machimbo ya Saza, wilayani Chunya juzi. Pia Kianana amewaahidi wachimbaji hao Serikali kuwapatia vifaa vya kuchimbia madini hayo.Kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
 Nape akila chakula cha aina ya kipologwa  kinachotengezwa kwa kutumia viazi vitamu.
 Wasanii wa kabila la wabungu wakitumbuiza kwa ngoma mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, wakati wa kikao kwa balozi wa shina eneo katika Kata ya Udinde, wilayani Chunya leo.
 Mbunge wa Jimbo la Songwe, Phillip Mulugo 9kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana wakulima cha St. Marcus, msaada wa sh. 800,000. kwa ajili ya kuendeleza kilimo.
 Dk. Migiro akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Udinde leo.
Kinana akiwa na mtumbwi mdogoo alipewa zawadi na wazee wa kimila wa kabila la wabungu, kwa ajili ya  kuvulia wanachama wapya. katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Udinde, wilayani Chunya leo.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

Sunday, December 1, 2013

ASAS NA MSOWOYA WAKEMEA SIASA ZA MAKUNDI NDANI YA UVCCM MKOA WA IRINGA





 makada wa CCM wakiwa  wamembeba  juu mwenyekiti mpya wa chipukizi  mkoa wa Iringa 

 kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa  Salim Asas kushoto akimkaribisha mwenyekiti wa  chipukizi mkoa Enock Luhala mara  baada ya kutangazwa mshindi  katika uchaguzi mkuu wa Chipukizi mkoa
 Kamanda  wa UV CCM ambae  alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi  wa Chipukizi mkoa wa Iringa  Salim Asas akiwa na viongozi  wa UVCCM mkoa Tumain Msowoya  mwenyekiti wa umoja  huo kushoto na mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoa Enock Luhala kulia
 Kamanda  wa   UVCCM mkoa  wa  Iringa  Salim Asas kushoto na mwenyekiti  wa  UVCCM mkoa wa Iringa  Tumain Msowoya wakiwa wamewapakata  wajumbe  wa mkutano mkuu wa Chipukizi mkoa  wa Iringa mara baada ya uchaguzi 

NA  FRANCIS GODWIN BLOG

KAMANDA  wa  umoja wa  vijana  wa  chama  cha mapinduzi (UVCCM)  mkoa  wa  Iringa Salim Asas  amewataka   UVCCM mkoa  wa Iringa  kujipanga  vema  kujenga  chama katika  jimbo la Iringa mjini  na kuepuka  siasa  za makundi .

Asas alisema  kuwa ili  kuwa na chama imara  ni vema jumuiya  hiyo ya vijana na jumuiya  nyingine ndani ya CCM mkoa wa Iringa kufanya kazi kama  timu moja  ya ushindi  na kuepuka  kuendesha  siasa  za makundi ambazo hazina faida  ndani ya CCM.

Asas ambae  alikuwa mgeni rasmi katika  uchaguzi  wa chipukizi mkoa  wa Iringa alitoa kauli hiyo  juzi wakati wa mkutano  uliofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Iringa mjini 

Alisema  kuwa  kila jumuiya ndani ya CCM kuna  makundi isipo kuwa   Chipukizi ambao  wao  wameendelea  kuungana kwa  kuwa  kundi  mmoja  bila ya  kujigawa kama  zilizo jumuiya  nyingine.

Katika  hatua  nyingine Asas  alitaka kuanzia  sasa  UVCCM mkoa  wa Iringa  kuhakikisha  inafanya kazi kwa  kushirikiana na Chipukizi badala ya kuendelea  kuwabagua .

Alisema mara  baada ya  uchaguzi huo sasa mkoa kuandaa mpango  wa  kuwatembeza  Chipukizi bungeni , katika  hifadhi  mbali mbali za Taifa na maeneo mengine kwa ajili ya kujifunza kwa gharama  za  UVCCM mkoa .

"Hivi   jumuiya  ya wazazi  tuna makundi , vijana tuna makundi , UWT  tuna makundi ila chipukizi  wao  hawana makundi...sasa ombi langu vijana  tuige mfano  wa chipukizi kwa  kuepuka makundi na badala  yake  tuungane pamoja  kuwa kundi moja  la CCM kwa ajili ya kuimarisha  chama"

Alisema  hivi  sasa   chama  hasa  vijana wanapaswa kuungana pamoja  ili  kukijenga  zaidi  chama katika  jimbo la Iringa mjini   na kuwa  iwapo  chama kitakuwa imara  zaidi muda  ukifika  wa  kumtafuta mgombea  hata  kama atawekwa nani atashinda  kwa  kishindo badala ya  kuendesha  siasa  za makundi ambazo  zinakigawa chama.

Awali  mwenyekiti wa UVCCM mkoa  wa Iringa Tumain Msowoya  akimkaribisha kamanda huyo  wa UVCCM kuzungumza  katika mkutano  huo alisema  kuwa  mwaka  kuna  uchaguzi  wa serikali za mitaa  hivyo anachoomba vijana kujiepusha na makundi ya kisiasa .

Kwani  alisema kuwa  vijana kama kisima  cha  kutoa  viongozi  baadhi ya  wagombea  wamekuwa na tabia ya kugawana vijana ili  kuwasaidia katika kampeni na mwisho wa siku  wamekuwa  wakikigawa  chama  jambo ambalo ni hatari zaidi  katika uimarishaji  wa chama .

Pia Msowoya  aliwataka  vijana kujiandaa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya serikali za mitaa ili ikiwezekana mitaa mingi zaidi mwakani katika mkoa  wa Iringa  kuongozwa na vijana .
 
Aliwaagiza viongozi wa UVCCM kwa ngazo zote kutoa taarifa ya kuwepo kwa baadhi ya watu wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi, ambao wanataka kuitumia jumuiya yao kama njia ya mafanikio yao kiuongozi.

“UVCCM ya sasa haitakubali kuyumbishwa wala kugawanywa na mtu yeyote mwenye nia ya kuomba madaraka, itafanya kazi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa,” alisema Msowoya.

Akizungumzia uchaguzi wa chipukizi mkoani humo, Katibu wa UVCCM mkoani humo Alawi Haidar alisema umefanyika kwa amani na utulivu na kwamba, watoto hao wameweza kuwapata viongozi bora walioona wanawafaa.

Mwenyekiti  mpya wa chipukizi  mkoa Enock Meshack  Luhala mbali ya kuwashukuru  wajumbe  waliomchagua bado  alisema kuwa ataendelea  kutoa  ushirikiano mkubwa kwa chama ili kuhakikisha chama kinapata  ushindi  wa kishindo katika mkoa  wa Iringa .

 Akitangaza matokeo hayo, Haidar alisema Mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoani humo, Enock Luhala alifanikiwa kushindwa kwa kura 18 kati ya 33 zilizopigwa na kuwashinda wenzake, Ashraf Mpogole aliyepata kura 12 na Magreth Lusingo kura nne.

Katika nafasi ya mkutano mkuu wa chipukizi taifa, Junior Mlelwa alishinda kwa kura 26 na kuwabwaga wenzake, Halid Aziz na Christopher Dalu.


Wengine walioshinda ni Tausi Mgambo, Rukia Kimweli na Amina Kimweli kuwa wajumbe wa kamati ya uendeshaji mkoa.

DK.Shein mgeni Rasmi Kilele cha Siku ya Ukimwi, Paje.

 Baadhi ya wananchi walioalikwa katika hafla ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi,wakisoma majarida yaliyotolewa katika maadhimisho hayo  yaliyofanyika Paje Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 Wananchi wa Vijiji mbali mbali vya Wilaya ya Kusini Unguja,wakiwa katika hafla ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo kwa mwaka,ambapo kwa mwaka  huu Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja,yamefanyika Maadhimisho hayo na mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika Kijiji cha
Paje,Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 Vijana wa Zapha+ ni Watu wanaoishi na Virusi vinavyosababisha Ukumwi, wakifanya igozo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) pamoja na Wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini Mkoa
wa Kusini Unguja
 Bibi Fauziat Ismail Aboud, kutoka Shirika la PSI Tanzania,akisoma risala wakati wa  maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani)
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji,alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto),kuzungumza na wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani yaliyoafnyika leo katika Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani yaliyoafnyika leo katika Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja,(kushoto)  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji, na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,Dk.Idrisa Muslim Hija,(kulia)
 Wasoma Utenzi kutoka  Makunduchi,Asia Bukheti,(kulia) na Amina haji Simai,wakitoa burudani hiyo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani yaliyoafnyika leo katika Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja,mbele ya mgeni rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiiangalia picha yake wakati alipokuwa Meneja wa Mradi wa Kitengo cha Ukimwi kutoka Nov 1997- Julai 1998, wakati wa maonesho katika banda la kitengo cha Ukimwi,cha Wizara ya Afya,wakati wa  maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani yaliyoafnyika leo katika Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini
Unguja,(kulia) ni Dk.Ahmed Khatib,Kitengo cha Ukimwi
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiiangalia vifaa mbali mbali wakati alipotembelea banda la kitengo cha Ukimwi la Wizara ya Afya,wakati wa  maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani yaliyoafnyika leo katika Kijiji cha Paje,Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja,(kulia) ni Dk.Ahmed Mohamed Khatib,Meneja Kitengo cha Ukimw
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Dk.Farhat Khalid,kitengo cha Ukimwi,wakati alipotembelea maonesho katika  banda la kitengo cha Ukimwi la Wizara ya Afya,wakati wa  maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani yaliyoafnyika leo katika Kijiji cha Paje,Wilaya ya
Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja,(katikati) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na jumuiya ya Zayedesa,wakati alipotembelea mabanda mbali mbali ya maonesho yanayojishuhulisha na kutoa elimu ya Ukimwi wakati wa Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani,Kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika leo katika Kijiji cha Paje, Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja. Picha  na Ramadhan Othman,Ikulu.