makada wa CCM wakiwa wamembeba juu mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoa wa Iringa
kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas kushoto akimkaribisha mwenyekiti wa chipukizi mkoa Enock Luhala mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu wa Chipukizi mkoa
Kamanda wa UV CCM ambae alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi wa Chipukizi mkoa wa Iringa Salim Asas akiwa na viongozi wa UVCCM mkoa Tumain Msowoya mwenyekiti wa umoja huo kushoto na mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoa Enock Luhala kulia
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas kushoto na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Tumain Msowoya wakiwa wamewapakata wajumbe wa mkutano mkuu wa Chipukizi mkoa wa Iringa mara baada ya uchaguzi
NA FRANCIS GODWIN BLOG
KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Salim Asas amewataka UVCCM mkoa wa Iringa kujipanga vema kujenga chama katika jimbo la Iringa mjini na kuepuka siasa za makundi .
Asas alisema kuwa ili kuwa na chama imara ni vema jumuiya hiyo ya vijana na jumuiya nyingine ndani ya CCM mkoa wa Iringa kufanya kazi kama timu moja ya ushindi na kuepuka kuendesha siasa za makundi ambazo hazina faida ndani ya CCM.
Asas ambae alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi wa chipukizi mkoa wa Iringa alitoa kauli hiyo juzi wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Iringa mjini
Alisema kuwa kila jumuiya ndani ya CCM kuna makundi isipo kuwa Chipukizi ambao wao wameendelea kuungana kwa kuwa kundi mmoja bila ya kujigawa kama zilizo jumuiya nyingine.
Katika hatua nyingine Asas alitaka kuanzia sasa UVCCM mkoa wa Iringa kuhakikisha inafanya kazi kwa kushirikiana na Chipukizi badala ya kuendelea kuwabagua .
Alisema mara baada ya uchaguzi huo sasa mkoa kuandaa mpango wa kuwatembeza Chipukizi bungeni , katika hifadhi mbali mbali za Taifa na maeneo mengine kwa ajili ya kujifunza kwa gharama za UVCCM mkoa .
"Hivi jumuiya ya wazazi tuna makundi , vijana tuna makundi , UWT tuna makundi ila chipukizi wao hawana makundi...sasa ombi langu vijana tuige mfano wa chipukizi kwa kuepuka makundi na badala yake tuungane pamoja kuwa kundi moja la CCM kwa ajili ya kuimarisha chama"
Alisema hivi sasa chama hasa vijana wanapaswa kuungana pamoja ili kukijenga zaidi chama katika jimbo la Iringa mjini na kuwa iwapo chama kitakuwa imara zaidi muda ukifika wa kumtafuta mgombea hata kama atawekwa nani atashinda kwa kishindo badala ya kuendesha siasa za makundi ambazo zinakigawa chama.
Awali mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Tumain Msowoya akimkaribisha kamanda huyo wa UVCCM kuzungumza katika mkutano huo alisema kuwa mwaka kuna uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo anachoomba vijana kujiepusha na makundi ya kisiasa .
Kwani alisema kuwa vijana kama kisima cha kutoa viongozi baadhi ya wagombea wamekuwa na tabia ya kugawana vijana ili kuwasaidia katika kampeni na mwisho wa siku wamekuwa wakikigawa chama jambo ambalo ni hatari zaidi katika uimarishaji wa chama .
Pia Msowoya aliwataka vijana kujiandaa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya serikali za mitaa ili ikiwezekana mitaa mingi zaidi mwakani katika mkoa wa Iringa kuongozwa na vijana .
Aliwaagiza viongozi wa UVCCM kwa ngazo zote kutoa taarifa ya kuwepo kwa baadhi ya watu wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi, ambao wanataka kuitumia jumuiya yao kama njia ya mafanikio yao kiuongozi.
“UVCCM ya sasa haitakubali kuyumbishwa wala kugawanywa na mtu yeyote mwenye nia ya kuomba madaraka, itafanya kazi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa,” alisema Msowoya.
Akizungumzia uchaguzi wa chipukizi mkoani humo, Katibu wa UVCCM mkoani humo Alawi Haidar alisema umefanyika kwa amani na utulivu na kwamba, watoto hao wameweza kuwapata viongozi bora walioona wanawafaa.
Mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoa Enock Meshack Luhala mbali ya kuwashukuru wajumbe waliomchagua bado alisema kuwa ataendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa chama ili kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo katika mkoa wa Iringa .
Akitangaza matokeo hayo, Haidar alisema Mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoani humo, Enock Luhala alifanikiwa kushindwa kwa kura 18 kati ya 33 zilizopigwa na kuwashinda wenzake, Ashraf Mpogole aliyepata kura 12 na Magreth Lusingo kura nne.
Katika nafasi ya mkutano mkuu wa chipukizi taifa, Junior Mlelwa alishinda kwa kura 26 na kuwabwaga wenzake, Halid Aziz na Christopher Dalu.
Wengine walioshinda ni Tausi Mgambo, Rukia Kimweli na Amina Kimweli kuwa wajumbe wa kamati ya uendeshaji mkoa.
No comments:
Post a Comment