Monday, December 2, 2013

KINANA AKUTANA NA JAMII YA WAFUGAJI WILAYANI CHUNYA LEO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano na Jamii ya Wafugaji katika kitongoji cha Mteka, Kijiji cha Kapalala, Jimbo la Songwe, Chunya Mbeya, alipokwenda kukagua mradi wa maji kwa ajili ya mifugo na jamii hiyo. Mradi huo uliojengwa kwa fedha za Halmashauri ya Chunya  umeleta manufaa makubwa kwa jamii hiyo.
 Kinana akiwa na jamii ya wafugaji kabila la wasukuma alipowasili katika kitongoji hicho kukagua mradi wa maji wakati ziara ya kuimarisha uhuai wa CCM na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya zote za Mkoa wa Mbeya.
 Kinana akimtwisha maji mmoja wa akina mama wa jamii ya wafugaji, baada ya kuyateka kwenye bomba lililojengwa katika kitongoji hicho kilichotengwa kwa ajili ya jamii hiyo.
 Kinana akiangalia sehemu ya bomba iliyotengwa kwa ajili ya maji ya kunyweshea mifugo katika Kijiji cha Mteka, wilayani cChunya leo.
 Katibu wa NEC wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro, (katikati), akisaidia kazi ya ujenzi katika jengo la Soko la Mulugo la Mwambani, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, wilayani Chunya, Mbeya. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye abaye naye anasaidia kazi hiyo.
 Kinana akikagua bweni la wasichana la Shul ya Sekondari ya Maweni wilayani Chunya leo.
 Kinana akifitisha mlngo katika nyumba ya kuishi watumishi wa  wa Hospitali na walimu katika Kijiji cha Saza, wilayani Chunya leo.
 Mbunge wa Jimbo la Songwe, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (kushoto) akiahidi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati)kuwasaidia wasaidia wachimbaji madini  wadogo wadoko katika machimbo ya Saza, wilayani Chunya juzi. Pia Kianana amewaahidi wachimbaji hao Serikali kuwapatia vifaa vya kuchimbia madini hayo.Kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
 Nape akila chakula cha aina ya kipologwa  kinachotengezwa kwa kutumia viazi vitamu.
 Wasanii wa kabila la wabungu wakitumbuiza kwa ngoma mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, wakati wa kikao kwa balozi wa shina eneo katika Kata ya Udinde, wilayani Chunya leo.
 Mbunge wa Jimbo la Songwe, Phillip Mulugo 9kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana wakulima cha St. Marcus, msaada wa sh. 800,000. kwa ajili ya kuendeleza kilimo.
 Dk. Migiro akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Udinde leo.
Kinana akiwa na mtumbwi mdogoo alipewa zawadi na wazee wa kimila wa kabila la wabungu, kwa ajili ya  kuvulia wanachama wapya. katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Udinde, wilayani Chunya leo.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

No comments: