WAFANYAKAZI wa Bodi ya Chakula, dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDB) wakiwa katika harakati za kuangamiza vyakula vilivyomaliza muda wake wa matumizi pamoja na dawa zilizokua hazina kiwango kwa matumizi ya Binaadamu vilivyokamatwa katika maduka mbali mbali pamoja na vingene katika bandari ya Zanzibar vikiingizwa Nchini. Vyenye zaidi ya tani 40 viliangamizwa katika eneo la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Haroub Hussein).
Sunday, December 1, 2013
TAMKO LA UMOJA WA MATAWI YA WANACHADEMA MKOA WA MWANZA DHIDI YA UAMUZI HARAMU WA KAMATI KUU YA CHADEMA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI
Ndugu wanahabari, mbele yenu ni muunganiko wa wawakilishi wa matawi 189 ya chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa mwanza. Umoja huu wa matawi unawajumuisha wajumbe kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.
Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30.nov 2013 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi wetu wanaotuwakilisha kwenye vikao vya maamuzi kama vile wilaya, mkoa na taifa wamekuwa waoga na wameshindwa kuwakilisha mawazo yetu tuliyowatuma badala yake wengi wao wamekubali kuwa vibaraka wa kile kinachoitwa CHADEMA KASKAZ
Kutokana na ukweli kwamba msingi wa chama chetu na chama kingine chochote kile cha siasa, uimara na uhai wake unatokana na uwepo wa misingi na matawi ya chama, hivyo sisi wanachama wa matawi haya 189 tumeamua kuunganisha nguvu zetu kutetea chama chetu na kuhakikisha haki, heshima, katiba na maadili ya chama vinafuatwa bila ya kuogopana wala kuoneana haya.
Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-
Chadema ni chama cha siasa kinachopaswa kuendeshwa kwa misingi ya kufuata taratibu, kanuni na katiba yake na si vinginevyo. Lakini badala yake kwasasa kumeibuka ombwe kubwa kwa viongozi wetu wa juu kujitwalia mamlaka ya chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama chetu hususan katika kutoa haki sawa kwa viongozi na wanachama wa chama chetu. Kumekuwepo na upendeleo wa hali ya juu sana kwa wale wanao amini kuwa ndani ya chama hawawaungi mkono hivyo kupelekea kuwaadhibu kama ndio kinga yao ya kuendelea kuongoza bila kuhojiwa au kukosolewa.
Sababu zilizotolewa na kamati kuu hazikubaliki
Maamuzi ya kamati kuu ya tarehe 20-21 /11/2013 ya kuwavua uongozi Mh: Zitto Zuberi Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Ndg SamsonMwigamba, kumeonyesha dhahiri si woga tu wa Demokrasia bali ni unafki na Uzandiki wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu kuikwepa Demokrasia kwa kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama. Katiba yetu imeweka wazi Ibara ya 6 Kifungu cha 3 kipengele cha 6. (a – f) Mamlaka za nidhamu na uwajibishaji ndani ya chama. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi bila kufuata taratibu hizi kwa viongozi hawa, tuonavyo sisi baadhi ya wanachama huo ni umangi meza na udhalilishaji wa kibaguzi ndani ya chama kwa viongozi wetu waliotumia nguvu zao na akili nyingi sana kukijenga chama.
Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni
1. Kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za chama zinazotokana na Ruzuku ya fedha za serikali.
2. Michango ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.
3. Harambee za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
4. Kutaka kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki ambapo ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.
5. Kutaka kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao makuu ya chama ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.
Kushamiri kwa migogoro
Mwenyekiti na katibu mkuu wameshindwa kutatua migogoro ya viongozi na wanachama kutoka mikoani kwa njia sahihi za vikao na kwa wakati hivyo kutoa mwanya kwa viongozi na wanachama kutumia njia ya mitandao ya kijamii tukiongozwa na katibu mkuu mwenyewe, kujitokeza mara kwa mara kwenye mitandao hiyo hiyo kwa madai ya kutolea ufafanuzi ya mambo mbalimbali ya husuyo maswala ya chama ilihali akijua kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa chama chake, njia hiyo ya nje ya vikao ilipelekea migogoro mikubwa sana hususan mkoa wetu wa Mwanza na kupelekea kupoteza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa kwa baadhi ya madiwani, kuvunjwa uongozi wa mkoa na wabunge kuwa juu ya chama na kutumia nafasi zao kuopanga safu za uongozi wanao uwona watawatumikia wao na si chama, hivyo kusababisha mifarakano mikubwa ndani ya chama na kupelekea kuvuliwa uongozi kwa viongozi mbalimbali katika mkoa wetu kwa maamuzi yasiyo zingatia utafiti na uhalisia wa kweli ndani ya chama.
Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa vinara wa kuvunja katiba Mfano:
· Kitendo cha kutoa muongozo nje na matakwa ya katiba juu ya kuwapata wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama wabunge kwamba wanaohitaji kugombea 2015 waandike barua makao makuu na wao ndio watatoa wagombea kinyume na katiba ya chama Ibara 7.2.13 inayotoa taratibu ya kuwapata wagombea, huwo ni uvunjaji wa katiba na ubakaji wa demekrasia ndani ya chama, sizani kama kuna uhaini zaidi ya huu swali la kujiuliza hapa, Je, kama leo sisi Chadema hatuheshimu katiba yetu tuliyoitunga sisi wenyewe itakuwaje siku tukikabidhiwa nchi yenye watu wenye mawazo na mtizamo tofauti na sisi?. Hatutaki kuamini kama nchi hii inaweza kugeuka uwanja wa maopambano ya kivita.
Tunataka kujua hatua gani zilizochukualiwa dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh: Godbless Lema kumkashfu kiongozi wa chama Mh: Zitto Zuberi Kabwe kuwa ni mnafki na Mzandiki kwendye mitandao ya kijamii pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa na chama dhidi ya Bw Henry Kilewo kwa kuweka waraka unaoitwa ripoti ya siri inayomhusu Zitto mbao chama makao makuu kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama kukana mbele ya vyombo vya habari kuwa waraka huo chama hakiusiki nao na hakiujui kabisa lakini chakushangaza Bw Kilewoambaye pia ni kiongozi wa chama ngazi ya mkoa wa Kinondoni kichama, waraka huo ambao chama kiliukana yeye aliweka kwenye Blog yake ilihali akijua kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi wa chama kuhusu maadili ya viongozi kanuni ya 10.
Pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa kwa waandaaji wa tamthilia hii ijulikanayo kama Ripoti ya siri kuhusu Zitto kwasababu tayari makada na viongozi wetu wamelidhihiri kuwa wao ndo miongoni mwa waandaaji wa tamthilia hii.
Lakini cha ajabu viongozi wetu wamelifumbia macho na kupelekea kwetu baadhi ya wanachama kuamini zengwe hili la kumchafua Zitto Lina Baraka zote za viongozi wa chama ngazi ya juu.
Tunataka kuona nguvu iliyotumika kuwaadhibu Mh: Zitto na wenzake kwa kuandaa waraka ujulikanao kama mkakati wa mabadiliko 2013 nguvu hiyo hiyo itumike kwa hawa waliotumia njia chafu ya kuandaa waraka wa kumchafua zitto ambao chama kinawajua na baadhi yao tumewaweka humu kwenye tamko letu.
Kingine tunataka kwa mara nyingine kwa viongozi wa chama makao makuu kuwaambia umma wa watanzania ni kwanini waraka huo huo uinaoitwa warajka wa siri kuhusu Zitto leo viongozi na wanachama mikoani na kwenye majimbo waraka huo uangawiwa kwa wanachama na wananchi kwa agizo la makao makuu kama si ubaguzi ni nini?.
Tunaonya na kulaani kitendo cha viongozi wetu kuendeleza utawala wa kibabe na kupelekea kuhatarisha maisha ya baadhi ya wanachama na viongozi wanaotofautiana nao kimtizamo mfano: kumezuka tabia ya baadhi ya viongozi na makada wa chama chetu wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja jukwaani hivyo kujikuta muda mwingi wa kutumia maneno ya uchochezi dhidi ya wanachama na viongozi wanaokinzana nao kifikra na kimtizamo na kuhamasisha wanachama wasiojua itikadi vizuri ya chama kuwa wawashughulikie na maneno haya yamekuwa yakisemwa hadharani kwenye mikutano mbalimbali hivyo wananchi wapenda Demokrasia ya kweli kubaki na maswali magumu kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali kuhusiana na jambo hili.
Hitimisho
Mwekiti na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na matumizi ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan chi hii, M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa Demokrasia.
Mwisho tunataka maamuzi haya HARAMU kamati kuu yabatilishwe na mchakato wa kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba tofauti na hapo tarehe 4/12/2013 tutaungana na wapigania Demokrasia kote nchini kufanya maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka uongozi uliopo utoke madarakani.
Vile vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie jimbo moshi na highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.
Tunamuagiza mbowe na slaa wasithubutu kukanyaga ardhi hii ya kanda ya ziwa ikiwa bado hawajajiudhuru ama kubadili maamuzi yao HARAMU haraka iwezekanavyo
Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani ya chama chetu,
Tumekuwa wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha, tumedharirishwa kwenye chama hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye chama hiki vya kutosha,
Sasa sisi wanachadema wa matawi ya mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, tunasema kwamba kanda ya ziwa na magharibi watupo chadema kwa bahati mbaya, tupo humu kama wapokezi na waasisi wakuu wa chama hiki, tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina Marehemu Bob Nyanga Makani, Marehemu Balozi ngaiza Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, kamanda Zitto Kabwe na sisi wengine wengi.
Vyovyote itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina yoyote ya upuuzi huu unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA
ROBERT E. GWANCHELE
Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA
Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA ZIWA MAGHARIBI
Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHEREHESHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM, LEO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwai, chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Angela Ramadhan, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahi na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani, wakati alipotembelea katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA, katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na yeye kuzaliwa salama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya wanafunzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya Jukwaa Kuu, wakati Makamu alipokuwa akipokea maandamano hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
Maandamano ya Siku ya Ukimwi duniani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid, (wa pili kulia) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi moja kati ya Vitabu vya Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Alhad Mussa, baada ya ya kuzindua mpango mkakati huo wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi, Mashine za CD4 kwa ajili ya Kanda za Juu Kusini, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi. Picha na OMR
KCB BANK YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI
Kaimu Mkuu wa masoko ya rejareja wa KCB Bank, Juma Abdul akizungumzia huduma za benki hiyo kwenye semina ya siku moja ya ujasiriamali iliyoandaliwa na benki ya KCB tawi la Zanzibar kwenye hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar
Meneja wa Tawi, KCB bank Zanzibar, Cosmas Mwankemwa akizungumza na washiriki wa wa semina ya ujasiriamali iliyoandaliwa na benki hiyo kwenye hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar .
Meneja wa Tawi, KCB bank Zanzibar, Cosmas Mwankemwa akizungumza na washiriki wa wa semina ya ujasiriamali iliyoandaliwa na benki hiyo kwenye hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar
Meneja Uhusiano wa Umma wa benki ya KCB Tanzania, Hellen Siria akitoa maelekezo kwa washiriki wa semina ya ujasiriamali iliyoandaliwa na benki hiyo tawi la Zanzibar kwenye hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar
Kaimu Mkuu wa masoko ya rejareja wa KCB Bank, Juma Abdul akizungumzia huduma za benki hiyo kwenye semina ya siku moja ya ujasiriamali iliyoandaliwa na benki ya KCB tawi la Zanzibar kwenye hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar
: Mshiriki wa semina ya Ujasiriamali, Nicholaus William kutoka kampuni ya Mass Global Investments ya mjini Unguja akichangi mada katika semina hiyo Iliyoandaliwa na KCB bank mjini humo.
Mkufunzi wa Ujasiriamali, Peace Lumelezi akitoa mada kwenye semina ya ujasiriamali iliyoandaliwa na KCB Bank kwenye hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar
TAMKO RASMI PAMOJA NA TAARIFA RASMI KUTOKA CHADEMA KUHUSU KUJIUZULU KWA KWA MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI MJUMBE BARAZA KUU TAIFA BW ALLY OMARY CHITANDA

Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu A.O. Chitanda, huku pia waandishi
wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;
Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama,
Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, mjadala wake kwa upande wa chama
umeshafungwa, huku taratibu za kikatiba za ndani ya chama zikiendelea.
Pili suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa
taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni wapya;
*1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson. *2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).* *3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu. *4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema. *5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale. Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu. Kama ni suala la kuangalia mtu anatokea wapi (ambalo halijawahi wala haliwezi kuwa moja ya vigezo), ili kuonesha ukweli na kubainisha uongo wa watu wanaojaribu kufanya kazi ya CCM wakisema wao ni wanCHADEMA, kwa kutumia propaganda zile zile na kuzifanya kuwa ni kete zao za kisiasa, tunaweza kutaja maeneo ya wanakotoka au asili yao kama ifuatavyo; *Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji, Antony Komu- Kilimanjaro. *Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare- Kagera. *Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila- Dodoma. *Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John John Mnyika- Mwanza *Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema- Kilimanjar. *Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala- Morogoro. Hadi sasa uteuzi wa kurugenzi za Makao Makuu ya CHADEMA haujakamilika. Bado kuna nafasi zinazotakiwa kujazwa kwa kufuata taratibu za chama. Hii ni kwa sababu *restructuring, *inayofanyika ndani ya chama, hadi sasa inaendelea katika ngazi ya Makao Makuu na kanda, kisha itaendelea kwa ngazi za mikoa, wilaya, majimbo, kata, kijiji na hatimaye kitongoji. Katika restructuring hiyo ya nafasi za uteuzi, inayoendelea sasa ambayo inakwenda hatua kwa hatua, hadi kuwa na makatibu wa kuajiriwa ngazi ya chini ya chama, chama kinazingatia uwezo, uadilifu na utayari wa mtu katika kutoa utumishi bora kwa wanaCHADEMA na Watanzania wote katika nafasi husika. Suala la maslahi ya watumishi wa CHADEMA ni utaratibu wa chama ambao unajadiliwa, kufikiwa uamuzi na kisha kuridhiwa kwenye vikao vya chama, kama ilivyofanyika kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichoketi karibuni. Katika suala hili la maslahi ya watumishi wanaojitolea Makao Makuu ya CHADEMA ambayo si siri, Ndugu Chitanda amesema uongo mkubwa. Kwanza si kweli kuwa Ofisa Mwandamizi anaweza kulipwa posho kubwa kuliko Mkurugenzi wa kurugenzi husika. Ndugu huyo anadhihirisha uongo huo yeye mwenyewe kwa kuandika hivi; “ *800,000/=* za awali na sasa itakuwa ni kuanzia *Tshs. * *1,500,000-2,500,000/=* kwa Mkurugenzi na kutoka *Tshs. **6,800,000/=* kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni *Tshs.**1,000,000-1,500,000/=”.* Pia si kweli kuwa kila mtumishi anayejitolea Makao Makuu analipwa. Mathalani, wakurugenzi wenye nafasi za ubunge, hawalipwi hata shilingi moja kwa kazi zote wanazokitumikia chama na Watanzania kwa ujumla. Kwa maelezo hayo ya kutengeneza, ni kwamba hadi sasa Ofisa Mwandamizi anapokea posho kubwa kuliko Mkurugenzi na hata baada ya ‘restructuring’ atapata posho kulingana na Mkurugenzi. Anapaswa kuwa mkweli. Mtu anayetaka kuonekana muungwana, anapaswa kujiweka mbali na uongo pamoja, maneno ya kutunga pamoja na upotoshaji wa makusudi. Kama ilivyoandikwa hapo juu, *restructuring* inaendelea. Ni hatua kwa hatua. Itafika ngazi za chini kama Baraza Kuu lilivyoagiza. Kwa sababu hiyo hadi sasa uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya haujafanyika. Hata hivyo ruzuku imekuwa ikipelekwa kila kanda, mkoa, wilaya na jimbo kama ilivyoridhiwa na Kamati Kuu. Na hii ni zaidi ya pikipiki, kompyuta na magari yaliyopelekwa kila kanda. Angelikuwa mkweli, nagelisema na hili pia. Ndugu Chitanda anajichanganya katika taarifa yake yote. Hii ni moja ya sifa ya kukosa hoja hivyo mtu anaamua kuibua viroja au kutunga maneno kwa sababu ya kushindwa kusema ukweli. Anaonesha kuwa alikuwa mtu aliyeaminiwa hadi kuwa katika vikao muhimu, lakini wakati huo huo anasema kuna ubaguzi! Tunapaswa kumhurumia kwa kushindwa kuunganisha hata mawazo yake na kupata mtiririko wa hoja zenye mantiki! Angelikuwa mkweli angesema katika vikao vya sekretarieti na CC, aliingiaje kama kuna ubaguzi wa dini! Kwa sababu anazozijua yeye, Ndugu Chitanda ameamua kujipachika cheo ambacho hajawahi kuwa nacho. Amejiita kuwa ni Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu. Ndani ya CHADEMA pamoja na kwamba nafasi hiyo imetajwa ndani ya Katiba ya Chama, hakuna mtu ambaye ameteuliwa kutumikia nafasi hiyo. Kama anaweza athibitishe kwa kutoa barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu Mkuu. Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa CHADEMA. Operesheni ya Chama inayoendelea nchi nzima kwenye majimbo 103, si suala la siri wala lengo bovu kama anavyotaka umma uamini. Ni mwendelezo wa mpango mkakati wa chama kupitia progamu za Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), unaotekelezwa kwa hatua mbalimbali na kwa mbinu tofauti tofauti pamoja na dhana ya CHADEMA ni msingi. Operesheni hiyo ambayo ni mwendelezo wa nyingi za namna hiyo zinazokwenda ngazi za chini kabisa za chama, zikilenga kuimarisha taasisi na mifumo, imeanza wiki hii na ilitangazwa mbele ya waandishi wa habari. Tungependa kumalizia ufafanuzi huu mfupi kwa kutoa tahadhari kwa umma kuwa makini na matamko ya watu wa namna hii. Maana tunajua kwa uhakika yako mengi ya namna hii yatatokea kadri ambavyo Watanzania wanakaribia kuona na kuishi matumaini ya mabadiliko ya kiutawala na mfumo ndani ya nchi yao. Mathalani katika taarifa yake, Ndugu Chitanda amedhihirisha na kuonesha kuwa ni aina ya watu ambao wanaCHADEMA na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuwaangalia kwa macho ya kuhoji na tahadhari ya hali ya juu, anasema hivi; *“Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.” Aya hiyo pekee inayotumia lugha wanayotumia mahasimu wa CHADEMA, wakiongozwa na viongozi waaandamizi wa CCM, wanaohangaika kutokana na Watanzania kuwakataa, wakijiandaa kuwaondoa madarakani kwa sababu sera zao zimeshindwa, inatosha kuonesha uhalisia wa taarifa yake yote. Ni kauli za namna hii (kuwatisha na kutaka kuwatenganisha Watanzania) ambazo zimekuwa zikitumiwa na watawala kama njia pekee ya kutaka kuzuia upepo wa mabadiliko unaovuma nchi nzima, zimekuwa zikiwaunganisha zaidi Watanzania kuiunga mkono CHADEMA bega kwa bega, ili kupata haki na matumaini ya wanyonge, katika mapambano ya awamu ya pili, kuelekea uhuru wa kweli. Imetolewa leo Novemba 30, 2013, Dar es Salaam na; Tumaini Makene Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA*
BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA KUUNGANA NA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI SHEREHE YA UHURU CALIFORNIA NA MHE. JANUARY MAKAMBA KUWA MGENI RASMI TANZANIA UHURU NIGHT WASHINGTON, DC

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Bumbuli Mhe January Makamba

Rais wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Liberata Mulamula
---
Tiketi zinapatikana online au Piga simu kwa Dj Luke 301 661 6696, Dj Seif 202 286 6595 na Baraka Daudi 301 792 8562

Hawa ndio watakaopendezesha Uhuru Bar



Kristina Sonia Nina

Uhuru Red Carpet
VIJIMAMBO Blog inakuletea TANZANIA UHURU NIGHT siku ya Jumamosi December 7, 2013 Ukumbi wa THE FRIENDSHIP CENTER, 9055C Maier road, Laurel, MD 20723 na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba kuwa mgeni rasmiNi usiku wa Uhuru wa Tanzania, kula, kunywa mpaka unasaza kwa $60 tu na muziki ni mpaka asubuhi nunua tiketi yako mapema nafasi za kukaa ni watu 200 tu na
Mimi ni mtanzania, natoka Tanzania, nchi yangu Tanzania, MIAKA 52 ya UHURU wa TANZANIA.
TANZANIA UHURU NIGHT Itaanza saa 12 jioni (6pm) kwa COCKTAIL
Tega sikio tutazidi kuwajuza mambo mazuri yakayojiri siku hii ya Tanzania Uhuru Night
ALL YOU CAN EAT AND DRINK ALL NIGHT FOR $60 ONLY
KARIBUNI WOTE
Sheikh Kilemile: Tukilea Watoto Vizuri, Tutapata Taifa la Waadilifu
Ustaadh Ally Abrahaman Muki, ambaye ni Mwl Katika Kituo Cha Madrassa
Mukkarramah & Nursery School akitunukiwa cheti pamoja na vifaa vya
Kufundishia na Mgeni Rasmi Sheikh Suleiman Amran Kilemile vilivyotolewa na
Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kituo
hicho Jana.
Kiongozi wa Kikundi cha Kinamama cha Ahbaabur Rasuul, Ukhty Samia
akipokea zawadi ya Jola ya Kitambaa kama sehemu ya Uwezeshwaji kiuchumi kwa
akina Mama uliotolewa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation kwa ajiri ya
unifomu za Wanafunzi wa Kituo Hicho.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation
walipokuwa katika picha ya Pamoja na wanafunzi wa Kituo cha Madrassa Mukarramah
& Nursery School kilichopo Kipala Mpakani – Mkuranga, Pwani.
Sehemu ya Nyumba ya Mwalimu wa Kituo Cha Madrassa Mukarramah &
Nursery School kabla ya Kupata Ufadhili wa Kuiboresha kama inavyonekana hapa
chini kwa kuwa ya Kisasa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation.
Sehemu ya Nyumba ya Mwalimu wa Kituo Cha Madrassa Mukarramah &
Nursery School baada ya Kupata Ufadhili wa Kuiboresha kama inavyonekana hapa
chini kwa kuwa ya Kisasa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation.
Ustaadh Ally Abrahaman Muki akiwa katika sehemu ya Mapumziko na wageni
ya Nyumba mpya iliyofadhiliwa na taasisi
ya Kalamu Education Foundation ili kuongeza ufanisi katika ufundishaji maadili
mema kwa watoto na Vijana.
Sheikh Suleimani Amran Kilemile Akifanya Uzinduzi wa Kituo cha kisasa
cha Madrassa Mukarramah & Nursery School Kilichopo Kipala Mpakani-Mkuranga
Pwani.
Madrasa
Kutoka Kulia, Sheikh Suleiman A. Kilemile Mwenyekiti wa Umoja wa
wanazuoni wa Kiislam Tanzania, Ustaadh
Ally Abrahaman Muki wa Madrassa Mukarramah & Nursery School na
Sheikh Ally Mbwela wakiwa pamoja na Akina mama wa kikundi cha Ahbaabur Rasuul
cha Madrassa Mukarramah & Nursery School wakati wa Uzinduzi wa Kituo hicho.
Sheikh Suleiman Amran Kilemile wakifurahia jambo na Ustaadh Ally
Abrahaman Muki na Mwl Ally Mbwela muda mfupi baada ya uzinduzi wa Madrassa
Mukarramah & Nursery School Mkuranga Pwani kilichojengwa na Kalamu
Education Foundation. Sheikh Kilemile alikuwa mgeni Rasmi katika shughuli hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa Madrassa Mukarramah & Nursery School ya
Mkuranga, Pwani wakiwa wenye matumaini makubwa baada ya Kupata Kituoa cha
Kisasa cha Elimu ya Dini na Shule ya Awali.
1. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania Sheikh Suleiman
Amran Kilemile akisisitiza Umuhimu wa Kuwapa Malezi bora watoto ili kujenga
Taifa la watu waadilifu na wenye utu
wakati wa uzinduzi wa Kituo Cha Madrassa
Mukarramah & Nursery School Kipala-Mpakani,
Mkuranga Pwani Kilichojengwa na Kalamu Education Foundation.
Ziara ya Kinana Wilayani Chunya, mkoa wa Mbeya
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akiruka kwenye moja ya
maeneo yanaotengenezwa kwenye barabara hiyo, inayopita kwenye safu ya milima,
wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo inayotengenezwa na kampuni ya kichina ya
CCCC. Nyuma yake ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana mbaye pia aliruka
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akikagua ujenzi wa
barabara ya lami ya eneo la kilometa 30 kutoka Mbeya hadi Chunya, wakati
msafara wake ulipopita katika barabara hiyo ukienda Chunya, akiwa katika ziara
ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na
kujaduiliana nao njia za kuzitatua mkoani Mbeya, Nov 30, 2013. Kulia ni Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na watatu ni Katibu wa NEC Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro anaofuatana nao kwenye ziara hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipandisha bendera kuzindua shina la wajasiriamali wa CCM, katika kituo cha mabasi cha mjini Chunya, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya, Nov 30, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi baada ya kuzindua shina la wajasiriamali wa CCM, katika kituo cha mabasi cha mjini Chunya, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya, Nov 30, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza Kijana, Frank Mwapololo, ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo katika machimbo ya mafunzo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, yaliyopo Chunya, alipozungumza na wajasiriamali wa mradi huo, Nov 30, 2013, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wapili kulia) akimrekebishia sawasawa vazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, baada ya wazee wa Kata ya Lupa, wilayani Chunya, kumvalisha vazi la wazee wa Kata hiyo, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya, Nov 30, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi mashine isiyotumia umeme, ya kufyatulia matofali, kwa kikundi cha wajasiamali, wakati wa mkutano wa hadhara aliofanya Nov 30, 2013, katika Kata ya Lupa, wilayani Chunya, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya, Nov 30, 2013. Wengine ni Mkuu wa mkoa huo, Abbas Kandoro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Picha zote na Bashir Nkoromo
Subscribe to:
Posts (Atom)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)