Monday, July 1, 2013

MAANDALIZI YA MAPOKEZI YA OBAMA YAKAMILIKA, TASWIRA ZA IKULU ASUBUHI HII

Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda mswano, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki. 
Bendera zikiwa zimepangwa na kupangika katika upande wa lango kuu la Mashariki,Ikulu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama.
Jengo la Ikulu.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akisoma ratiba.
makundi ya wananchi wa Dar es salaam walikishangilia wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipopita kuwasalimia.PICHA NA IKULU.

NIPO TAYARI KUUTUMIKIA UMOJA WA MATAIFA –LUTENI JENERALI MELLA

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akiwa na Mkuu mpya ya UNAMID Luteni Jenerali Paul Ignace Mella na kulia ni Luteni Jenerali Wynjones Mathew Kisamba Naibu Kamanda na ambaye pia alikuwa akikaimu nafasi ya Kamanda Mkuu UNAMID. Luteni Jenerali Mella na Luteni Jenerali Kisamba walikuwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ziara ya Kikazi na mafunzo. Lt. Jenerali Mella anasema yupo tayari kulitekeleza jukumu alilokabidhiwa na Umoja wa Mataifa na kwamba uteuzi wake katika wadhifa huo ni heshima kubwa wa Tanzania, Afrika, kwake yeye binfasi na zaidi kwa JWTZ ambayo mwaka itakuwa inatimizia miaka 50 tangu kuanzishwa kwake
Mkuu Mpya wa UNAMID Luteni Jenerali Mella akiwa katika picha ya pamoja na waambata wa kijeshi kutoka nchi za Afrika na kwingineko wakati alipotambulishwa kwao katika hafla fupi iliyoandawali na Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. kutoka kushoto ni Naibu Mwakilishi Balozi Ramadhan Mwinyi, Lt. Jenerali Wynjones Kisamba, Balozi Tuvako Manongi, Lt. Jenerali Paul Mella na Maj. Jenerali Ngodi Mkuu wa jeshi la kulinda amani huko Lebano (UNFIL).
Mkuu mpya wa UNAMID, Luteni Jenerali Paul Mella akibadilishana mawazo na Kanali Mike Redmond ambaye ni Mwambata Jeshi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa.
Luteni Jenerali Mella akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa mataifa, wamo pia Balozi Tuvako Manoni, na Luteni Jenerali Kisamba.


Waambata Jeshi kutoka kushoto Kanali Mike Redmond ( UK) Luteni Kanali Tiffany Harris ( mwanadada) Naibu Mwambata Jeshi( Marekani), anayefuatia ni Mwabata Jeshi wa Kenya na Mkuu wa UNAFIL.

Na Mwandishi Maalum

Ni heshima kubwa kwa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni heshima kubwa kwa Afrika, ni heshima kubwa kwangu mimi binafsi, lakini kubwa zaidi ni heshima kubwa kwa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambalo mwakani litakuwa linatimiza miaka 50 tangu   kuanzishwa kwake.

Hiyo ni kauli  ya  Luteni  Jenerali Paul Ignace Mella,   Mkuu  mpya wa Jeshi la kulinda Amani la Umoja wa Mataifa  katika Jimbo la Darfur (UNAMID)
Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki,  wakati wa  hafla fupi iliyoandaliwa na  Uwakilishi wa Kudumu  wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  kwa madhumuni ya kumtambulisha  Mkuu huyo mpya wa UNAMID kwa   Waambata wa Kijeshi hususani wa  Kiafrika na wengineo  walioko  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Aidha hafla hiyo ililenga pia kutambua mchango mkubwa na wa kutukuka wa Naibu Kamanda na ambaye pia amekuwa akikaimu  nafasi ya  Kamanda Mkuu wa UNAMID Luteni  Jenerali Wynjones Mathew Kisamba naye  kutoka JWTZ.

Akizungumzia uteuzi huo ambao ulitangazwa hivi karibu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon.  Luteni Jenerali Mella amesema pamoja na heshima kubwa kwa nchi yake, kwa Afrika na JWTZ, lakini pia anasema anatambua fika changamoto  na jukumu kubwa  lililombele yake, jukumu la kuwalinda wananchi wa Jimbo la Darfur na kurejesha amani ya kudumu kati ya pande zinazopingana.

“Ni jukumu kubwa  lenye changamoto nyingi, lakini nimejiandaa kulikabili na kuzikabili changamoto zilizo mbele yangu nipo tayari kuutumikia  Umoja wa Mataifa” anasema Luteni Jenerali Mella.

Na   kuongeza “ Dhamana kubwa ya jeshi la  kulinda amani katika Darfur ni kuhakikisha usalama unapatikana wakati wote hususani kwa  wananchi wasiokuwa na hatia na vilevile kwa  Mashirika ya Kimataifa yanayopeleka misaada ya kibinadamu kwa wananchi hao. Pamoja na kuendeleza majadiliano ya kutafuta amani na kuhakikisha kwamba makubaliano  yanapatikana na yanadumishwa kati ya pande zinazopigana”.

Mkuu huyo  wa UNAMID alikuwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ziara ya mafunzo na maandalizi ya kuanza  jukumu lake, ambapo pia alihudhuria  kikao cha pamoja cha Makamanda wa Misheni zote za Ulinzi wa amani chini ya Umoja wa mataifa. Kikao hiki hufanyika   New York  kila mwaka.

Akizungumzia kuhusu mafunzo waliyopewa,  Luteni Jenerali Paula Mella, anasema  mafunzo waliyopewa pamoja na mambo mengine, yalihusu mafunzo ya ukaguzi na uthibitishaji wa weledi, utayari na  utimamu  wa wanajeshi wanaopelekwa kulinda amani  kupitia Umoja wa Mataifa.

Amefafanua zaidi kwa kusema kwamba  wanajeshi wanaopelekwa  katika misheni za kulinda amani wanapitia hatua mbalimbali za mafunzo ya  kuthibitisha weledi wao, utayari na utimamu. Mafunzo , ukaguzi  na uthibishaji wa kwanza   unafanyika kwanza  katika nchi yao wanakotoka na pili  yanafanyika  wakisha fika katika  kituo  cha   kazi.

Aidha akasema, katika mafunzo hayo pamoja na mkutano walioufanya,  matumizi ya teknolijia za kisasa katika misheni za ulinzi yalisisitizwa sana.
Teknolojia ambazo Umoja wa Mataifa  umeamua kuanza kuzitumia katika baadhi ya maeneo  kwa lengo la  kuimarisha ulinzi wa raia na kuboresha operesheni za ulinzi  ni pamoja na ndege ambazo haziendeshwi na rubani (unmanned aerial systems ).

Akifafanua zaidi kuhudu teknolijia hiyo ya kutumia ndege ambazo hazirushwi na rubani ,  Mkuu   huyo wa UNAMID anasema  matumizi ya teknolojia hiyo ni muhimu sana hasa katika ukusanyaji wa taarifa za kitelejensia,  na kutambua mwenendo wa makundi ya wanamgambo wenye silaha.

“ Hii ni  teknolojia muhimu sana kwanza, kwa sababu inauwezo wa kukusanya habari na pili kupiga picha  ya nini kinachoendelea katika eneo fulani,na kwa kutumia zana hii itasaidi sana katika kuyadhibiti makundi yenye silaha na hivyo   kuwa na uwezo wa kuwalinda wananchi  dhidi ya hatari ambayo inaweza kuwakabili.

Vilevile ameeleza kwamba katika mafunzo hayo, wakuu wao wa  majeshi ya  kulinda amani walifundishwa umuhimu ya kuwa karibu na vyombo vya habari.

“ Tumejifunza mengi kwa kweli, likiwano hili la uhusiano wetu na vyombo vya habari, hili ni jambo ambalo pia limepewa msisitizo wa aina yake, kwamba tunapashwa, katika utekelezaji  wa majukumu  yetu kufanya kazi kwa karibu na vyombo vya habari” anasema Luteni Jenerali Mella.

Awali akimtabulisha  Mkuu  huyo  mpya wa UNAMID  kwa waambata jeshi hao,  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, aliomba ushirikiano kutoka  kwa waambata jeshi hao na serikali zao.

Akasema ingawa nafasi  hiyo  amepewa mtanzania lakini wanajeshi wanaounda  UNAMID wanatoka katika nchi mbalimbali zikiwamo za Afrika kwa hiyo heshma hiyo ilikuwa ni ya waafrika wote na kwamba mafanikio ya  UNAMID ni mafanikio ya  Afrika,  ni mafanikio ya Umoja wa Mataifa na ni mafanikio ya wapenda  amani na kubwa zaidi kwa amani, usalama na ustawi wa ni wananchi wa Sudan hususani jimbo la Darfur.

Lt. Jen. Paul Ignace Mella, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Lt. Jenarali Patrick Nyamvumba kutoka Rwanda ambaye amestaafu Marchi 31, 2013. 

Jeshi la  kulinda amani la UNAMID linahudumiwa na  watu wa kada za aina mbalimbali wapatato 19,148 . Kati yao vipo  vikosi vya kijeshi vyenye wanajeshi 14,055, wangalizi wa kijeshi  342 ( Military  Observers), Polisi 4,721, wafanyakazi wa kimataifa  1,077 , wafanyakazi wenyeji ni   2,924    na 448 ni wafanyakazi wa kujitolea  kutoka Umoja wa Mataifa.

SPERANSIA MHONDELE NI BINTI WA MIAKA 18 MWENYE NDOTO LA KULITANGAZA TAIFA KISOKA


Mwanadada  mkali  wa soka  Iringa na mikoa ya nyanda za juu  kusini Speransia Mhondele  akionyesha uwezo wake  kisoka

Hapa  aklionyesha jinsi ya  kutuliza mpira  kwa gamba
Akionyesha mbinu ya  kumkabili  adui  kwa mpira  wa angani
Hapa  akijiandaa kuondoka na mpira  baada ya  kuutuliza  kutoka hewani

Timu ya  watuma  salam mkoa wa Iringa ambayo  binti Speransia ( wa pili  kushoto waliosimama) alipata  kuonyesha soka la uhakika  jana wakati wa mchezo wa kirafikin kati ya  watangazaji wa radio  Furaha Fm na  watuma  salam mchezo uliomalizika kwa  watangazaji  kushinda  baada ya kuigagadua timu ya  watuma  salam mabao 2-0
.......................................................................................
Spransia  Evaristo Mhondele ni  binti  wa miaka 18  mkazi  wa Kihesa katika manispaa ya Iringa mwenye  kipaji  cha hali ya  juu katika mchezo  wa mpira  wa  miguu mwenye ndoto  za kuj kulipa heshima  kubwa Taifa la Tanzania  katika soka la  wanawake .
“mimi nilihitimu masomo yangu ya  sekondari mwaka 2012 katika  shule ya  sekondari Mlamke katika Manispaa ya  Iringa na  nimepata  kuchaguliwa kujiunga na timu  za UMISETA katika mchezo wa  soka wanawake “
Nilianza  kucheza mpira  mwaka mwaka 2010 nikiwa katika mashindano ya UMISETA  yaliyofanyika katika Ifunda kwa wilaya ya  Iringa  ambako nilikwenda  kushiriki mchezo  wa Basketi  .
Baada ya  kufika  huku nilikuta kuna ushindani mkubwa katika mchezo huo ambao  nilichaguliwa na  hivyo baada ya   kuchujwa  wengi nikiwemo mimi katika mchezo huo  ndipo  nillipoamua  kubadili mchezo na  kuanza kucheza mchezo wa mpira wa  miguu kwa  kufanya mazoezi .
Nilifanya mazoezi  usiku na mchana na baada ya mashindano mengine ya  UMISETA ndipo nilipoamua  kuelekeza  nguvu  huko na kujiunga kabisa katika timu ya mpira wa miguu ya  wanawake .
Kujiunga kwangu na  timu ya  mpira  wa  miguu wanawake  kuniliwezesha  kupita hatua kwa  kuchaguliwa  kuwakilisha  mkoa  wa Iringa katika mashindano ya kanda ya  kusini  kwa  kuelekea  mkoani Ruvuma kwa mara  ya kwanza kufika katika mkoa  huo na baada ya kufanya vizuri huko  nilichaguliwa  kuwakilisha kanda  ya kusini katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani .
“ Jitihada  binafsi nilizoonyesha  na  wachezaji wenzangu  tuliiwezesha  timu  yetu  kutoka  kanda ya nyanda za juu kusini  kushika nafasi ya  tatu kitaifa “
Mchezaji  huyo anadai kuwa  ndoto yake  kubwa katika soka  kuja kuchezea timu  kubwa  za  kitaifa ili   kuweza  kuonyesha uwezo  wake  zaidi .
“Kwa  sasa  nasuburi  ruhusa ya  mzazi  wangu  ili  kuweza  kuniruhusu   kujikita  zaidi katika michezo  ili  kuweza  kutafuta  fursa ya  kulitumikia  Taifa  langu  Tanzania katika michezo …..nilishindwa  kujiunga na  timu  za  wanawake  nje ya mkoa  kutokana na  wazazi  kunizuia kutokana na  wakati huo  nilikuwa masomoni “
Spransia  anasema  kuwa  katika maisha  yake wakati akiwa  shule  kwa sehemu  kubwa alikuwa akiwaza  michezo zaidi  na  hasa  kuwa na ndoto ya  kuja  kuchezea timu kubwa za  mpira  wa miguu kwa  wanawake na yawezekana  hata kufeli kwake  kulitokana na mawazo ya  michezo .
Hata  hivyo anasema  kuwa kati ya mambo ambayo katika maisha  anaona  bado  kufanikiwa na hana ndoto ya  kukimbilia  kuolewa  wala katika  mahusiano na  wanaume kwa sasa ni kutokana na  kutotimiza  azma yake ya  kuchezea  timu  kubwa ya  soka  wanawake  nje ya  mkoa  wa Iringa .
Kwani amesema katika mashindano ya  UMISETA kwa jitihada  zake binafsi amepata  kuifungia  timu yake magoli matatu na  kuwa kwa  sasa baada ya  kuhitimu  elimu ya  sekondari amepata kuchezea  timu mbali mbali kama  Kwa kilosa FC , Sengo FC na  timu  ya  watuma  salam mkoa  wa Iringa  wanaume ambapo kwa upande upande wa  Sengo Fc nimepata  kufunga magoli mawili .
Pia  amesema  kuwa anaomba  chama  cha mpira  wa miguu  wanawake  Taifa  iwapo  kuna  nafasi ya  kusajili  wachezaji  wapya  kuweza  kumtazama hata  kumpa nafasi ya majaribio  ili aweze  kuonyesha kipaji chake .
Code hizo
Mwandishi  wa makala  haya  alipata  kushuhudia kandanda safi iliyoonyeshwa na mchezaji  huyo  Speransia wakati  wa mchezo wa kirafiki kati ya  timu ya  watuma  salam mkoa  wa Iringa na  timu ya  watangazaji  wa kituo cha  radio Furaha  Fm ambapo mchezaji Speransia  alipata  kuchezea timu ya  watuma salam na  kuwa binti  pekee katika  timu  hiyo  ya  wanaume  ila aliweza  kuwahenyesha  watangazaji wa radio  Furaha Fm japo  ndio  iliyoweza  kushinda kwa magoli 2-0 dhidi ya  watumasalam
Mwandishi  wa makala  haya ni milimiki wa mtandao  wa www.matukiodaima.com
anapatikana kwa simu 0754 026 299 au 0789 281030 barua pepe mailto:francisgodwin2004@yahoo.com%3C/span%3E%3C/div>

REDD’S MISS MOROGORO 2013 AJIONGEZEA TAJI LA KANDA MASHARIKI.

Habari na Picha na John Nditi, Morogoro
MWANAFUNZI wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Ulinzi wa Jamii kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM), Diana Laizer (21) amefanikiwa kunyakua taji la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki baada ya kuwashinda wenzake 12 walioshiriki kuwani taji hilo mwaka 2013. 
 Mshindi huyo ambaye pia ni malkia wa taji la Redd’s Miss Morogoro 2013 akiwa amevalia namba sita ya ushiriki ,amefanikiwa kuchukua mikoba ya mtangulizi wake Rose walifanikiwa kunyakua taji hilo juzi usiku katika ukimbi wa Nashera Hoteli wa Mjini hapa baada ya kutangazwa na majaji wa shindano hilo. 
 Jaji Mkuu , Albert Makoye ambaye ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, mbali na kumtangaza malkia wa Kanda ya Mashariki , alimtangaza pia mshiriki kutoka mkoa wa Morogoro Sabra Islam (19) kushika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro hicho. 
 Sabra aliingia kwenye shindano hilo baada ya kushika nafasi ya pili katika shindano ya Redd’s Miss Morogoro 2013 ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu huyo, mshindi wa tatu wa Redd’s Miss Kanda ya Mashairiki ilitwaliwa na mrembo Janeth Awet ( 19) kutoka Mkoa wa Lindi na nafasi ya nne ilinyakuliwa na mrembo Elizabeth Perty (22) kutoka Mkoa wa Pwani. Makoye alisema kutokana na washiriki wa kinyang’anyiro hizo Kanda ya Mshariki kuwa na warembo karibu wote wenye sifa na vigezo, 
Kamati ya Miss Tanzania imeamua kuwachukua washiriki wanne kuingia katika kambi ya shindano ya Miss Tanzania mwaka huu. Hata hivyo alimtaja mwingine aliyeingia tano bora ni Ivon Stephen (22) kutoka Mkoa wa Mtwara , ambapo wengi walioshiriki na mikoa yao katika mabano ni Zulfa Semboja (19) ( Mtwara) na Pulkeriah Ndovi (21) ( Mtwara). 
 Wengine ni Sophia Maganga (21), Lindi, Zainabu Shaaban (23) (Lindi), Lilian Joseph (21) ,(Pwani ) Easther Albert (20) ( Pwani), Muzne Abduly ( 19) na Ummy Mohamed (21) wote ni kutoka Mkoa wa Morogoro. Naye Mratibu wa Shindano hilo, Alex Nikitas, aliwakabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza sh: 600,000, Mshindi wa pili sh: 400,000 na mshindi wa tatu sh: 300,000 , ambapo mshindi wanne na watano walipatiwa sh: 200,000 kila mmoja na wengine waliobakia kusawadiwa sh: 100,000 kila moja.
 Katika shindano hilo, Mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Kilosa , Mustafa Mkulo na pia kuhudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo na Mbunge wa Jimbo la Gairo , Ahmed Sabiby pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Jaji Frederick Werema ambapo pia mwanamuziki wa kizazi kipya Tunda Man walitumbuiza likiwemo na kundi la sanaa la Wanne Star.
 Baadhi ya wacheza shoo wa mwanamuziki wa kizazi kipya , Tunda Man, wakiongesha ujuzi wao mbele ya watanzamani hawapo pichani.
 Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, wakiwa katika vazi la jioni
Mshindi wa nne , Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, Elizabeth Perty kutoka mkoa wa Pwani akipita jukwaani akiwa na vazi la ubunifu.
Furaha ya ushindi na zawadi.

 
MC katika shindano la kumpata malkia wa Taji la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Kaka Aidan Ricco ambaye ni Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania  akielezea utaratibu wa kuwapata washindi watano


 Mshiriki Zulfa Semboja kutoka mkoa wa Mtwara akionesha vazi la ubunifu mbele ya watazamaji
Washindi wanne wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013 wakisubiri Jaji Mkuu kutaja majina yao katika nafasi ya ushindi kuanzia kwanza, pili , tatu na ya nne

 Mwanamuziki wa Kike wa kizazi kipya, Keisha ( wa kwanza kulia) akipiga makofi kufurahiamchuano wa warembo wa Redd's Miss Kanda Mashariki , Juni 29, mwaka huu
 Mshindi wa Taji la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2013, Mwanafunzi  wa mwaka wa kwanza wa  Shahada ya Ulinzi wa Jamii  kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM) ambaye pia ni Malikia wa Taji la Mkoa wa Morogoro  Diana Laizer (21) ( kati kati) akiwa na wenzake mshindi wa pili  , Sabra Islam (19) ( Kushoto) pia kutoka Mkoa wa Morogoro pamoja na mshindi wa tatu Janeth Awet ( 19) kutokaMkoa wa Lindi  mara baada ya kutagazwa Juni 29, mwaka huu  kuwa washindi.
 Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013 yenye taji kishwani akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wenzake waliokuwa wameingia tano bora.
 Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, Diana Laizer akifurahia kitita cha fedha alichokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mustafa Mkulo baada kutangazwa mshindi.
 Redd's Miss Morogoro , Diana Laizer ( kushoto) pamoja na mshindi wa pili wa Mkoa wa Morogoro, Sabra Islam akishikana mikono kusubiri nani atatangazwa kuwa Redd's Miss Kanda ya Mashariki , Juni 20, mwaka huu.
Wapenzi wa fani ya urembo wa Umiss wa kutoka sehemu mbalimbali ndani ya nje ya Mkoa wa Morogoro akishangilia kutajwa kwa Diana Laizer , Redd's Miss Morogoro kutwaa taji la Kanda ya Mashariki

Spika wa Bunge la Oman, (Majlis A'shura) Sheikh Khalid Bin Bilal Bin Nasir Al Maawali atembelea Serengeti

Spika  wa Bunge la Oman pamoja na wabunge 6 na wafanyakazi wengine wa Bunge la Oman, (Majlis A'shura) Sheikh Khalid Bin Bilal Bin Nasir Al Maawali leo ametembelea mbuga ya wanyama  ya Serengeti na kushuhudia sehemu ya 'Great Migration' katika mbuga hiyo. . Spika huyo ameishauri Tanzania kuitangaza zaidi utalii kwa kupitia vyombo vyote vya habari pamoja na mitandao ya kijamii ili kuvutia watalii wenye uwezo wa kifedha zaidi. Amehaidi ushirikiano wa kuitangaza Tanzania katika Inchi ya Oman na kuifanya iwe kivutio kwa wawekezaji wa kiarabu zaidi.
Spika wa Bunge la Oman, (Majlis A'shura) Sheikh Khalid Bin Bilal Bin Nasir Al Maawali akiwa katika hoteli ya kitalii ya Serengeti Four Seasons kabla ya kuelekea mbugani
Safari ya mbugani ikianza
Msafara wa  Spika wa Bunge la Oman, (Majlis A'shura) Sheikh Khalid Bin Bilal Bin Nasir Al Maawali
Pundamilia
Nyumbu kibao kila sehemu
Nyumbu
Safari ikiendelea
Nyumbu kila mahali
Msafar ukiendelea Serengeti

Mapumziko
 Spika wa Bunge la Oman, (Majlis A'shura) Sheikh Khalid Bin Bilal Bin Nasir Al Maawali akiongea machache
 Spika wa Bunge la Oman, (Majlis A'shura) Sheikh Khalid Bin Bilal Bin Nasir Al Maawali na msafara wake pamoja na wenyeji wake
Askari wa TANAPA akiwa lindoni
Mapumziko
Pundamilia
Msafara watua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Karume, Zanzibar