Thursday, February 16, 2012

HAFLA YA UZINDUZI WA NEMBO YA REDD’S MISS TANZANIA 2012 YAFANA SANA JIJINI DAR

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mawasilano wa TBL,Steven Kilindo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Redd's Miss Tanzania 2012 kwenye ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam usiku huu.
Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Redd's Miss Tanzania 2012 kwenye ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam usiku huu.
Mkurugenzi wa LINO Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania,Hasim Lundenga akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Redd's Miss Tanzania 2012 kwenye ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam usiku huu.
MC Taji Liundi akiwajibika.
Warembo walioshiriki Miss Tanzania mwaka 2011,wakiongozwa na Mrembo anaeshikilia taji hilo.Salha Israel (wa tatu kushoto) wakifungua pazia kuaziria uzinduzi wa nembo mpya ya Redd's Miss Tanzania 2012 wakati wa hafla iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.
Baada ya Uzinduzi sasa ni Burudani ya kijipongeza kwa warembo wa Miss Tanzania na Wakuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ndio wadhamini wakuu wa Redd's Miss Tanzania 2012.
Miss Tanzania anaeshilia ttaji hivi sasa,Salha Israel akiwa na kinywaji cha Redd's Original mbele ya Nembo mpya ya wadhamini hao.
Cheazzzzz.........
Nembo Mpya.
Kina Sie tuwajibikavyo.

Wednesday, February 15, 2012

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LAZINDUA KAMPENI YA KUPAMBANA NA UTAPIAMLO KWA WATOTO: MDAU WA HAKI ZA WATOTO HOYCE TEMU ASHAURI ELIMU YA LISHE ITOLEWE KWA WANANCHI.

 Baadhi ya Wanafunzi hao wakiwa na Mh. Hilda Ngowi.
 Mh. Mbunge wa Viti Maalum toka mkoa wa Iringa Lediana Ng'ong'o akizungumza na waandishi wa habari ambapo ametoa ushauri kwa  serikali kuwaajiri wataalam wa lishe kwa kila wilaya ili kufanikisha malengo ya Mkakati wa Kitaifa wa Lishe wa 2011/12 hadi 2015/16.

 Mwanaharakati wa Haki za Watoto na Afya zao Bi. Hoyce Temu akizungumza na wanahabari kuhusiana na kampeni ya kupambana na utapiamlo kwa watoto, ambapo amesema tatizo hilo ni kubwa sana hapa nchini na kuishauri serikali ielimisha jamii umuhimu wa kula chakula bora na pia kutoa ufafanuzi kuwa chakula bora ni kipi.
 Wanafunzi wakiwa makundi kuandika mapendekezo wanayodhani yakifanyiwa kazi na Serikali yatasaidia kuhamaisha mpango wa kupambana na Utapiamlo kwa watoto. 
 Dr. Ellen Otaru Okoedian akitoa mwongozo kwa wawakilishi wa mabaraza ya Wanafunzi kutoka wilaya za jiji la Dar es Salaam wakati Shirika la Save the Children lilipofanya uzinduzi wa taarifa ya Lishe leo jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wakiandika mapendekezo yao kwenye Bango kubwa maalum la EVERYONE.

 Mh. Lediana N'gong'o na Bi. Hoyce Temu wakiainisha baadhi ya mambo muhimu yanayotakiwa kutekelezwa ili kufanikisha kampeni ya kupambana na utapiamlo hapa nchini. 
 Meneja Kampeni wa EVERYONE wa Tanzania Jasminka Milovanov (kushoto) akibadilishana mawazo na Bi. Hoyce Temu. 
  Mjadala wa Mapendekezo ukiendelea
  Makundi ya Wanafunzi hao katika picha ya pamoja na  Waheshimiwa Wabunge na waandaaji wa uzinduzi huo.
Hoyce Temu katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge.



Shirika la Save the Children Tanzania limesema licha ya kuwepo maendeleo, watoto wanne kati ya kumi wenye umri wa miaka isiyozidi mitano nchini Tanzania wamedumaa.

Katika muhtasari wa wa hali ya Tanzania inaonyesha asilimia 17 wameathirika sana na kila siku watoto 130 wanakufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na utapiamlo.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa lengo la Milenia namba 4 linalotaka kupunguza theluthi mbili ya vifo vya watoto haliwezi kufikiwa bila kukabiliana na utapiamlo.

Akizungumza wakati wa hafla ya chakula baada ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mh. Lediana Ng’ong’o ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya lishe ameshauri serikali kuajiri wataalam wa lishe ikiwezekana katika kila wilaya nchini.

Naye Mdau wa Kuhamasisha Haki za Watoto na Afya zao Hoyce Temu aliyealikwa katika uzinduzi huo, amesema ni muhimu serikali ikatoa elimu ya lishe kwa wananchi, ili waweze kutambua umuhimu wa kula chakula bora na faida zake kimwili na kiakili.


Tuesday, February 14, 2012

airtel yashoo love kwa wateja wake leo siku ya valentine

Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel  wakiwa katika picha ya pamoja na wateja waliotembea Maduka ya Airtel na kuzawadiwa  ua ikiwa ni katika kuonyesha upendo kwa wateja katika siku hii maalumu ya valentine 
Meneja huduma kwa wateja Godfrey Kavishe (kulia) akikabidhi zawadi ya ua kwa mteja aliyetembelea duka la Airtel lililopo Mlima City Dar es Saalam  ikiwa ni katika kuonyesha upendo kwa wateja katika siku hii maalumu ya valentine  akishuhudia ( wapili kulia) ni Edina Mlay Afisa Msimamizi huduma kwa wateja Airtel akifatiwa na Mkurugenzi  wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba
 Mwakilishi wa  huduma kwa wateja akikabidhi zawadi ya ua kwa mteja aliyetembelea duka la Airtel lililopo Makao Makuu ya Airtel Morocco  ikiwa ni katika kuonyesha upendo kwa wateja katika siku hii maalumu ya valentine  akishuhudia ni Edna Mlay Afisa Msimamizi huduma kwa wateja Airtel Tanzania.
Pichani kushoto ni Mteja wa Airtel akifurahi baada ya kukabidhiwa ua  na maafisa wakuu wa huduma kwa wateja pale alipotembea duka la Airtel lililopo Mlima City Dar es Saalam, (kulia) ni Mkurugenzi  wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba

Mkurugenzi  wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (Kulia) akikabidhi zawadi ya ua kwa mteja aliyetembelea duka la Airtel lililopo Mlima City Dar es Saalam  ikiwa ni katika kuonyesha upendo kwa wateja katika siku hii maalumu ya valentine  akishuhudia ni Edina Mlay Afisa Msimamizi huduma kwa wateja Airtel Tanzania.