Thursday, December 13, 2018

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA TANZANIA NA DIGITAL PIPELINE UK (COMPUTERS 4 AFRICA) KUZINDUA MRADI WA ELIMU KWA NJIA YA MTANDAO SEHEMU YA KWANZA YA KOMPYUTA, PRINTERS, KOMPYUTA MPAKATO, PROJECTORS NA VIFAA MBALIMBALI VYA ICT VYENYE THAMANI ZA SHILINGI ZA KITANZANIA MILLIONI MIA SITA VIMEONDOKA UINGEREZA LEO KUJA TANZANIA.

Katika kuungana na juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mh. Rais Dkt John Pombe Magufuli, Shirika la Digital Pipeline UK, kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia wameanzisha mradi mkubwa utakaobadilisha na kuboresha utoaji wa elimu nchini kuanzia shule za msingi za serikali hadi kidato cha sita kwa njia ya mtandao salama (Secured School Network) utakaobeba mtaala (curriculum) na vitabu vya maarifa mbalimbali vinavyokwenda na wakati ili kuwafanya walimu na wanafunzi kujinoa ipasavyo na kuwa wabunifu wanaoweza kushindana katika ulimwengu wa maarifa kwa wakati. (Communication Tool).
Hayo yameelezwa jijini Kent nchini Uingereza leo, tarehe 12/12/18 na Ndugu Abraham Sangiwa, Mkurugenzi na Mwenyekiti wa DIGITAL PIPELINE UK ambayo inafadhiliwa na Bill and Melinda Gate Foundation, Metropolitan Police UK, National Health Services UK and Vauxhall Motors UK, Katika hafla iliyofanyika katika ofisi kuu Priory Park jijini Kent nchini Uingereza
Uzinduzi huo pia ulishuhudiwa na wadau mabalimbali akiwemo Deputy Lieutenant of Kent Trevor Sturgess, Bevil Williams C.E.O at Digital Pipeline, board members, wafanyakazi wa Digital Pipeline UK na wadau mbalimbali.
Ndugu Abraham Sangiwa aliendelea kusema napenda kuishukuru wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia kwa kuniteua kuwa Balozi wa Wizara katika Mradi huu wa Digital Campus in Tanzania, haikuwa kazi rahisi kufanikisha mradi huu kwa Tanzania kwani Digital Pipeline UK inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya ishirini na saba barani Afrika, nchi nane bara la Asia, baadhi ya nchi bara la  Ulaya, Amerika ya Kati na Kusini, na kila moja ilipenda mradi huu mkubwa wa kujenga Digital Campus Plant kubwa na ya pekee barani afrika unfanyike katika nchi zao, lakini kutokana na uzalendo na uelewa kwa timu nzima ya Wizara ya Elimu na viongozi wake na  kwa kuzingatia vigezo vilivyo wazi kwa serikali ya Tanzania vimesaidia kuleta mradi huu wenye manufaa makubwa nchini.
Tumeingia makubaliano na Wizara ya Elimu kufanya mradi huu kwa kusaini “memorandum of understanding, MoU” ambapo leo hii sehemu ya kwanza kuhudumia zaidi ya shule elfu moja unaanza kwa kupakia makontena haya ya vifaa husika na kuondoka hapa Uingereza kuelekea Tanzania, kwani serikali ya Tanzania kupitia TIE imekwishatoa eneo lilipo Mikocheni jijini Dar es salaam Tanzania ambapo kutajengwa Digital Campus kubwa itakayokuwa ikipokea vifaa vya mradi, pia mahali hapa patakuwa kituo kikubwa cha “recycling and assembling Plant” kwa ajili ya e learning na kufanya mageuzi kwa kutumia portal mbalimbali za “smart learning” mtandaoni
Digital Campus itatoa ajira, mafunzo na huduma  kwa watanzania wa kawaida, wafanyabiashara, serikali na mashirika mbalimbali yatakayotaka kuphase out thier ICT equipment safely with certification of data wiping under EU LAWS (World Standard) and US Military Standards.

Tunatarajia kuanza na shule elfu moja na kuleta computers, laptops, printers na projectors Zaidi ya eflu arobaini kwa awamu hii ya kwanza ,pia tunaamini kutoa vifaa hivi pekee bila kufanikisha upatikanaji wa mtandao (internet connection) hasa kwa maeneo ya vijijini itakuwa vigumu, hivo Digital Pipeline kwa kushirikiana na wizara ya Elimu,Sayansi, teknolojia na Wizara ya mawasiliano na Uchukuzi kupitia kampuni ya TTCL itaanda mkakati wa kufanikisha upatikanaji wa mtandao (internet connectivity) vijijini. Digital Pipeline kwa kushirikiana na “Avanti iknowledge program” wataunganisha mtandao kwa njia ya satellite, pia kusaidia upatikanaji wa umeme kwa njia ya “solar power” supply of panels and fittings ili kuweza kufanikisha malengo ya mradi huu muhimu katika kuboresha utoaji wa elimu 
Ndugu Abraham Sangiwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio UK (TZUK DIASPORA) aliendelea kusema kutakuwa na mafunzo kwa walimu namna ya kutumia smart e learning equipments (education “e” content partners) watakaotoa vitabu na majalida ya elimu yenye kwenda na wakati (innovative) online kutokakama na mtaala utakaowekwa. Mh. Rais Dkt John P Magufuli na Mh. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na timu yake katika Wizara wamejitahidi sana kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bure kwa kujenga madarasa na shule nyingi, sisi watanzania tunaoishi hapa UK na sehemu nyingine ulimwenguni tunahitaji kusaidia katika ubora wa elimu ili lengo la Tanzania ya Viwanda liweze kutimia kwa kutumia vipaji na ubunifu toka ndani ya nchi ambao unapotea kwa kiasi kikubwa hasa maeneo ya vijijini kutokana na kukosa walimu wenye kuweza kujiongezea maarifa kwa njia ya mtandao wa elimu duniani unaokwenda na wakati, pia wanafunzi kukosa vitabu vya sasa (up to date texts book) ambavyo ni rahisi kuvipata chini ya smart secured learning program
 Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi, Digital Pipeline UK (Computers 4 Africa) Ndugu Abraham Sangiwa (Kushoto), Bevil Williams C.EO.  Katikati ni Deputy Lieutenant of Kent Uingereza - Trevor Sturgess wakibadilishana mawazo katika ofisi kuu ya DP jijini Kent nchini Uingereza, wakati wa kushuhudia upakiaji wa vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya mradi wa “Digital Campus on Education in Tanzania” utakaofanywa kwa pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. 

Vifaa mbalimbali vya kielektroniki vikipakiwa kwenye container tayari kwa safari ya kuelekea Tanzania
Digital Pipeline - Computers Data are wiped to US military standards and recycled to protect the environment.

No comments: