Tuesday, December 18, 2018

WAZIRI MKUU AZUNGUMZIA UONGOZI WA SHEIKH MKUU ALIVYOZIMA MIGOGORO KATIKA MISIKITI, AGUSIA MCHANGO WAO

Na Said Mwishehe ,Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza Mufti wa Tanzania kwa namna ambavyo uongozi wake umemaliza migogoro ambayo ilikuwa inaibuka kwenye misikiti mbalimbali nchini na kwamba kwa sasa Waislamu ni wamoja.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa ametumia nafasi hiyo kuzungumzia hali ya amani nchini ambayo msingi wake unatokana na viongozi wa dini zote ambao wamekuwa wakihimiza umoja na mshikamano.

Majaliwa amesema hayo jana mbele ya Rais Dk.John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za BAKWATA kufikisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Desemba 17 mwaka 1968 ambapo amesema dini zote zimekuwa mstari wa mbele katika kushiriki katika maendeleo nchini.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Mufti wa Tanzania ambavyo chini ya uongozi wake ambavyo amesaidia kuwafanya Waislamu nchini kuwa wamoja na kushiriki kwenye maendeleo ya nchi yao.

"Leo hii tunashudia chini ya Mufti wa Tanzania,hatusikii migogoro ambayo tulikuwa tunaisikia siku za nyuma.Kumetulia na mambo yanakwenda vizuri.Hongera Mufti Sheikh Aboubakary Zubeiry kwa uongozi wako mahiri.Tangu uwe kwenye nafasi hiyo sasa ni mwaka wa tatu,umetuunganisha ," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Wakati huo huo amezungumzi mchango wa viongozi wa dini zote pamoja na waumini wa dini hizo kwa namna ambavyo wamekuwa wakishiriki katika kuleta maendeleo ya nchi yao na kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Magufuli katika kuleta maendeleo.

Amesema" Mchango wa viongozi wa dini zote wamekuwa mstari wa mbele katika kushiriki kwenye maendeleo ya nchi yetu, kupitia taasisi zao mbalimbali wamekuwa wakisaidia sekta ya afya, maji na utoaji wa huduma nyingine za kijamii.Kabla ya Waziri Mkuu kuzungumza Mufti wa Tanzania Sheikj Zubeiry alieleza namna ambavyo sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali BAKWATA ambao wamefika hapo.

Pia amesema Mufti Zubeiry amesema BAKWATA limefurahishwa na uamuzi wa Rais Dk.John Magufuli kukubali wito wao wa kuhudhuria sherehe za baraza hilo kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Amesisitiza kwamba viongozi wote wa BAKWATA nchini zima wako kwenye sherehe hizo za kutimiza miaka 50, pamoja na viongozi wengine wa taasisi ya dini,mabaraza ya dini pamoja na maimamu mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo.

"Viongozi wote wako hapa kuqnzia ngazi ya wilaya hadi Taifa.kwa idadi ya waliokuwepo leo tungeweza kusema ni kama mkutano mkuu kutokana na idadi ya walioshiriki na nafasi zao," amesema Mufti Zubeiry wakati anazungumzia sherehe hizo na aina ya viongozi waliohudhuria

No comments: