Saturday, December 8, 2018

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MRADI WA VIOSKI TEMBEZI JIJINI DODOMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajasiriamali (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa vioski (Trolley Push Cart) wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, Disemba 8, 2018, Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo wa vioski wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC). (Kushoto) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi huo.
Mkurugenzi wa Masoko, Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bi. Awaichi Mawalla akifafanua jambo kwa kuhusu mradi huo uliobuniwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TCC na wajasiriamali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi wa vioski uliobuniwa na kampuni ya Sigara Tanzania.
Mkurugenzi wa Masoko, Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bi. Awaichi Mawalla akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama kuhusu matumizi ya Vioski mara baada ya uzinduzi wa hafla hiyo. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi mkataba kwa mjasiriamali Bi. Pendo Godfrey wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi wa vioski iliyofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa pamoja na Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) wakimsikiliza Fundi Mkuu wa Vifaa Saidizi kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Mwita Marwa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Viungo Dodoma, Bw. Hassan Hussein. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali walioweza kunufaika na mradi huo, mara baada ya uzinduzi wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma, Disemba 8, 2018.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua mradi wa vioski tembezi wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC).

Akizungumza leo Disemba 8, 2018 Waziri Mhagama amesema kuwa mradi huo utasaidia wajasiriamali wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo kuweza kujiajiri na kupata kipato kitakacho wanufaisha kiuchumi.“Hii ni faraja kubwa kwetu kama Serikali kuona mnaunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto za ajira nchini kwa kuwawezesha wajasiriamali kuchangamkia fursa za kujiendeleza kibiashara”, alisema Mhagama.

Aliongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau na kuwataka wawekezaji wengine waweze kubuni miradi kama hiyo yenye manufaa kwa wananchi.Aidha, Mhe. Mhagama aliipongeza kampuni ya Sigara Tanzania kwa ubunifu na kuwasihi waendelee kufanya vizuri katika nyanja nyingine kwa manufaa ya watanzania kwa ujumla.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa ni jambo la faraja mradi huo umezinduliwa Jijini Dodoma ikiwa ni fursa kubwa kwa wajasiriamali kuweza kunufaika kiuchumi.

Naye, Mkurugenzi wa Masoko, Bi. Awaichi Mawalla amesema kuwa Vioski 400 vitagawiwa nchi nzima kwa wajasiriamali wadogo ambao wamekuwa wakifanya kazi na kampuni ya TCC na wataweza kuuza bidhaa mbalimbali.


No comments: