Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama akiongoza kikao cha pamoja na Watumishi wa Ofisi
hiyo walipokutana akujadili masuala yao ikiwa ni sehemu ya kufahamiana
na kuendelea kufanya kazi kwa umoja, mkutano huo ulifanyika Desemba 10,
2018 katika Ukumbi Mikutano wa LAPF Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi yaWaziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene
Isaka, akifafanua masuala ya malipo ya Pensheni kwa watumishi wa Ofisi
ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo.
Mkaguzi wa Ndani Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Omari Mpayage akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu) Bw. Peter Kalonga akifafanua masuala ya utawala kwa watumishi
wa Ofisi hiyo wakati wa kikao hicho.
Msaidizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Richard Kalinga akiuliza swali wakati wa mkutano huo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameitaka Menejimenti ya Ofisi yake
kushughulikia kero za watumishi kwa haki na usawa ili kumaliza kero
zilizopo.
Ameyasema hayo wakati wa Mkutano
na Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu walipokutana kujadili masula
yanayowakabili wawapo kazini uliofanyika Desemba 10, 2018 katika Ukumbi
wa LAPF Dodoma.
Waziri aliwataka Watendaji wa
ofisi yake kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili watumishi kuhusu
madai mbalimbali ikiwemo; kupanda madaraja, uhamisho, usalama mahali pa
kazi na masuala ya kuzingatia afya wawapo kazini ili kuhakikisha
wanatekeeleza majukumu yao katika mazingira rafiki.
“Kama kuna motisha kubwa kwa
mtumishi ni kumsaidia kutatua kero yake inayohusiana na utumishi wake
kwa uzito unaolingana na tatizo au uhitaji wake ili kusaidia kuongeza
morali yake katika kufanya kazi.”Alisema Mhagama.
Sambamba na hilo waziri aliwaasa
watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kutumia mabaraza ya Wafanyakazi katika
kujadili na kutatua kero wanazokabiliana nazo wawapo kazini.
“Ni vyema watumishi kuendelea
kuyatumia mabaraza ya wafanyakazi yaliyopo kisheria katika ofisi ili
kabla masuala hayajafika ngazi za juu yawe yamekwishwa sikilishwa na
kutafutiwa ufumbuzi pale inapowezekana”.Alisistiza Waziri
Aliongezea kuwa, ni wajibu wa
Makatibu wakuu kuendelea kusimamia na kuhakikisha haki na usawa
vinazingatiwa katika Ofisi ili kuwa na weredi na ufanisi katika
kutekeleza majukumu ya kila siku.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi aliahidi
kuchugua maagizo ya waziri na kuahidi kuyatekeleza kama ilivyoelekezwa
katika mkutano huo.
“Tutaendelea kusimamia shughuli za
Ofisi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuhakikisha
haki na usawa vinazingatiwa mahali pa kazi ili kuweza kufikia malengo
na kuendelea kuiletea nchi maendeleo”.Alisema Tarishi
No comments:
Post a Comment