Wednesday, December 12, 2018

NAIBU WAZIRI AWESO ATOA MAAGIZO KWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAJI PROFFESA MKUMBO


NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso wa kwanza kulia akikagua mabomba yatakayotoa maji eneo la Kilapula ambayo yatapeleka maji wilayani Muheza kutoka Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maji kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua moja ya miundombinu ya maji wilayani Pangani
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipanda juu kuangalia tanki ya kuhifadhiwa maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambapo mradi huo unatoa maji katika eneo la Pongwe Jijini Tanga na kuyapeleka wilayani humo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi huo
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald wakati wa ziara hiyo.

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiangalia moja ya miradi ya inayotekelezwa wilayani Pangani Mkoani Tanga wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kata ya Madanga wilayani Pangani wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akisalimia na mmoja wa wananchi wa wilayani Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maji
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mradi huo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia na wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald




NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Kitila Mkumbo kumtafutia kazi nyingine Mhandisi wa maji Wilaya ya Pangani Novath Wilson kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo miradi ya maji wilayani humo na kupelekea wananchi kushindwa kupata huduma hiyo muhimu kwa wakati.

Ametoa agizo hilo wakati akiwa wilayani Pangani ikiwa ni ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga alipotembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa wilayani humo na kutokuridhishwa nayo kutokana na utekelezaji wake kuwa chini ya kiwango hatua iliyomlazimu kuzivunja baadhi ya kamati za usimamizi wa maji ambapo ziara hiyo alianzia wilayani Muheza

Licha ya mhandisi huyo kutoa sababu mbalimbali ya baadhi ya miradi kukwama kutoa maji lakini Naibu Waziri huyo alionyeshwa kutokuridhishwa na majibu hayo kutokana na baadhi ya maelekezo aliyokuwa akimpa ili kuweza kukabiliana na changamoto juu ya miradi hiyo.

“Nimekuita marangapi Wizarani ..tena nikakukutanisha na viongozi wengi labda watakusaidia na kila mara nakupigia simu lakini bado unaonekana si mtendaji wa kazi sasa nitamwambia Katibu Mkuu wetu akutafutie kazi sehemu nyingine lakini sio hapa Pangani”Alisema Aweso.

Aidha alisema ni jambo la ajabu ikiwa Serikali inapambana kutenga fedha kwa ajili ya kuwakomboa wananchi na tatizo la maji huku baadhi ya watendaji wa Serikali wakishindwa kusimamia vema miradi hiyo na kupelekea wananchi kuichukia Serikali yao.

Awali akijibu hoja za Naibu Waziri juu ya sababu za mradi huo wa Maji uliotekelezwa kwa zaidi ya shilingi Milioni 260 Mhandi huyo wa Wilya alisema mradi huo ulimalizika machi 2013 na unamiaka mitano tangu kukamilika kwake.

Mhandisi huyo alisema mradi huo unaendeshwa na jumuiya ya watumia maji ambayo iliundwa kwa mujibu wa kishera na ndio inayoendelea kusimamia mradi huo ambao kunatakriban mita 1500 kuelekea Kijiji cha madanga ambapo mabomba yake yalionekana kuchakaa.

“Mh:Naibu Waziri mradi huu unanjia mbili kuelekea Jaira na Madanga lakini kunauchakavu wa miundombinu ambapo jumuiya iliyopo haikukusanya fedha ili kuweza kufanya ukarabati na ndio sababu ya eneo hilo kukosa maji muda wote”Alisema Mhandisi Wilson.

Naibu Waziri huyo alishangazwa na hitaji la mabomba hayo kwa urefu wa mita hizo 1500 ambayo ni kiasi cha shilingi milioni 3 kwa ajili ya bomba za nchi mbili huku jumuiya hiyo ikiwa haina hata shilingi kumi jambo lililomtia wasiwasi Waziri huyo wa mradi huo kufa.

“Mradi wa shilingi milioni 260 na leo hakuna hata shilingi kumi na leo hakuna maji maana yake wananchi hawana maji na kila kitu mnatoa majibu ya hakuna mradi huu unaweza ukafa na wananchi wakakosa maji swala hili sitolivumilia”Alisema.Wakati huohuo amemuiagiza Katibu Mkuu huyo kuhakikisha Mkandarasi wa Kampuni ya Koberg Constraction Ltd anaetekeleza mradi mkubwa wa maji toka Pongwe Jijini hadi Wilayani Muheza analipwa fedha kwa wakati ili kumuongezea ufanisi wa kazi zake.

Akizungumzia mradi huo Mhandisi toka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira(Tanga Uwasa) Salum Hamisi alisema mkandarasi anasimamia mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 2.6 yupo katika asilimia 50 huku akikabilia na changamoto ya fedha ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Mhadisi Hamisi ambae ni msimamizi wa mradi huo alisema mradi huo unatarajiwa kumalizika mwezi Mei mwakani ikiwa Wizara itamlipa mkandarasi fedha zake kwa wakati mradi utakaosukuma maji katika matank matano na kutarajia kupunguza kwa kiasi kikubwa adha ya maji Wilayani Muheza. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald alisema ziara ya Naibu Waziri inamanufaa kwa wananchi hasa baada ya kutembelea baadhi ya miradi na kubaini baadhi ya chanagamoto huku baadhi ya kamati zikionekana kutofanya vizuri na kuchukuliwa hatua. 

No comments: