Monday, December 3, 2018

WAZIRI KAKUNDA AZUNGUMZIA UWEKEZAJI WA CHINA, MKURUGENZI MTENDAJI TIC APONGEZA TAMKO LA RAIS

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amesema China ndio nchi pekee ambayo imeweka fedha nyingi zaidi kwa ajili ya uwekezaji ambapo fedha waliyoweka kwenye kuwekeza ni Dola za Marekani bilioni 5.8 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh.trilioni 12 huku akisisitiza umuhimu wa kujengwa kwa viwanda nchini ambako kutsaidia kuzalisha bidhaa nyingi ambazo zitauzwa nje ya nchi yetu.

Kakunda amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati mkutano uliowakutanisha wawekezaji kutoka nchini China, maofisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta zinazojihusisha na uwekezaji nchini ambapo wametumia nafasi hiyo kujadili fursa za uwekezaji ambazo zipo nchini.

Akifafanua zaidi wakati anazungumzia ujio wa wawekezaji kutoka nchini China ambao wapo nchini kuangalia fursa za uwekezaji, amesema kuwa kwa sasa China ndio nchi ambayo imeweke fedha zake nyingi kwa ajili ya masuala ya uwekezaji ambao wamewekeza nchini.

"Nchi ya China au wawekezaji kutoka China ndio ambao wameka fedha nyingi sana katika maeneo ya uwekezaji.Wamewekeza kwenye viwanda vya aina mbalimbali, vimo viwanda vya saruji, viwanda vya kubangua kurosho na pia wapo pia kwenye uwekezaji katika eneo la ujenzi ambako nako huko wameweka fedha nyingi,"amesema Kakunda.

Amesisitiza pamoja na uwekezaji huo wa China ,Kakunda amefafanua mikakati ya Serikali ni kuhakikisha wawekezaji hao wa China wanajenga viwanda vingi nchini Tanzania na hiyo itasaidia katika kuongeza uzalishaji wa bidhaa ambazo zitauzwa nje ya nchi na kujipatia fedha nyingi.

Ameongeza kupitia ujenzi wa viwanda nchini Tanzania, kutakuwa na faida nyingi zikiwemo za nchi nyingine nazo kununua bidhaa zinazozalishwa nchini."Bado tunahitaji wawekeze zaidi kwenye uzalishaji bidhaa.Tukifanya hivyo tutakuwa tumepunguza urari wa kibiashara."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TIC Geoffrey Mwambe ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mazingira ya uwekezaji nchini ambayo ni tulivu na salama kwa wawekezaji kuwekeza.Pia amesema anapongeza na kuunga mkono tamko ambalo limetolewa na Rais Dk.John Magufuli jana akiwa mkoani Arusha kuhusu suala la kodi kuwa rafiki kwa wananchi wakiwamo wafanyabishara.

Mwambe amesema kuwa "Tunaunga mkono juhudi za Rais wetu ambaye jana tu ametoa tamko zito kuhusu suala la kodi, Rais amesisitiza mazingira ya uwekezaji nchini yawe salama na yenye kuvutia.Tamko kuhusu kodi naamini wawekezaji wengi na wafanyabiashara watakuwa wamelisikia na inaonesha namna ambavyo Rais hataki kuona kodi ambayo si rafiki.Tusilazimishe kukusanya kodi kwa siku moja na matokeo 
yake biashara zinafungwa."

Amesema kiongozi wa nchi amesisitiza kwenye ukusanyaji wa kodi kufanyika katika mfumo ambao utafanikisha zaidi ukusanyaji kodi ambao ni rafiki ili kuhakikisha kila mfanyabiashara au mwekezaji anamudu kodi ambayo anakadiriwa.

Wakati huo huo Godfrey Sembeye kutoka TPSF amesema sekta binafsi nchini 
imempongeza Rais Dk.Magufuli kwa kukemea tabia ya ukusanyaji kodi ambao si rafiki katika mazingira ya biashara na uwekezaji na kwamba kitendo cha Rais kuikemea TRA wananchi watakuwa na imani naye kwani wataamini anafahamu manyanyaso ambayo wanayapata kutokana na TRA.

"Tanashukuru Rais kwa tamko lake la jana kwani tumekuwa tukilalamikia 
manyanyasayo ambayo wafanyabiashara wamekuwa wakiyapata na hatimaye amesikia kilio chetu,"amesema Sembeye.

Kuhusu China amesema ni kama chai ambayo haipukiki na kwa kutambua umuhimu wao TPSF wameanzisha dawati maalumu kwa ajili ya kushughulikia raia Wachina waliko nchini kwenye masuala la biashara na uwekezaji kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi(TPSF) Godfrey Sembeye akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji baina ya wawekezaji waChina na Tanzania ambalo limefanyika leo jiiini Dar es Salaam.
 Baadhi ya  wawekezaji kutoka nchini China ambao wapo nchini wakiangalia fursa za uwekezaji wakimsikiliza Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseoh Kakunda wakati wa kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania.wakimsiki
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania(TIC)Geoffrey Mwambe (kulia) akiteta jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Wang Ke wakati wa kongamano la uwekezaji ambalo limejumuisha wawekezaji wa nchi hizo mbili
 Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Uhusiano kati ya nchi zinazoendelea kutokana China Lyu Xinhua akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji kati ya wawekezaji wa China na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda (kushoto)akiandika kabla ya kuzungumza kwenye kongamano la uwekezaji ambalo liliwahusisha wawekezaji kutokana nchini China ambao wamefika nchini kuangalia fursa za uwekezaji

No comments: