Wednesday, December 5, 2018

Tony Elumelu kufungua dirisha Programu ya Wajasiriamali Afrika, Januari 1, 2019

Na Bakari Kimwanga -DAR ES SALAAM 

TAASISI ya Tony Elumelu (TEF), imetangaza kufungua mzunguko wa tano wa programu ya Wajasiriamali Afrika kuanzia Januari 1, 2019 

Maombi hayo yatatumwa na kushughulikiwa kwenye kwenye jukwaa kubwa la mitandao kwa wajasiriamali wa Afrika, TEFConnect - www.tefconnect.com

Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Tony Elumelu yenye makao makuu yake Lagos, nchini Nigeria ilieleza kwamba kuanzia Januari 1, 2019, saa 12 asubuhi, Tony Elumelu itaanza kupokea maombi ya mzunguko wa tano wa Programu ya Wajasiriamali. Ambapo waombaji 1,000 waliochaguliwa wataunganishwa msimamizi wa sasa wapatao 4,470 katika program hiyo. 

Tangu mwaka 2015, Mpango wa Biashara wa TEF – imekuwa ni kichocheo kiliasisiwa kwa misingi ya Afrika ambapo aina hiyo, imewawezesha wajasiriamali 4,470 wa Afrika, ambao kila mmoja amenufaika kwa kupatiwa Dola 5,000 kila mmoja. 

Hatua hiyo huenda sambamba na mjasiriamali kuhudhuria mafunzo ya biashara yanayoendeshwa kwa wiki 12, ambao hupata ushauri na uzoefu na kujifunza zaidi mazingira ta Biashara ya Afrika. 

Wanufaika wa Programu wamefanikiwa kuhojiwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Forbes (Afrika) 30 chini ya orodha 30. Ambapo wamevutia wawekezaji, na pia wamepewa tuzo za Impact Google na Tuzo ya "Venture" kwa wajasiriamali. 

Programu ya ujasiriamali imewezesha kubadilishana uzoefu kati ya wajasiriamali wa Afrika na viongozi wa sekta ya umma na wa kimataifa, wawekezaji na washirika wa maendeleo ya namna bora ya kuongeza biashara zao. 

Sambamba na hilo pia wameweza kuongeza fursa na kuonyesha ubunifu wao na kutambua njia za kuimarisha mazingira ya biashara katika Bara la Afrika. Mnamo Juni 2017, Foundation iliandaa Jukwaa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na wajasiriamali wadogo wa Kiafrika walihudhuria. 

Na pia mnamo Oktoba mwaka huu (2018), TEF ilifurahi kuwa na Rais wa Jamhuri ya Ghana Nana Akufo-Addo wa Ghana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambao kwa pamoja waliweza kuzungumza na mkusanyiko wa wajasiriamali wadogo wa Afrika katika jukwaa hilo lililofanyika Lagos, Nigeria. 

Uwekezaji wa Foundation, umekuwa na mafanikio kutokana na kujitolea kuendeleza ujasiriamali na inaangaziwa kwamba ni ufunguo kwa Bara la Afrika kuweesha mabadiliko Afrika. 

Lengo la Tony Elumelu Foundation ambayo ilizindua Programu ya Uwekezaji, mpango wake kuwekeza Dola milioni 100 kwa kipindi cha miaka 10, ambapo wajasiriamali 10,000 wa Afrika watanufaika kutokana na kuwasilisha mawazo ambayo yana uwezo wa kubadilisha bara la Afrika. 

Hatua hiyo inakwenda sambamba na lengi kuu la kuwekeza katika biashara ambazo zinaweza kuzalisha angalau ajira 1,000,000 na kuchangia angalau dola bilioni 10 katika mapato ya kila mwaka ya Afrika. 

Programu ya Wajasiriamali ya TEF ni wazi kwa wananchi na wakazi wananchi wote wa nchi zote za Bara la Afrika, ambapo huendesha biashara zilizo chini ya miaka mitatu. Pia mpango huu unasistiza kwamba hata mawazo ya biashara ambayo bado hayajaanza yanapokewa na kufanyiwa kazi. 

Maombi ya mwaka 2019 yatashughulikiwa kwenye jukwaa kubwa la mitandao ya digital kwa Afrika TEFConnect on www.tefconnect.com.
Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu (kushoto), akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, wakiwa na kijana mshiriki wa kongamano kutoka nchini Ghana baada ya kijana huyu kutaka ufafanuzi kwa Rais wake wa namna vijana wanavyopewa kipaumbele katika ujenzi wa uchumi wa nchi hiyo. Mkutano huo ulifanyika Lagos, Nigeria Oktoba mwaka huu.
Sehemu ya vijana walioshiriki jukwaa kubwa la wajasiriamali Afrika, lilofanyika Oktoba mwaka huu, Lagos, Nigeria

No comments: