Monday, December 3, 2018

ONGEZEKO WAHITIMU CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DUCE NI MAFANIKIO- PROF KILLIAN

Na Zanab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mahafali ya kumi na moja (11) ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yamefanyika jana kwa jumla ya wahitimu 1769 wametunukiwa katika ngazi mbalimbali.

Kwenye mahafali hayo wahitimu 1736 wametunukiwa digrii za awali katkka fani mbalimbali, 26 wakitunukiwa stashada ya uzamili katika elimu na 7 wakitunukiwa shahada ya umahiri.

Akitoa hotuba kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es salaam Dkt Jakaya Mrisho Kikwete , Rasi wa Chuo Kikuu Kishirikishi Professa Bernadeta Killian amesema kuwa kati ya wahitimu wote wa mwaka huu wanaume ni 1255 na wanawake ni 514.

Amesema idadi ya wahitimu kwa upande wa digrii za awali ni kubwa ikilinganishwa na wahitimu wa miaka yote iliyopita, kwani wahitimu wa digrii za awali kwa mwaka 2017 ilikua ni 1443 ambalo ni ongezeko la wahitimu 239 na kufikia 1736 na wahitimu wa masomo ya sayansi kuongezeka mara mbili kutoka 231 kwa mwaka 2017 kufikia 472 kwa mwaka 2018.

"Ongezeko hilo ni kielelezo cha mafanikio katika jitihada za serikali za kupambana na upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi katika shule za umma na binafsi na kufikia mahafali haya chuo kinakuwa kimetimiza wahitimu 11,436 waliobobea kwenye fani mbalimbali tangu kuanzishwa kwake.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa DUCE, Profesa William Anangisye aliwaomba wahitimu wote watambue kuwa maisha ya mtaani sio mepesi yanahitaji kujituma na kufanya kazi kwa bidii hivyo mtalazimika kufanya kazi wakati mwingine katika mazingira magumu lakini kwa maarifa na ubunifu, kuhakikisha mnajikomboa na umaskini na kuisadia Tanzania kufikia maendeleo endelevu.

Katika mahafali hayo Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete alitoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri na kuwakabidhi vyetu vyao kabisa.
Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dkt Jakaya Kikwete akitoa cheti kwa Mwanafunzi Bora wa kike kutoka kitivo cha Elimu Irene Loshiro wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).Mahafali ya kumi na moja (11) ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yamefanyika jana ambapo jumla ya wahitimu 1769 wametunukiwa katika ngazi mbalimbali.
Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Dkt Jakaya Kikwete akitoa cheti kwa Mwanafunzi Bora wa kiume kutoka kitivo cha Sayansi Mohamed Hassan wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) .
Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Dkt Jakaya Kikwete akiwa na  Mwanafunzi Bora wa kike kutoka kitivo cha ElimuIrene Loshiro  na Mwanafunzi bora wa Kiume Kitivo cha Sayansi Mohamed Hassan wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jana.
Wahitimu wakiwa wanatunukiwa kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).
Maandamano ya Kitaaluma yakiingia uwanjani wakati wa Mahafali ya 11 ya Chuo Ikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).

No comments: