Sunday, December 9, 2018

NAIBU WAZIRI MHE. KANYASU AENDESHA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto) akizungumza mara baada ya ibada iliyofanyika katika ya Kanisa la Wasabato la Geita kati wakati ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita

Baadhi ya waumini ibada wa Kanisa la Wasabato la Geita kati wakifuatilia ibada kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

Mchungaji na Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke akitoa mahubiri kwa waumini waliojumuika katika ibada ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Kanisa la Wasabato la Geita wakisikiliza mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

Baadhi ya wanakwaya wakiimba wakati wa mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa skafu na vijana wanafunzi wa Skauti kanisa la Wasabato la Geita Kati kabla ya Naibu Waziri huyo kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita mara baada ya kusomewa taarifa ya hali ya uhifadhi wa misitu na wanyamapori kabala ya kushirikia harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)



LUSUNGU HELELA-GEITA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesali katika Kanisa la Wasabato la Geita Kati mkoani Geita ambako ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya.

Lengo la kuendesha harambee hiyo ni kwa ajili ya kuchangisha pesa zitakazotumika katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kanisa la Wasabato kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo kitakachosaidia kuihudumia jamii.

Katika harambee hiyo Naibu Waziri Mhe. Kanyasu aliambatana na wadau wake ambapo kwa pamoja waliweza kukabidhi Sh15 milioni zikiwa ni fedha taslimu kama mchango wao.Katika harambee hiyo, ahadi mbali mbali zimeweza kutolewa ikiwemo matofali, saruji pamoja na malori ya mchanga na mawe.

Sambamba na hilo, Mhe. Kanyasu ameupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa kuwa na mpango huo wa kuisaidia serikali katika kutoa huduma kwa jamii ambayo kimsingi ni kazi ya Serikali,”Suala la kujenga vituo vya afya ni jukumu la serikali lakini ninyi mmeamua kuisaidia serikali nawapongezeni sana na msisite kunishirikisha kwa lolote.

Aidha, Mhe. Kanyasu amewataka waumini wa Kanisa hilo kuendelea kujitolea kukamilisha hatua za ujenzi wa kituo hicho cha AfyaKwa upande wake Mchungaji na Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke amesema kituo hicho cha Afya mara baada ya kukamilikwa kwake kitatumika kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na sio kwa ajili ya kupata kitu

Ameongeza kuwa kituo hicho kitawasaidia kitasaidia kuijenga jamii kiroho na kimwili na ili kukamilika kwake jumla ya sh 150 milioni zinahitajika.

No comments: