Monday, December 10, 2018

MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI













MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco akizungumza na wajumbe cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Handeni wakati wa ziara yake ya kujitambulisha ambapo alisisitiza umoja na mshikamano itakayofanyika mkoa mzima wa Tanga.
Mjumbe wa Halmashauri ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mwalimu Mwantumu Zodo akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia niMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco kushoto ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo 
MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Godwin Gondwe akizungumza wakati wa ziara hiyo.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco wa pili kutoka kulia akiwa na Mjumbe wa Halmashauri ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mwalimu Mwantumu Zodo wakisikiliza hoja mbalimbali za wanachama.
Sehemu ya wanachama wa CCM wilayani Handeni wakimsikiliza MNEC 
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco katiati akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mwalimu Mwantumu Zodo kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Handeni Salehe Kikweo 







MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco amewataka wanachama wa chama hicho wajiepushe na migogoro, makundi na majungu yasiyokuwa na tija kwa ustawi wa chama chao kwani yanaweza kusababisha mpasuko miongoni mwao.

Salim alitoa wito huo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kuzungumza na wajumbe katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Handeni ambapo alisema kwa sasa wanachama hao wanatakiwa kubadilika na kutokuipa nafasi kwani inaweza kurudisha nyuma maendeleo.

Alisema suala hilo limekuwa likimuumiza sana huku akiwataka wanachama kuhakikisha wanaachana nayo ili waweze kuunganisha nguvu za pamoja katika kukijenga chama chao ili kiendelee kuwa imara na kuendelea kuwatumikia watanzania.

“Ndugu zangu labda niwaambie kwamba mimi naumizwa sana na migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza kwani haina tija kwa ustawi wa chama chetu na inaweza kutugawa sisi hivyo niwatake msiipe nafasi kwenye maeneo yenu tuungane kwa pamoja tushirikiana kwa lengo la kuhakikisha haipewi nafasi “Alisema Mnec huyo.

Aidha pia aliwataka wajumbe hao kuwatumikia wananchi bila kubaguana rangi, jinsia ikiwemo kushuka chini kufanya kazi na wenzao waliowapa dhamana hiyo muhimu ili kuweza kusogeza mbele gurudumu la maendeleo kwao na jamii zinazowazunguka.

“Katika uchapaji kazi wetu tuige mfano wa Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli ambaye amekuwa akifanya mambo makubwa na yenye maendeleo kwa watanzania na hivyo kupelekea kuinua uchumi wa nchi ...lakini niwaambie kwamba uwepo wa CCM kushika dola hata wafanyabiashara na watu wengine wanaofanya shghuli zao kwa amani na utulivu,

“Niwaambie kwamba katika awamu zote tano ni nzuri lakini hii tulionayo ilipelekea mimi kuvutiwa na kugombea nafasi hiyo ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa nilikuwa kwenye chama muda mrefu kutoka mfumo wa vyama vingi ulipoanza lakini baada ya kuona Mwenyekiti wao wa Taifa analipigania sana Taifa na kutoa maamuzi yenye tija kwa ustawi wa maendeleo ya nchi yetu ndipo nilipoona tunapaswa kumuun ga mkono “Alisema.

Pia aliwaaambia wajumbe hao kwamba wanapotafuta nafasi kwa njia ya demokrasia na inapotokea bahati mbaya mwenzako kura zake hazikutosha naombeni muweka moyo wenu safi kwa kushirikina na wenzanu waliopata ridhaa.

Katika hatua nyengine Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Ratco alimuagiza katibu wa CCM wilaya ya Handeni kuhakikisha miradi ya chama hicho wanaiorodhesha ili aweza kutambua ipo mingani na nini kinapatikana ili waweze kusaidiana katika kusimamia mradi iweza kutatua kero zao zinazowakabili.

Naye kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Handeni Salehe Kikweo alisema kwamba chama wilayani humo kinawanachama 60015 ambapo kati ya wao wanaume ni 29990 na wanawake ni 30025 huku akieleza wanaendele kuhakikisha ilani CCM inatekelezwa na wilaya hiyo kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020

Alisema mkakati wa CCM wilaya ni kuhakikisha wanazidi kufanya vizuri kutokana na kwamba wilaya hiyo ni ngome ya CCM ikiwemo kuaanda semina kwa viongozo huku mambo ya kiuchumi yakiibuliwa ili kukiimariusha chama kuelekea kwenye uchaguzi.

No comments: