Wednesday, December 12, 2018

MMILIKI MABASI YA PRINCES MURO ALIPA FAINI YA MILIONI 115/-AKWEPA KWENDA JELA MIAKA NANE

*Ni baada ya kukiri makosa ya kutakatisha fedha, kuongoza genge la kuiba mafuta bomba la bandari


Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya Princes Muro Majid Kimaro kulipa faini ya Sh. milioni 115 au atatumimia kifungo cha miaka nane jela baada ya kukiri mashtaka yanayomkabili ya kutakatisha fedha na kuongoza genge la uhalifu ili kuiba mafuta katika bomba linalomilikiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Pia Mahakama imeamuru gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 856 ADH ambalo lilitumika kuiba mafuta hayo ambayo ni zaidi ya lita 26,875.25 ya dizeli na petroli litaifishwe na kuwa mali ya Serikali.

Hukuumu hiyo imesomwa leo Desemba 12, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kuhukumiwa na jopo la mawakili likiongozwa na Wakili wa Serikali Wankyo Simon akisaidiana na Jackline Nyantori, Patrick Mwita

Alitoa Hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema, Mahakama imemtia hatiani mshitakiwa kwa makosa mawili baada ya kukiri kutenda makosa hayo mwenyewe.

Akisoma adhabu, amesema, katika shitakalLa kuongoza genge la uhalifu, Muro anahukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano na iwapo akishindwa atatumimia kifungo cha miaka mitatu gerezani. Wakati katika shtaka la utakatishaji fedha, mshtakiwa ameamriwa kulipa faini ya Sh.milioni 110 au kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani.

Mapema kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili Wankyo ameiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwa sababu makosa hayo ya wizi husababisha kuathirika kwa uchumi na nchi kukosa mapato.

Pia ameiomba gari hilo litaifishwe na kuwa mali ya serikali kwa sababu ndilo lililotumika kubeba mafuta baada ya kulitoboa bomba na kuiba mafuta hayo.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 81/2018 inadaiwa kati ya Julai Mosi, 2016 na Januari 8, mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam na maeneo mengine Muro akiwa pamoja na wenzake ambao hawako mahakamani, kwa kujua aliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kutoboa bomba la mafuta la TPA na kuiba mafuta ili kupata faida.

Mshtakiwa Muro pia anadaiwa adaiwa kujipatia lita 15,950.3 za mafuta ya diseli na lita 10,925.22 za mafuta ya petroli na kusambaza mafuta hayo kwenye vituo vyake vya mafuta na kuyauza kwa watu mbalimbali huku akijua kwamba wakati akipata mafuta hayo, yametokana na makosa ya uhalifu.
Pichani mshtakiwa Majid Kimaro ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya Princes Muro akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kufanikiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 115 na kukwepa kutumikia kifungo cha miaka nane gerezani.

No comments: