Sunday, December 23, 2018

Mkazi wa Kivule Dar aondoka na 10m/-za Jigiftishe

 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni kumi katika Promosheni ya Tigo igiftishe Jane Jisandu (wa pili kushoto) akifurahia mfano wa hundi  kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa (wa pili kulia). Wanaoshguhudia wa kwanza kushoto ni mtangazaji wa radio clouds FM Mina Ally na wa kwanza kulia ni Deogratius  David kutoka Tigo.
 . Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni kumi katika Promosheni ya Tigo igiftishe Jane Jisandu (wa pili kushoto) akifurahi jambo  na mmoja ya rafiki zake wa karibu  alyefika kushuduia akikabidhiwa zawadi yake mwishoni mwa wiki Kivule jijini Dar es Salaam.
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni kumi katika Promosheni ya Tigo igiftishe Jane Jisandu (wa tatu  kushoto) akiwa kaika picha ya pamoja na washindi wa shilingi milioni moja moja na wafanyakazi wa Tigo muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake Kivule jijini Dar es Salaam
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja katika Promosheni ya Tigo igiftishe Anna Lyimo (wa tatu kushoto)akifurahi jambo na Mkurungenzi wa Tigo kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa (wa pili kulia) pamoja na mtamgazaji wa radio Clouds FM Mina Ally (wa pili kulia) muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake. Wengine ni wafanyakazi wa Tigo Alex Msigala (wa kwanza kushoto) na Deogratius David(wa kwanza kulia )

Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja katika Promosheni ya Tigo igiftishe Anna Lyimo (wa tatu kushoto)Abrahaman Kasimu  (wa pili koshoto) akitoa ushudumua namna alivyoshinda muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake. Wa kwanza kushoto ni mtangazaji wa radio Clouds Mina Ally na wa kwanza kulia ni Deogratius David kutoka Tigo.



Mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam Bi Jane Jisandu, ameibuka mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni kumi katika promosheni inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo.

Jane anakuwa mshindi wa tano wa zawadi ya shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga wote wa Dar es Salaam, Mbwana Mbela mkazi wa wMpwapwa mkoani Dodoma na Flora Somba wa Morogoro.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake Kivule jijini Dar es Salaam, Jane alisema zawadi hiyo ni muujiza na kuongeza kuwa itasaidia kuokoa maisha ya mwanaye ambaye anatakiwa kwenda India kwa ajili ya matibabu.

“Kwangu huu ni muujiza mkubwa sana. Nina mtoto mgonjwa na ambaye nimeambiwa anaweza kutibiwa lakini mpaka nchini India. Gharama za matibabu yake ni kubwa, nilikuwa nikiwaza wapi ningepata fedha za matibabu lakini Mungu amenitendea muujiza kupitia Tigo, naishukuru Tigo kwa kuokoa maisha ya mwanangu,” alisema

Jane alisema amefanikiwa kushinda zawadi hiyo baada ya kuwa antumia huduma za Tigo kama kuweka kuma wa maongezi, kununua vifurushi mbali mbali pamoja na kutuma pesa kwa njia ya Tigo Pesa huku akiwataka watu kutumia huduma za Tigo ili kujishidia zawadi za fedha taslimu.

Akimkabidhi zawadi kwa mshindi wa shiligi milioni kumi na wengine wa shilingi milioni moja moja,Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa alisema anayofuraha kuona zawadi za fedha zinazotolewa katika Promosheni ya Jigiftishe zinagusa na kubadilisha maisha ya wateja wa Tigo

Mutalemwa aliwataka wateja wa Tigo kuendelea kutumia huduma za kampuni hiyo ili kujishindia zawadi za fedha taslimu na kuongeza kuwa zawadi za fedha bado ni nyingi ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa za shilingi milioni 50,25 na 15 anbazo zitaolewa mwishoni mwa Promosheni 



No comments: