Friday, December 7, 2018

KAMPUNI YA GOOD JOB ENTERTAINMENTS YANDAA SAFARI YA KUTEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii

KAMPUNI ya Good Job Entertainments imesema imeona umuhimu wa kutoa fursa kwa Watanzania kuwa na mazoea ya kutembelea utalii wa ndani zikiwamo mbuga za wanyama.

Hivyo kampuni hiyo imeamua kuandaa safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Tarangire mkoani Manyara katika msimu huu Sikukuu ya Krismass ambapo Mratibu wa Safari ya keenda Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Juma Mtetwa amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa safari hiyo itaanza Desemba 24 na kurudi Desemba 26 mwaka huu.

Amefafanua lengo la kuandaa safari hiyo ni kuhamasisha na kuuza elimu ya maisha ya wanyamapori na kupata muda wa kumpumzika katika msimu huu wa Sikukuu ya X-Mas huku akisisitiza uamuzi huo pia unalenga kuunga mkono kauli mbili ya kuhamasisha utalii wa ndani vitendo.

"Washiriki wa safari hiyo wanatakiwa kufanya maombi ya ununuzi wa tiketi mapema Good job Entertainment ambapo Bibi na Bwana itakuwa Sh.350,000 na kwa mtu mmoja ni Sh.200,000,"amesema.Kwa upande wake Ofisa Masoko wa Tarangire National Park Gedfrey Mbona amesema kuwa 

Watanzania watumie fursa ya kuhamasika kutembelea utalii wa ndani ambao baada ya hapo watakuwa mabalozi wazuri wa kuelezea utalii wetu kwa wageni wanaotoka nchi mbalimbali kuja nchini."Tarangire ni nyumbani kwa tembo kwani kuna idadi kubwa ya wanyama hao kuliko mbuga zote hapa nchini.Pia kwenye hifadhi zetu tunao Simba, Duma, Chui, Twiga na wengine wanyama wengine wengi.Tumeajindaa vizuri kuwapokea watalii wetu na tunaimani mtakaporudi majumbani mtakuwa wajumbe wazuri kwa wengine,"amesema.

Aidha Mtetwa amesema kabla ya kufika Mbugani huko, Desemba 24 wakazi wa Babati watapata fursa ya kuonesha vipaji vyao katika onyesho la mitindo ya mavazi (Phinar Fashion Show) mjini hapo mkoani Manyara.Wakati huo huo Mkurugenzi wa Dreams & Ligacies Investment Anthony David amesema kuwa wao watashirikiana na kampuni ya Kampuni ya Good job Entertainments kuandaa tamsha hilo na kwamba hawataishia hapo kwani watandaa na mengine.

"Tutaungana na wakazi wa Babati kwenye onesho la mitindo ya mavazi (Phinar Fashion Show) na lengo ni kukuza vipaji vya vijana katika tasnia hiyo.Pia tutatoa fursa kwa vijana hao kuja Dar es Salaam kuonesha maonyesho yao, bila kusahau tutasaidia kutoa ushauri kwa wanandoa 
na kuwatengenezea mahusiano mazuri katika msimu huu mzuri wa Sikukuu ya X-Mass,"amesema.

No comments: