Friday, December 7, 2018

Hafla ya kuwapongeza Waalimu Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela yafana



Diwani Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Godlisten Kisanga (CCM) akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha pamoja na waalimu wote wa Shule tatu za Msingi (Nundu, Nundu D na Nyamwilekelwa) katika Kata hiyo iliyolenga kuwapongeza waalimu hao kwa juhudi zao za kuimarisha ufaulu kwa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba.
Afisa Elimu Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Mwl. Agnes Mugyabuso (kushoto), Shule zilizofanya vizuri kwa kila somo katika Kata hiyo kwenye mtihani wa darasa la Saba mwaka huu ambapo Shule hizo zilikabidhiwa cheti cha pongezi na Diwani wa Kata ya Mecco, Godlisten Kisanga.
Diwani Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Godlisten Kisanga (kulia), akimkabidhi Cheti cha pongezi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamwilekelwa, Mwl. Lyatura Mukama (kushoto) baada ya Shule yake kuibuka kidedea kwenye masomo ya Kiswahili na Kiingereza.
Alama za ufaulu/ ushindi zilizoshindanishwa ni A na B tu
Diwani Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Godlisten Kisanga (kulia), akimkabidhi Cheti cha pongezi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nundu D, Mwl. Lucas Robert (kushoto) baada ya Shule yake kuibuka kidedea kwenye masomo ya Hisabati na Maarifa ya Jamii.
Utaratibu huu wa kushindanisha Shule za Msingi Kata ya Mecco umelenga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa alama A na B tu.
Diwani Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela, Godlisten Kisanga (kulia), akimkabidhi Cheti cha pongezi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nundu, Mwl. Charles Njuka (kushoto) baada ya Shule yake kuibuka kidedea kwenye somo la Sayansi.
Mtendaji Kata ya Mecco akitoa neno la pongezi kwa waalimu wa shule za Msingi katika Kata hiyo.
Diwani wa Kata jirani ya Buzuruga, Richard Machemba (Chadema), akiwasilisha salamu zake za pongezi kwenye hafla hiyo.
Mwakilishi wa mbunge Jimbo la Ilemela, akiwasilisha salamu zake.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Mecco, Charles Matiku akiwasilisha salamu zake kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Manispaa ya Ilemela, Mohamed Yusuph akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo aliahidi kuanzia mwakani atasaidia kudhamini mitihani mbalimbali ya ushindani ili kuwajengea uwezo zaidi wanafunzi.
Baadhi ya waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Mecco wakiwa kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Mecco wakiwa kwenye hafla hiyo.
Diwani wa Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Godlisten Kisanga (CCM) amewapongeza waalimu wote wa Shule za Msingi katika Kata hiyo kwa juhudi zao za kuhakikisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kinazidi kuongeza.

Kisanga alitoa pongezi hizo jana Disemba 06, 2018 kwenye hafla ya chakula cha pamoja na waalimu hao kutoka Shule za Msingi Nundu, Nundu D na Nyamwilekelwa iliyolenga kuwapongeza na kukabidhi vyeti vya pongezi kwa Shule zilizofanya vizuri kwa kila somo kwenye matokeo mtihani wa darasa la saba.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments: