Saturday, December 22, 2018

DKT. ABBASI: SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI HAKI ZA WAANDISHI WA HABARI

Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mara baada ya kuwasili katika semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambako Dkt. Abbasi alikuwa Mgeni Rasmi.
3
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala( wa tatu kulia)  akitoa moja ya maada zilizokuwa zikijadiliwa kwenye Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam,  kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Ofisi ya Shekhe Mkuu wa Tanzania, Haris Othmani na Kushoto ni `Mkurugenzi Mkuu TAMWA Eda Sanga, Mwanyekiti wa Blogu (Bloggers ) Joachim Mushi, Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Hassan Abbasi wakifuatilia semina hiyo.
4
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina ya Jukumu la Mwanahabari wakati wa utoaji maada katika semina hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
5
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina Jukumu la wanahabari wakati wa utoaji maada katika semina hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi wakifuatilia semina hiyo.
6
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akitoa hotuba fupi kuhusu maada ya  uhuru wa habari kwa mwandishi katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akifuatilia hotuba hiyo.
7
9
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo  kuhusu maada ya uhuru wa habari kwa mwandishi katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akifuatilia hotuba hiyo na kushoto ni Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa wakifuatilia maada hiyo.
10
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa dini pamoja na watoa maada katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
……………………

Na Mwandishi Wetu,MAELEZO,DAR ES SALAAM.

SERIKALI imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi  na kuimarisha misingi ya haki na wajibu ya waandishi wa vyombo vya habari nchini ili kuwawezesha kutekeleza vyema majukumu yao yaliyoanishwa katika Mikataba na Sheria mbalimbali za kitaifa na Kimataifa.

Hayo yamesema leo Jumamosi (Desemba 22, 2018) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu ya Shia Ithsheriya.

Dkt. Abbasi alisema kwa kuzingatia Mikataba na Sheria mbalimbali za Kimataifa ikiwemo Kifungu cha 19 cha Mkataba wa Kimataifa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kiutendaji ili kuhakikisha maboresho na tasnia ya habari na utangazaji inapiga kubwa za maendeleo.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema moja ya mafanikio ya Serikali ni pamoja na kutungwa kwa Sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari na Sheria Haki ya Kupata Taarifa ambazo kwa kiasi zimeweka mazingira wezeshi ikiwemo kuwepo kwa vipengele vya kisheria zinazopaswa kutekelezwa na Taasisi za umma na Binafsi katika utoaji na upatikanaji wa taarifa kwa umma.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema pamoja na kuwepo vya vipengele hivyo vya kisheria, Serikali pia iliamua kuweka kipengele cha haki ya ukusanyaji, usambazaji na upatikanaji wa taarifa katika jamii kupitia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo pia imewazesha waandishi wa habari kutekeleza vyema majukumu yao.

“Katika Sheria hizi kwa mara ya kwanza katika historia ya Nchi yetu na hata Bara la Afrika kwa ujumla wake, waandishi wa habari wamepewa haki tatu za msingi ambazo ni pamoja na Haki ya kukusanya Habari, Uhuru wa Kuhariri Habari pamoja na Uhuru wa kusambaza Habari, na hili limendelea kuwafanya kutekeleza vyema wajibu wao” alisema Dkt. Abbasi.

Aidha Dkt. Abbasi alisema Serikali kwa kutambua misingi ya haki na wajibu wa vyombo vya habari nchini kupitia mikataba mbalimbali ya kimataifa na Sheria za Kitaifa, waandishi wa habari wameendelea kupewa fursa kwao ya kueleza hisia zao katika masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa masuala mbalimbali ya kitaifa nchini.

Akifafanua zaidi Dkt. Abbasi alisema iwapo waandishi wa vyombo vya habari nchini wataweza kutambua wajibu na haki walionao katika jamii, itawawezesha utekelezaji wa haki zote za msingi zilizoanishwa kwa mujibu wa misingi ya kimataifa na Sheria mbalimbali za Kitaifa.

Awali Kiongozi Mkuu wa  Jumuiya ya Waislamu ya Shia Ithsheriya, Sheikh Hemed Jalala alisema nafasi ya waandishi wa habari katika jamii ni sawa na mitume ya mungu kwa kuwa wanawajibika kutambua maadili mema katika jamii ikiwemo kuhamasisha umoja, upendo na mshikamano ndani ya jamii.
Sheikh Jalala alisema waandishi wa vyombo vya habari watatakiwa kutafuta, kusambaza habari zilizo sahihi mbele ya jamii, kwa kuwa jukumu hilo la msingi litawezesha jamii kuishi katika mazingira yenye utulivu na kuimarisha misingi ya amani na utulivu.

No comments: