Thursday, December 6, 2018

AGIZO LA WAZIRI LUGOLA KWA WANANCHI AMBAO HAWAJAPATA KITAMBULISHO CHA TAIFA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (aliyemshika mtoto), akitoka mkutanoni baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimpongeza mwanachama mpya wa CCM, Andrea Mutesigwa (kulia) ambaye amerudisha kadi ya Chadema katika Mkutano wa Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Katika mkutano wake na wananchi hao, Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. 


Na Felix Mwagara, (MOHA), MARA. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. 

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nansimo, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola amesema katika Mkoa na mikoa mingineyo zoezi la kujiandikisha lilishakamilika ila wale ambao hawakuandikishwa kipindi kile ambacho Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wanaandikisha wananchi mitaani, wanapaswa kwenda katika ofisi Wilaya za Mamlaka hiyo ili waweze kujiandikisha. 

“Wapo ambao kipindi kile NIDA wanaandikisha wananchi mitaani hawakuwepo hilo nalijua, na pia kuna wale ambao kipindi kile zoezi la kuandikishwa linafanyika walikua hawajafikisha miaka 18, hao wote ambao hawajaandikishwa wanapaswa sasa kwenda kujiandikisha haraka iwezekanavyo katika ofisi za NIDA katika Wilaya zao,” alisema Lugola. 

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara aliongeza kuwa, zoezi la vitambulisho vya utaifa ni lalazima kwa kila mtanzania aliye hapa nchini, ni kosa bwa kama wewe ni raia akaamua kukaidi ikiwa Rais Dk John Magufuli ameamua kutoa vitambulisho hivyo bure bila malipo yoyote nchini. 

“Ndugu wananchi wa Mwibara na kote nchini, kupata kitambulisho ni jambo kubwa la nchi hivyo tusililinganishe na jambo lingine lolote na tusilichukulie kirahisirahisi tu, na ninawaambia baada ya mchakato huu kuisha tukamkuta mtu hana kitambulisho maelezo yake yatakuwa ni magumu kueleweka kama kweli yeye ni mtanzania halali,” alisema Lugola.
 
Lugola alisema kwa Mkoa wa Mara tayari zoezi lilikamilika na kinachofanyika sasa ni Kuhakiki, kuyafanyia kazi mapingamizi pamoja na Uchakataji, likikamilika zoezi hilo kwa wale waliojiandikisha na ambao wana sifa watapewa vitambulisho vyao. 

“Hakuna Mtanzania mwenye sifa atakayekosa kitambulisho cha taifa, lakini lazima muwe na subira wakati zoezi la utambuzi wa watu gani wanaweza kupata vitambulisho hivi, na pia katika utambuzi tunapaswa kuwa makini sana kwasababu tusije tukapenyeza wasio raia wasiostahili na wao wakaweza kupata vitambulisho na baadaye tukaja kupata shida,” alisema Lugola. 

Aidha, Waziri Lugola aliwataka wananchi wa jimbo lake waanze maandalizi ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara ili kuepuka janga la njaa lisije liwakumba endapo hawata lima. Hata hivyo, kijiji hicho alichokitembelea, kwa mujibu wa taarifa ya mipango yao ya kilimo walisema kuwa wana upungufu mkubwa wa mbegu za mazao mbalimbali hasa zao la pamba. 

Lugola anaendelea na ziara yake kwa kutembelea vijiji vyote jimboni kwake Mwibara akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.

No comments: