Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
Na Mathias Canal-WK, Mtwara
Wakulima
wa zao la korosho wa Wilaya ya Tandahimba na Masasi wamekubali kuuza
korosho zao mbele ya Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb)
kutokana na kuridhia na kukubaliana na maamuzi ya serikali.
Hayo
yamejili katika mnada wa nne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019
uliojumuisha kampuni za ununuzi 11 katika maghala tofauti uliofanyika
katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba,
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba alisema kuwa bei ya zao la
korosho imeonyesha mwelekeo wa kushuka katika mwaka 2018/2019 tofauti na
hali ilivyokuwa katika msimu wa mwaka 2017/2018 ambapo bei ya zao hilo
ilifikia shilindi 4,128
Katika
mkutano huo wakulima wa korosho walikubali mbele ya waziri wa kilimo
Mhandisi Dkt Tizeba kuanza kuuza korosho zao kwa bei ya juu ya shilingi
3,016 huku bei ya chini ikiwa ni shilingi 3000.
“Wafanyabiashara
wasipangiwe muda wa kuchukua korosho ghalani kwa ajili ya usafirishaji
na wasipangiwe kutumia bandari gani, wawe huru kulingana na maagizo
yaliyotolewa na Rais Magufuli’’
“Nitashangaa
sana kuona mnunuzi mwenye akili timamu akitoa barua na kutaka kuuziwa
korosho chini ya shilingi 3,000 au akitaka kwa shilingi 2,500”
Alikaririwa Dkt Tizeba
Kufuatia
hali hiyo tarehe 26 Octoba 2018 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Kassim Majaliwa alitangaza maamuzi ya serikali kusimamisha
minada yote hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Kufuatia
uamuzi huo tarehe 28 Octoba 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alikutano na wanunuzi wa zao la
korosho katika mkutano uliokuwa ukiendelea kati ya wanunuzi hao na
Waziri Mkuu na kutoa msimamo wa serikali kuhusu zao hilo kufuatia kuwepo
kwa mvutano wa bei ya zao hilo kati ya wanunuzi na wakulima.
Katika
mnada huo wa nne uliohudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe
Gelasius Gasper Byakanwa, Waziri wa kilimo Dkt Tizeba alisema kuwa
matokeo ya mnada huo hayakuwa mabaya ukilinganisha na minada iliyopita
katika msimu huu wa 2018/2019 ambapo bei ilishuka.
Alisema
baada ya Rais Magufuli kutangaza msimamo wa serikali kuwa bei ya
kiwango cha chini ya mnadani katika msimu wa 2018/2019 kuwa shilingi
3000 kwa kilo moja ya korosho, wafanyabiashara wameitikia wito kwa
kuweka bei nzuri mnadani.
Aidha,
Waziri wa kilimo alisema kuwa katika vikao vingi vya serikali
vilivyotuama kujadili mwenendo wa zao hilo kwa mujibu wa kifungu cha 8
cha sheria ya Tasnia ya Korosho Na 18 ya mwaka 2018 ameielekeza Bodi ya
korosho kupata kibali cha waziri wa kilimo na waziri mkuu kabla ya
kuyafanyia maamuzi.
Alisisitiza
kuwa mnunuzi akishalipa ushuru katika Halmashauri moja hapaswi kudaiwa
kulipa ushuru huo katika Halmashauri nyingine, Bodi kutotoa bei elekezi,
Tozo ya Bodi ya korosho ambayo iliongezwa kwa msimu wa mwaka 2018/2019
kufikia shilingi 17 kwa kilo irudi shilingi 10 kwa kilo kama ilivyotozwa
msimu wa 2017/2018
Wanunuzi
wa korosho wana hiari ya kusafirisha korosho kwenda nje ya nchi kupitia
bandari ya mtwara, Dar es salaam au Tanga huku wanunuzi wakiruhusiwa
kwenda na magunia yao kununua korosho ya wakulima, Bodi ya korosho
kuangalia utaratibu wa wabanguaji wadogo kupata/kununua korosho katika
mfumo wa mnada, sambamba na dhamana ya mnada (Bill Security) kupungua.
Dkt
Tizeba alisema kuwa baada ya maelekezo ya serikali kuhusu mwenendo wa
zao la Korosho katika hatua ya kwanza ya utekelezaji Wizara yake ilianza
kutathmini kuhusu mfumo mzima wa uuzaji wa korosho hatimaye kufikia
uamuzi huo.
Aliwasisitiza
wakulima kutokata tamaa na minada kwani ni kawaida kwa bei za mazao
kupanda na kushuka kulingana na uzalishaji katika nchi zingine pamoja na
soko la Dunia.
No comments:
Post a Comment