Wednesday, November 21, 2018

Vikosi kazi vya TNBC vyazinduliwa rasmi

Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Balozi John Kijazi(kushoto) akisalimia na Kaimu Katibu Mkuu wa TNBC Bi.Oliver Vengula(kulia) mara baada ya kuwasili katika kikao cha uzinduzi wa vikundi kazi vinne vya Baraza hilo jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF) Salum Shamte na wapili kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Prof.Faustine Kamuzora
Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Balozi John Kijazi akizungumza jambo na wajumbe wakamati tendaji wakati wa uzinduzi wa vikundi kazi vinne vya Baraza hilo jijini Dar es salaam zitakavyoleta mapendekezo ya kuboresha sera ,sheria na miongozi ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.


KATIBU Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara(TNBC), Balozi John Kijazi amezindua vikundi kazi vya baraza hilo kwa lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kuibua changamoto na
kuzijadili kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa vikundi kazi hivyo jijini Dar es salaam juzi, Balozi Kijazi alisema madhumuni ya kuunda vikundi kazi hivyo vilivyowajumuisha wataalum katika sekta mbalimbali vitawezesha majadiliano juu ya changamoto zajadiliwe kwa kina zaidi kabla ya
kupelekwa katika ngazi ya Baraza.

“jumla ya vikundi kazi vinne nimevizindua leo (juzi) ikiwa ni pamoja na kikundi kazi cha Mazingira ya Biashara, Viwanda, Misitu na Kilimo vitavyokwenda kuibua changamoto na kuleta mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sera na miongozo iliyopo,” alisema Balozi Kijazi. Alisema ushirikiano kati ya sekta binafsi na Sekta ya umma unahitajika sana ili kuweza kuibaini changamoto na kuzijadili na kuja na mapendekezo yatakayo leta tija katika mustakabali wa kujenga uchumi wa
Taifa.

“Serikali itapokea mapendekezo yote yatakayowakilishwa na timu za wataalum kutoka katika vikundi kazi hizi na tutayafanyia kazi mapendekezo yote, zaidi kwa mengine yanayoweza kuchukuliwa na maamuzi kwa ngazi yenu endeleeni lengo ni kupunga majadiliano katika ngazi ya
taifa,” alisema Balozi Kijazi Alisisitiza kuwa mijadala ya vikundi kazi hivi ifanyike kwa uhuru na
usawa kwa kutoa hofia cheo cha mtu au mali wote wawekitu kimoja ili majadiliano yaweze kuleta tija na mapendekezo yatakayofanya mazingira ya biashara kuboresheka zaidi.

“Vikundi kazi hizi vikapitiwe Sera,Miongozo na Sheria zilizopo ili waje na mapendekezo yatayoboresha mazingiria ya biashara kuwa rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara nchini,” alisema Alisema kuwa kumekuwa na malalamiko mengi juu ya tozo , mamlaka za uthibiti na kero mbalimbali katika uanzishaji wa biashara nchini hivyo ni muhimu vikundi kazi hizi zikajana na mapendekezo katika maeneo hayo ili tuyafanyie kazi.

“Uongozi wa awamu ya tano umefanikiwa kupunguza baadhi ya changamoto ikiwemo utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara, hivyo ni matumaini yangu tutakwenda kumaliza kabisa changamoto zilizopo na kupelekea nchi yetu kupiga hatua kiuchumi,” alisema Balozi Kijazi. Pia Balozi Kijazi alisema kikosi kazi cha kilimo kisimamie utekelezaji wa nguzo kumi za kilimo kwanza na pia kufanya mapitio ya Mpango wa Awamu ya Pili wa Maendeleo ya Kilimo(ASDP- II) na kuleta mapendekezo
ya utekelezaji wake.

“Lengo letu ni kutizima azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025, vikundi kazi hizi ndiyo vitatupa mwanga wa kufikia malengo kwa kuja na mapendekezo yenye tija na utekelezaji ufanywe maendeleo yapate kuonekana,” alisema Balozi Kijazi kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF)Bw.Salum Shamte ambaye pia mwenyekiti mwenza wa kamati tendaji ya baraza alisema kuundwa kwa vikundi kazi hizi kumeonyesha
nia ya dhati ya Sererikali ya kuboresha mazingira ya biashara nchini.

“Sisi sekta binafsi tumefurahiswa na hatua zinazofanywa na Serikali, ushirikiano wetu katika kivundi kazi hizi utakuwa mkubwa na mapendekezo yanayotakiwa katika kuboresha sera ,Sheria tutawasilinao Serikai ili yafanyiwe kazi,” alisema Bw.Shamte alisema lengo kubwa ni kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini na hii ni kutoakana na kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji katika hatua za kuwekeza nchini.

Mwenyekiti wa Kikundi kazi cha Mazingira ya Baishara ambaye pia ni Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora alisema atakwenda kushirikiana na wajumbe wenzake wa kamati hiyo kuibua mapendekezo yatayosaidia kuboresha mazingira ya biashara
nchini.

No comments: