Tuesday, November 6, 2018

UWT PWANI YAMPA SALUTE RAIS .DK MAGUFULI KWA UTEKELEZAJI NA KASI YA MAENDELEO NCHINI

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI .

JUMUIYA ya wanawake ya Chama Cha Mapinduzi (UWT) mkoani Pwani, imempa big up ,Rais Dk. John Magufuli kwa kasi yake ya utekelezaji katika sekta mbalimbali, ikiwemo miradi ya REA awamu ya III kwa vijiji 150 na mradi mkubwa wa Rufiji Hydropower utakaozalisha 2,100MW baada ya kukamilika .

Aidha wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutenga bajeti ya bilioni 12.4 kwa ujenzi wa vituo 18 vya afya mkoa mzima na hospital tatu Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Kibiti. 

Awali akiishukuru serikali Mbunge wa viti maalum mkoani hapo, Subira Mgalu, wakati wakisheherekea miaka mitatu ya Rais Magufuli akiwa madarakani, sherehe iliyodhuriwa pia na kamati ya utekelezaji ya UWT mkoa. Anasema"Nikianzia sekta nayoisimamia nikiwa naibu waziri wa nishati nampongeza kupitia uongozi wake na maelekezo yake kuwasilisha bajeti ndani ya bunge ,wizara ya nishati imekuwa ikipata ongezeko kila mwaka "

"Wakati akiingia madarakani mh Rais alikuta asilimia 38 ya wanapata huduma za umeme lakini sasa ni asilimia 60 wamepata umeme kupitia miradi iliyokaribu nao, na miradi ya umeme vijijini "alifafanua Subira. Subira alielezea, kuna REA awamu ya tatu ambayo inaendelea ambapo vijiji 7,873 vilikuwa havina umeme lakini kwa kazi inayoendelea mzunguko wa kwanza vijiji 3,559 vinafanyiwa kazi na wakandarasi wapo kazini .

Alibainisha kwamba, kulikuwa na mradi wa ujazilizi ambapo vijiji 105 vimepata umeme na wananchi zaidi ya 25,000 kwenye mikoa nane ukiwemo nane wameunganishiwa umeme na mradi unaendelea .Hata hivyo alisema, serikali hiyo imeweza kufanikisha miradi ya maji katika miji ya Bagamoyo, Kibiti ,Utete pamoja na mradi wa maji WAMI -Chalinze ,Ruvu -Chalinze -Msoga, mradi wa maji katika miji ya Kisarawe na Mkuranga. 

Subira alitaja ujenzi wa barabara kwa makao makuu ya wilaya ya Kibaha, Kisarawe, Mkuranga na Bagamoyo na upatikanaji wa dawa za kutosha kwenye vituo vya afya, zahanati na hospital za wilaya. Nae mwenyekiti wa UWT Pwani, Farida Mgomi aliishukuru serikali kwa utoaji elimu bure kwa shule za msingi na sekondari .

Ukarabati wa miundombinu ya elimu kwa shule kongwe za sekondari Kibiti, Kibaha, Ruvu, Minaki ,Kikaro, Mtanga Delta, Nyamisati na shule za msingi maeneo mbalimbali mkoani hapo. Mgomi alitaja mafanikio mengine ,kuwa ni ununuzi wa boti kwa ajili ya visiwa vya wilaya za Rufiji ,Kibiti na Mafia milioni 600 .#

"Ujenzi wa gati la Nyamisati -Mafia bilioni14 ,miradi ya REA III kwa vijiji 150.Wajumbe hao kwa umoja wao walipongeza mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta mbalimbali kwa kipindi alichokuwepo madarakani Rais. Dk Magufuli. "alisema Farida. 

Wajumbe wote kwa umoja wao walipongeza jitihada zinazochukuliwa na serikali kutatua kero mbalimbali kwenye sekta ya afya, nishati, maji, elimu na huduma za kijamii . Walimtakia afya njema Rais,makamu wa Rais Samia Suluhu na waziri mkuu Kassim Majaliwa. 

No comments: