Wednesday, November 7, 2018

BREAKING NEWZZZZZ: CGP KASIKE AFANYA MABADILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA

Katika kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Martin Kasike amefanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi kwa kuwateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa Tanzania Bara(RPOs) 19 wapya na saba (7) kuwabakiza katika nyadhifa zao. 

Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali Kasike ameteuwa na kuthibitisha maafisa sita (6) kuwa Wakuu wa Vyuo vya Magereza na kuwabadilisha maafisa wengine watatu (3) katika vitengo muhimu ndani ya Jeshi hilo. 

Aidha, Kamishna Jenerali Kasike katika mabadiliko hayo kwa mara ya kwanza amewateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa katika mikoa ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita ambayo ilikuwa haina uongozi wa kimagereza katika ngazi ya mikoa hiyo. 

Katika mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa RPO (DSM) SACP. Hamis Nkubasi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kitengo cha Ujenzi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP. Julius Ntambala, SACP. Salum Hussein RPO (Dodoma) amebakia katika kituo chake na aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kiwira SACP. Luhende Makwaia anakwenda kuwa RPO (Mbeya) na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Mathias Mkama na aliyekuwa RPO (Mbeya) SACP. Kijida Mwakingi amehamishiwa Makao Makuu, Kitengo cha TEHAMA. 

Aliyekuwa RPO (Mtwara) SACP. Ismail Mlawa amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Mipango na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Varisanga Msuya aliyekuwa Kaimu Bohari Mkuu wa Jeshi ambapo nafasi yake inachukuliwa na ACP. Robert Masali ambaye anakuwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza. Aliyekuwa RPO (Mwanza) SACP. Athuman Kitiku amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza sehemu ya Utumishi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP. Hamza Hamza aliyekuwa RPO Tabora. 

Aidha, ACP. Joseph Mkude anakuwa RPO (Tabora) na aliyekuwa RPO (Kagera) SACP. Boyd Mwambingu amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Utawala na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Rymond Mwampashe. Aliyekuwa RPO (Lindi) SACP. Rajabu Bakari amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Mawasiliano na Usafirishaji na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Josephine Semwenda. 

Aliyekuwa RPO (Rukwa) SACP. Benno Hunja amehamishiwa Makao Makuu sehemu ya Kilimo, Mifugo na Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Jail Mwamgunda na aliyekuwa RPO (Kilimanjaro) SACP. Hassan Mkwiche amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Rajab Igongi. Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe ACP. Wilson Rugamba anakuwa RPO (Shinyanga). 

Pia, Aliyekuwa RPO (Morogoro) SACP. Mzee Nyamka amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Takwimu na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Stylvester Mrema. Aliyekuwa Kaimu RPO (Mara) ACP. Benezeth Bisibe amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mdhibiti wa Fedha (FC) na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Hospitius Adrian. Mkuu wa Mkuu wa Chuo KPF ACP. Lazaro Nyanga anabakia katika nafasi hiyo, ACP. Anthony Sogoseye anabakia kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani. Aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa chuo Ruanda SSP. Enock Mwanguku anakuwa Mkuu wa Chuo hicho. 

Aidha, waliokuwa Kaimu RPOs, Vyuo na maeneo mengine ambao sasa wamethibitishwa ni kama ifuatavyo:- ACP. Hasseid Mkwanda (Iringa), ACP. Anderson Kamtearo (Arusha), ACP. Emmanuel Lwinga (Tanga), ACP. Masudi Kimolo (Manyara), ACP. Joel Matani (Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji), ACP. Rehema Ezekiel (Pwani), ACP. Msepwa Omary (Singida), na SP. Ally Uwesu (Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza). 

Walioteuliwa kuwa RPOs katika mikoa mipya ni ACP. Alexander Mmassy (Katavi), ACP. Lyzecky Mwaseba (Songwe), ACP. Festo Ng’umbi (Njombe), ACP. Robert Rumanyika (Geita) na ACP. Andulile Mwasampeta (Simiyu). Wakati huo huo ACP. Alexander Nyefwe anakuwa RPO (Ruvuma) na ACP. Leonard Burushi anakuwa RPO (Kigoma) kufuatia waliokuwa RPO katika mikoa hiyo kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria. 

Maafisa wengine waandamizi walioko Makao Makuu ambao wamepangiwa majukumu mengine ni SACP. Bertha Minde anakuwa Mkuu wa Kitengo cha Parole na SACP. Chacha Jackson ambaye anakuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Mahabusu. 

Kwa mujibu wa Kamishna Jenerali Kasike Maafisa wote waliohamishiwa Makao Makuu wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma.
   
Imesainiwa na; Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Deodatus Kazinja – Ofisa Habari,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM,
07 Novemba, 2018.

No comments: