Wednesday, November 28, 2018

UJUMBE MKUBWA WA SEKTA BINAFASI ZA MAFUTA NCHINI UGANDA WAONYESHA NIA YA KUPITISHA BIDHAA BANDARI YA TANGA

Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na Ujumbe Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea Bandari ya Tanga na  kuvutiwa kuitumia Bandari ya Tanga kupitisha bidhaa zao kutokana na uwezo wa kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 30 mpaka 45 ikiwemo kutumia muda mfupi kuhudumia shehena.
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza na UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akisalimiana na UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea ofisini kwake kabla ya kutembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine
 UJUMBE huo wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine wakitoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella mara baada ya kufanya naye mazungumzo
Mmoja wa wajumbe wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya mambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
 Sehemu ya ujumbe huo wakifuatilia kwa umakini mazungumzo hayo
 Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katika akiwa na baadhi ya wajumbe wakiwa eneo la  yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akitoa maelezo kwa  wajumbe hao wakati  wakiwa eneo la  yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.
Wakipata maelezo kutoka kwa Viongozi wa Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga GBP
 Ujumbe huo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutembelea eneo la Chongoleani Jijini Tanga
 Wakipata maelezo kutoka kwa Viongozi wa Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga GBP
 Wakipata maelezo kutoka kwa Viongozi wa Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga GBP

NA MWANDISHI WETU, TANGA.

UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda leo wametembelea Bandari ya Tanga huku wakionyesha nia yao ya kutumia Bandari ya Tanga kupitisha bidhaa zao kutokana na uwezo wa kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 30 mpaka 45 ikiwemo kutumia muda mfupi kuhudumia shehena.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya ujumbe huo kutembelea Bandari ya Tanga ikiwemo maeneo yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.

Alisema kwamba lengo la ujumbe huo kutua mkoani Tanga ni kuangalia fursa eneo gani ambalo wanaweza kupitisha bidhaa zao kutoka nchini Uganda kwenda kwenye soko la nje kwa gharama nafuu zaidi na kupelekwa pia eneo ambalo litapokelea mafuta, Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga ya GBP na sehemu ambayo mafuta yanaposhushwa (Gati ya Meli za mafuta).

“Kwa kweli tunawashukuru TPA makao makuu na Serikali kutuletea ujumbe huu mkubwa wa sekta binafsi za mafuta za Uganda wakiwemo Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano ya Uganda jambo ambalo linatusaidia kutangaza fursa kubwa tulionayo Bandari yetu ya Tanga “Alisema.

Alisema msingi wake wa kutumia muda mfupi wakati wa upitishaji wa bidhaa msingi wake ni meli kwenye Bandari ya Tanga inakuja moja kwa moja inapata gati tofauti na maeneo mengine unalazimika kusubiri kwa kipindi cha wiki moja mpaka mbili ambapo kitaalamu wanasema dunia kwenye biashara za bandari na meli katika kila sh, mia moja mwenye meli anaingia gharama ya s h.65 akiwa bandarini.

Aliongeza kwamba hivyo meli inapofika bandari na kuondoka gharama zake inashuka kwa kiwango kikubwa lakini pia inaweza kusababisha mambo ya kupigwa penati kutokana na kuchelewesha meli lakini kwa bandari ya Tanga hilo halipo.

Meneja huyo alisema jambo la pili ni kwamba wamekuta na mji ambao barabara zake zipo wazi za kutosha hivyo kuingia na kutoka bandarini hakuna haja ya kukutana na foleni sambamba na kushuhudia mifumo ya utengenezaji wa nyaraka ya kwamba wadau wote wanakaa jengo moja hivyo utengenezaji wake unakuwa wa kasi kubwa sana

Naye kwa upande wake Meneja wa Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga (GBP) Amour Ally alisema wanashukuru sana kupata ugeni kutoka nchini Uganda ambao wanataka kupitisha mafuta yao kwenye Bandari ya Tanga waliokwenda kuangalia miundombinu na uwezo walionao kwa sasa ambapo waliwaambia kwa sasa wanafanya kazi ni lita milioni 122 na laki tano.

Meneja huyo alisema wana uwezo wa kupeleka mzigo kwa njia ya reli kupitia Mwanza na wanaangalia uwezo wa kupakia mabehewa 20 kwenda Kigoma hivyo wana machagua mawili kutumia reli inayofanya kazi kwa sasa au kutumia magari 12 kwa wakati mmoja.

Aidha alisema kwamba pamoja na hayo alitumia nafasi hiyo kuwashawishi kuitumia bandari ya Tanga kupitisha bidhaa zao huku akiishukuru Serikali kwa kuweka miundombinu ya kisasa na kuwezesha mazingira mazuri kwa wawekezaji ikiwemo kusifu juhudi za kubwa za Bandari na kuwawezesha kushusha tani elfu 40 kwa siku mbili na nusu.

No comments: