Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (kushoto), Meneja Uhusiano wa Tigo Woinde Shisael (kati) pamoja na Balozi wa promosheni ya Tigo Jigiftishe, Lucas Mkenda almaarufu Joti (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Jigiftishe itakayowapa wateja wote watakaotumia huduma za Tigo katika msimu wa sikukuu fursa ya kushindania jumla ya shilingi 600 milioni.
Mkuu wa Masoko wa Tigo, Tarik Boudiaf (kushoto), Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (wa pili kushoto), Balozi waTigo Lucas Mkenda almaarufu Joti (katikati), Meneja Mawasiliano Woinde Shisael (wa pili kulia) pamoa na Mkuu wa Bidhaa za Tigo Pesa, James Sumari (kulia) wakizindua promosheni ya Jigiftishe itakayowapa wateja wa Tigo fursa ya kushinda hadi TSH 50 milioni katika msimu huu wa sikukuu.
Wateja watakaoongeza salio au kuweka Pesa Kwenye Tigo Pesa au Kutumia huduma yoyote ya Tigo watapata nafasi ya kushinda zawadi nono za hadi TSH milioni 50!
Dar es Salaam, 15 Novemba 2018; Tigo Tanzania - kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, itawezesha wateja wake kuwa mamilionea baada ya kuzindua promosheni kubwa zaidi itakayogawa kiasi cha TSH milioni 600 katika msimu huu wa sikukuu.
Promosheni hiyo ya kipekee ya ‘JIGIFTISHE’ kutoka Tigo katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya itawafanya zaidi ya wateja 450 kuwa mamilionea ndani ya siku 45, kutokana na kutumia huduma za Tigo pekee. Ni rahisi na hakuna kujiunga kwenye promosheni hii.
‘Wateja wa Tigo watakaoweka pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa, kuongeza salio au kununua simu janja kwenye maduka yote ya Tigo au kutumia huduma zozote za Tigo katika kipindi hiki cha sikukuu watapata fursa ya kujishindia TSH milioni 1 kila siku au TSH milioni 10 kila wiki. Pia kutakuwa na zawadi kubwa za TSH milioni 15, TSH milioni 25 au TSH milioni 50 zitakazotolewa mwishoni mwa promosheni hii ya JIGIFTISHE!’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Akibainisha vigezo vya ushiriki katika promosheni hiyo ya JIGIFTISHE, James Sumari, Mkuu wa Bidhaa za Huduma za Tigo Pesa wa Tigo alisema kuwa ili kupata fursa ya kushinda, wateja wa Tigo wanahitaji kununua kifurushi chochote kwa njia yoyote (ikiwemo kupitia *147*00#, *148*00# au kuongeza muda wa maongezi kwa njia ya kielektroniki, kadi au kupitia Tigo Pesa) au kufanya miamala ya Tigo Pesa kupitia *150*01# katika msimu huu wa sikukuu.
‘‘Ni rahisi sana! Hakuna kufanya kitu chochote maalum ili uweze kushinda. Unachohitaji kufanya ni kuendelea kutumia huduma au kununua bidhaa za Tigo ili upate nafasi ya kuwa milionea!” Woinde alisisitiza. Kila muamala utakaofanyika utampa mteja nafasi moja ya kushiriki katika droo, na wateja wanaweza kutazama nafasi zao za kushinda kwa kupiga *149*22#. Kadri unavyofanya miamala zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi za kushinda.
Promosheni hii ya JIGIFTISHE itakayojaza mifuko ya wateja na manoti na kubadilisha maisha yao inathibitisha kuwa Tigo ndio mtandao unaotoa huduma bora zaidi za kidigitali kwa wateja wake na kuwawezesha kufurahia msimu huu wa sikukuuu huku wakimaliza au kuanza mwaka mpya kwa mtindo tofauti.
‘Hii ndio njia yetu ya kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuendelea kutumia huduma zetu bora, zenye kasi ya juu na rahisi. Tunachukua fursa hii kuongeza tabasamu katika nyuso za wateja wetu,’ Woinde alisema.
Tayari wateja wa Tigo wanafurahia unafuu na urahisi wa kutumia huduma bunifu za Tigo kama vile kufanya miamala ya Tigo Pesa (kutuma na kupokea pesa ikiwemo kutoka mitandao mingine na benki), kulipia huduma mbali mbali kama vile LUKU, kufanya manunuzi kutoka kwa wafanyabiashara tofauti, kukamilisha malipo ya Kiserikali na pia kufurahia huduma bora za maisha ya kidigitali kwenye mtandao mkubwa zaidi wa 4G nchini.
No comments:
Post a Comment