Mtendaji mkuu Citi bank Tanzania joseph Carasso akizungumza. Mwingine ni wmenyekiti wa bodi ya Tamsi Joel Mwakitalu
Kwa mara ya tatu mfululizo, CITI Foundation ikishirikiana na Shirikisho la Asasi zinazotoa huduma ndogo za fedha (TAMFI), jana wamezindua awamu ya tatu ya tuzo za wajasiriamali za CITI (CITI Micro entrepreneurship Awards – CMA).Tuzo hizi zinalenga kutambua mchango mkubwa wa wajasiriamali kwenye kuinua uchumi wa familia zao na jamii zinazowazunguka.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Citibank Tanzania, Bw. Joseph Carasso, tuzo za CITI zimeshamiri na katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na mafanikio makubwa kwa wajasiriamali wadogo na walio wabunifu.
Washiriki katika uzinduzi
Watu walionufaika katika msimu uliopita wakizungumza umuhimu wa tuzo hizo
Mtendaji huyo alisema CITI inaamini kuwa wajasiriamali wadogo wenye ubunifu ndio wajasiriamali wakubwa wa kesho. Tunawathamini sana.Tuzo za wajasiriamali za CITI (CMA) zimekuwa alama kubwa ya utendaji wa kazi za Citi Foundation kwa zaidi ya muongo mmoja.
Tangu mwaka 2005, wakati zilipoanzishwa nchini Marekani tuzo za CITI, zimelenga kuleta mageuzi ya kiuchumi na fursa kwa wajasiriamali katika nchi zaidi ya nchi thelatini duniani kote.Hapa nchini katika awam,u ya tatu , CITI itatoa zaidi ya shilingi milioni 70 kwa washindi kumi na sita. Na tuzo hizi zitaweka alama na kutoa motisha kwa wajasiriamali na asasi zinazotoa huduma ndogo za fedha.
waandishi wa habaria wakirekodi tukio
Mtendaji wa TAMFI Terry akielezea hafla ya uzinduzi wa tuzo
waandishi kazini
Malengo ya Citi Foundation ni kufanikisha kuainisha huduma za fedha jumuishi na kuchangia Maendeleo endelevu (Sustainable Development Goal (SDG) 8,), ambayo pamoja na mambo mengine yanaainisha ajira zenye staha kwa wote.Akielezea zaidi, Bw Carasso, alisema kwamba tuzo hizi pamoja na kuinua viwango vya huduma za fedha jumuishi nchini zinasaidia mjasiriamali mmoja mmoja kuinua viwango vya maisha vya familia zao na jamii zinazowazunguka na Taifa kwa ujumla.
Hii inalenga moja kwa moja malengo ya SDG 9.3 ambalo linalenga kuongeza idadi ya wajasiriamali wadogo katika nchi zinazoendelea pamoja na huduma za kifedha katika mnyororo wa thamani na masoko.Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TAMFI, Bw Joel Mwakitalu, alisema kwamba “tuzo hizi ni chachu kwa wajasiriamali na wanachi kwa ujumla na kwamba kukopa na kurejesha katika biashara ni ufunguo wa maendeleo ya ki-uchumi.”
Aliongeza kwamba “kwa miaka miwili iliyopita, zaidi ya wajasiriamali 30 wamenufaika na tuzo hizi. Wajasiriamali hawa walipita katika mchujo uliokuwa na vigezo vya urejeshaji wa mikopo kwa muda uliopangwa, ukuaji wa biashara, ubunifu katika biashara, uzalishaji wa ajira, na bishara endelvu. Miongoni mwa wajasirimali waliofaidika na fedha hizo walikuwepo katika hafla ya uzinduzi kwa msimu wa 2018/19.
Wajasiriamali hawa waliopita kwenye mashindano haya walipata Zaidi ya Shillingi Milioni 140 ambazo tafiti zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya pesa hizi za tuzo zimeziwekeza kwenye biashara zao.” Tuzo hizi zitazingatia maeneo ya kijiografia, jinsia, na sekta za uchumi. Biashara itakayoshindanishwa ni lazima iwe endelevu, inaleta mabadiliko katika maisha ya mjasiriamali na jamii inayomzunguka. Kutakuwa na mshindi wa jumla na mshindi kutoka taasisi inayotoa huduma ndogo za fedha.
VIGEZO VYA TUZO
Wajasirimali wadogo wenye mafanikio ni lazima wawe wale ambao kwa juhudi binafsi wamesababisha mabadiliko makubwa katika shughuli zao, katika jamii na familia zao.
Maombi ya ushiriki yatachambuliwa kwa kuangalia yafuatayo:
Ukuaji wa kibiashara: Mjasirimali anatakiwa kuelezea historia ya biashara, ikoje kwa sasa, ilianza linin a ilianzishwaje, mapato na ukubwa wa mauzo wakati ananza na sasa na kiasi kinachouzwa kwa mwezi. Kwa sasa kuna matawi mangapi ukilinganisha na wakati alipoanza au kama utoaji huduma huo umetanuliwa au kubadilishwa.
Kutambua msukumo ulioletwa na biashara hiyo kwa biashara nyingine na faida ambazo wanunuzi au wateja wamezipata kutokana na kukua kwa biashara na kama biashara hizo zipi ndani ya jamii, nje ya wilaya au mbali zaidi.Uzalishaji wa ajira: je biashara imepanda kutoka kuwa na ajira ya mtu mmoja na kuajiri watuw engi wakiwemo wale ambao si wa familia moja.Watu wangapi waliajiriwa wakati wa kuanza na sasa wapo wangapi. Je jinsia katika ajira zikoje.
Uendelevu: je uendeshaji wa biashgara hiyo unaenda sawa na gharama zake, je imesajiliwa au inafikiriwa kusajiriwa?Je inategemea mafanikio ya mjasirimali au inajitegenmea na endelevu kwa kuzingatia msiungi uliowekwa?Ubunifu: je ni kitu gani kinafanywa tofauti ili kuifanya biashara kuwa na mafanikio?Je inatoa bidhaa adhimu? Je wameanzisha mawasilino ya Tehama au uhifadhi wa nishati ili kuendelezwa kwa ufanisi?
Nidhamu ya kifedha: je mshiriki ameonesha nidhamu ya fedha na hasa katika uwekaji wa akiba, urejeshaji wa mikopo na uwekezaji. Hapa anatakiw akuleta taarifa kamili inayohusu mikopo na akiba na historia yake.Manufaa kwa familia: Ni kwa namna gani biashara hiyo imeleta athari chanya kwa jamii. Je mafanikio ya biashara hiyo imewezesha kuboresha makazi, huduma za afya, elimu kwa watoto, afya na kadhalika. Onesha na mifano.
No comments:
Post a Comment