Monday, November 19, 2018

SERIKALI YAJENGA SEKONDARI YA MFANO KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI ARUSHA

picha 1
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wadau wa Elimu pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum ( Hawapo Pichani) katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
P2
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimpongeza mwanafunzi mwenye mahitaji maalum baada ya kufanya vizuri katika maonyesho ya mavazi katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro
P3
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti za kutambua mchango wa CCBRT wa udhamini wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports lililoshirikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum, ambapo alitoa wito kwa wadau wa Elimu kuendelea kushiriki katika kuboresha Elimu Maalum
P4
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akibadilishana mawazo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro
P5-min
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya Mgeni Rasmi Prof. Joyce Ndalichako (Hayupo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro iliyoshirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum

.......................

Serikali inajenga Shule ya Sekondari Maalum ya mfano kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Ualimu Patandi kilichopo mkoani Arusha yenye uwezo wa kudahili wanafunzi 600 kwa mara moja ikiwa ni mkakati wake wa kuongeza fursa za udahili kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo amesema Serikali imekarabati miundombinu kwenye shule kongwe ya Moshi Ufundi inayopokea wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Serikali inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali inayolenga kuongeza upatikanaji wa fursa na kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa katika ngazi zote kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo tayari serikali imekarabati miundombinu ya shule kongwe ya Moshi Ufundi ambayo inapokea wanafunzi wenye mahitaji maalumu”. Alisisitiza Prof. Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema watu wenye mahitaji maalum wana fursa sawa ya kushiriki katika michezo na kufanya hivyo kunasaidia kuondoa kasoro za kimwili na kiakili na baadhi ya ulemavu unaweza kurekebishwa kwa kushiriki katika michezo na burudani.

Prof Ndalichako amesisitiza kuwa ushiriki katika michezo, hususan kwa watoto wenye mahitaji maalum ni muhimu sana kama ilivyowekwa bayana katika kifungu cha 52 cha Sheria ya Watu wenye Ulemavu Namba 9 ya mwaka 2010 kinachosisitiza umuhimu wa Watu wenye ulemavu kushiriki katika michezo, starehe na burudani.

Akizungumza katika Bonanza hilo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) Stella Ikupa amewataka wanafunzi wenye mahitaji maalum kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kujitambua, kujikubali na kujituma ili kujikwamua katika changamoto wanazokutana nazo katika masomo yao.

Waziri Ikupa amewataka wanafunzi hao pia kujiunga na vyuo vya ufundi ambavyo vitawawezesha kupata satadi ambazo watazitumia kwa ajili ya kujiari wenyewe badala ya kuwa tegemezi.

Naye Mratibu wa Bonaza hilo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Vyuo Vikuu) Esther Mmasi amesema wakati wa maandalizi ya Bonanza hilo amebaini kuwepo kwa uhaba wa viwanja vya michezo katika shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo ameiomba serikali kuhakikisha inaboresha miundominu ili kuwajengea uwezo wanafunzi hao.

No comments: