Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph
akiwasisitiza Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kukamilisha
ujenzi wa ofisi kwa wakati katika Mji wa Serikali ili iweze kutumika
kuwahudumia wananchi.
Afisa Ugavi
Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Bw. Deograsius Michael (kulia) akikabidhi hati ya makabidhiano ya
kiwanja kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma,
Mhandisi David H. Shunu (kushoto) kwa lengo la kuanza ujenzi wa Ofisi
katika Mji wa Serikali. Anayeshuhudia ni Afisa Ugavi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Benard Makanda.
Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph (wa
pili kushoto) akizungumza na Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA) mara baada ya kukabidhi kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi
katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugezi
wa Huduma za Ushauri wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma,
akiahidi kutimiza jukumu lake ili kuhakikisha ujenzi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora unakamilika kwa wakati
katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha
Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Bw. Peter Mabale akisisitiza jambo kwa TBA ili kuhakikisha
ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma unakamilika kwa
wakati.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora imekabidhi kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili wakala
hiyo ianze ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.
Akikabidhi kiwanja hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Musa Joseph amesema ujenzi wa Ofisi hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais, Dkt John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za Serikali Makao Makuu ya nchi Dodoma.
Bw. Joseph amefafanua kuwa, kiwanja kilichokabidhiwa kina ukubwa wa ekari 5.7 na kuwataka TBA kuanza ujenzi mara moja ili kuwawezesha watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwahudumia wananchi wakiwa katika mji wa Serikali.
Bw. Joseph ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tayari imeshaingiza fedha kwenye Akaunti ya Wakala wa Majengo Tanzania kiasi cha shilingi 700, 000,000/= ili kuiwezesha TBA kuanza ujenzi na kuongeza kuwa nia ya kufanya malipo mapema ni kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi kwa wakati.
Akipokea kiwanja hicho, Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania mkoani Dodoma, Mhandisi David H. Shunu ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuiamini TBA na kuahidi kukamilisha ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati na kwa kiwango bora.
Naye, Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Peter Mabale ameitaka TBA kufanya mawasiliano haraka iwezekanavyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pindi kunapotokea changamoto yoyote itakayokwamisha shughuli ya ujenzi badala ya kusubiri vikao ili kutatua changamoto hizo.
Makabidhiano ya Kiwanja hicho yamefanyika baada ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalinga kusaini mkataba wa ujenzi wa Ofisi hizo Novemba 22, 2018 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kuhamishia Shughuli za Serikali makao makuu ya nchi Dodoma.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekabidhi kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili wakala hiyo ianze ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

No comments:
Post a Comment