Friday, November 2, 2018

MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA


Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

KUFUATIA operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu ndani ya Ziwa Tanganyika inayoendelea Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza zana mbalimbali za uvuvi haramu zenye zaidi ya shilingi bilioni tatu zilizokuwa zikitumika katika ziwa Tanganyika.

Akiongea na wananchi baada ya zoezi la kuteketeza zana hizo haramuza uvuvi katika eneo la Businde nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mpina amewataka wananchi kushirikiana na serekali kwa kuwafichua wahalifu wanaotumia zana haramu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini na kwenda jela.

Alisema serekali haitomuonea mtu yoyote huruma ambayeatakamatwa anafanya uvuvi haramu au kuwa na zana za uvuvi haramu awe kiongozi au raia wa kawaida sheria lazima ichukue mkondo wake.''Sisi lengo letu ni kuona samaki wanaongezeka katika ziwa Tanganyika,na watu wavue kwa kufuata sheria ili Taiafa lipate mapato na watu wapate ajira"alisema

Alisema oparesheni inayofanyika katika ziwa Tanganyika ni oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo itaendelea katika maeneo yote ya ziwa Tanganyika lengo likiwa ni kuondoa uvuvi haramu na mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia samaki wachanga na utoroshwaji wa samaki na mazao yake kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Alisema takwimu zinaonyesha utoroshwaji wa samaki na dagaa kwenda nje katika ZIwa Tanganyika ilikuwa ni mkubwa kwenda nje ya nchi bila kulipa chochote na wageni nao kutoka nchi za jirani wanakuja kwenye maji yetu wanavua na kuondoka.

''Kwa muda mfupi wa siku 15 ambao oparesheni hii imefanyika toka ianze tayari nyavu haramu 3250 thenye thamani ya bilioni tatu haramu zimekamatwa na tumeziteketeza leo hapo ni mitaji imetekea'alisema

Alisema pamoja na nyavu hizo haramu pia wamekamata mitumbwi 93,magari 32,pikipiki 16 na samaki tani kilo elf tano vyote vimekamatwa katika maeneo mbalimbali.Aliongeza kwa kusema kuwa oparesheni hiyo ameizindua ila itaendelea mpaka pale biashara ya uvuvi haramu itakapo koma na kubakia historia.

Kiongozi wa oparesheni hiyo kwa kanda ya Kigoma Nchama Marwa alisema kuwa katika oparesheni hiyo ambayo mpaka sasa ina siku 15 toka ianze kuna baadhi ya wananchi wasiowaaminifu wamekuwa wakiwapa hifadhi raia wa kigeni wanaofanya shughuli za uvuvi huku wakiwa hawana vibali na kuisababishia serekali hasara ikiwemo kukosa mapato.

Marwa alisema changamoto nyingine ni baadhi ya wanasiasa kujaribu kuingilia zoezi hilo,kutokuwepo kwa ushirikiano kwa taasisi za serikali wakati wa kutekeleza oparesheni hadi maelekezo yatolewe toka ngazi za juu.Alisema oparesheni hiyo imeanza kutoa matokeo ambapo baadhi ya wavuvi wameanza kujisalimisha kwa kutii sheria na kukata leseni katika baadhi ya maeneo.

Aliiomba serekali itenge bajeti ya kutosha katika kuendesha oparesheni hiyo ili washiriki wa opareshini hiyo wawe wa kutosha.Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma mjini Samson Hanga amewatahadharisha watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu yeyote ataksayebainika katika kitendo hicho serekali itamchukulia hatua .

''Mhe.Waziri nikuhakikishie tutaendelea kushirikiana na kuwakamata wale wote wanaofanya uvuvi haramu nia yetu ni kuwa na uvuvi endelevu,serekali tupo macho tutawakamata tutawapiga faini ikibidi tutawapeleka mahakamani na tutachoma zana haramu ambazo hazifai kutumika katika uvuvi''alisema
 Waziri wa Mifugo na Uvivu Luhaga Mpina akiteketeza nyavu 352 haramu za uvuvi katika eneo la Businde nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji zilizokamatwa kwenye oparesheni maalum ya kuzuia uvuvi haramu ndani ya  ziwa Tanganyika.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiongea na wavuvi pamoja na wafanyabiashara wa mazao ya dagaa na samaki katika mwalo wa Kibirizi kabla ya kuteketeza zana haramu za Uvuvi zilizopatikana kufuatia oparesheni ya kuzuia uvuvi haramu inayoendelea katika Ziwa Tanganyika

No comments: