Friday, November 2, 2018

MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORAMeneja Mwandamizi NMB Wakala, Tito Mangesho (mbele) akiwasilisha mada kwenye semina kwa mawakala wa Benki ya NMB wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Mmoja wa mawakala wa NMB akiuliza swali kwenye semina hiyo.
Meneja wa NMB Wakala Kanda ya Dar es Salaam, Kisamo Edwin akizungumza na mawakala wa NMB kwenye semina kwa mawakala wa Benki hiyo wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd akizungumza na mawakala wa NMB kwenye semina kwa mawakala wa Benki hiyo wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Sehemu ya mawakala wa NMB waliohudhuria semina hiyo wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akimkabidhi cheti pamoja na zawaadi wakala bora kwa mwaka 2018 Kandaa yaa Dar es Salaam kwenye semina kwa mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Meza kuu kwenye semina kwa mawakala wa Benki ya NMB wa jijini Dar es Salaam ikipiga picha ya pamoja na mawakala bora kwa mwaka 2018 wa Benki hiyo kwa kanda ya Dar es Salaam.BENKI ya NMB imetoa semina kwa mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuboresha huduma na ufanisi kwa wateja wa NMB wanaojipatia huduma za kibenki kwa mawakala hao.
Akizungumza katika semina hiyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema semina hizo ni mwendelezo wa mafunzo kwa mawakala wa NMB nchi nzima ili kuboresha huduma, kukuza biashara zao na kuleta ufanisi katika kumuhudumia mteja.

Alisema NMB ndio benki pekee yenye idadi kubwa ya mawakala zaidi ya 6,000 ambao hutoa huduma nchi nzima huku ikiwa na matawi 228 na mashine za ATM zaidi 800 lengo likiwa kusogeza huduma kwa wateja wake.Mafunzo haya yanaenda sambamba na kuwapongeza mawakala waliofanya vizuri kwa mwaka huu katika kazi zao, ili kuleta chachu kwa wengine kufanya vizuri zaidi.

Akiwasilisha mada za mafunzo kwa mawakala, Meneja Mwandamizi NMB Wakala, Tito Mangesho alisema mikakati ya NMB ni kuongeza idadi ya wateja huku ikitumia njia rahisi na salama ya kuwahudumia watanzania. Alisema malengo mengine ni pamoja na kuongeza unafuu wa gharama zake na uharaka wa kuwahudumia wateja, kupunguza msongamano na kuboresha kamisheni kwa mawakala wake.

1 comment:

Constantine said...

I wish there were more places like this, because it was simply too amazing for words. I came here with my boyfriend the other night, and it was absolutely fabulous. The use of wood throughout the event space Chicago adds a very warm and inviting feel to venue.