Friday, November 16, 2018

MEYA MANISPAA YA IRINGA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA


Na Francis Godwin,Iringa

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani  Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Alex Kimbe kupitia chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA)   makosa mawili ya jinai kuomba na kupokea rushwa .

Kaimu kamanda wa takukuru mkoa wa Iringa Mweli Kilimali akizungumza leo na vyombo vya habari ofisibni kwake alisema kuwa meya huyo alipokea kiasi cha shilingi milioni 2 kutoka kwa mteja wao .

Alisema kuwa tukio la kukamatwa meya huyo lilitokea Novemba 15 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika Hotel ya Gentle Hills mjini Iringa .Kuwa meya huyo ambae ni diwani wa kata ya Isakalilo aliokea pesa hizo kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.

Alisema meya Kimbe alipokea fedha hizo za mtego wa rushwa akiwa kwenye gari yake aina ya nadia yenye rangi ya Marron ikiwa na namba za usajili T 456 CKD iliyokuwa imeegeshwa katika eneo la kuegesha magari kwenye hoteli hiyo .“ Maafisa wa takukuru waliweza kumfuatilia meya huyo kwa muda mrefu na hivyo kuweza kumkamata akiwa amekwisha pokea fedha hizo za mtego kutoka kwa mtoa taarifa wao “

Kilimali alisema kuwa awali walipokea taarifa ya kuwepo kwa ushawishi wa  kutoka kwa meya huyo kwenda kwa mmoja kati ya wakandarasi wanaoendesha tenda katika Manispaa ya Iringa ili muda ukiisha apate nafasi ya kupata tenda husika .Hivyo meya huyo alimuomba mtoa taarifa rushwa na shilingi milioni 10 na baada ya mtoa taarifa kujitetea hatokuwa na uwezo wa kutoa fedha hizo mtuhumiwa alikubali kupokea shilingi milioni 2.

Akiwa mahakamani Mwendesha mashtaka upande wa jamhuri Restuta Samson alisema hamakamani hapo jana kuwa Kimbe anashitakiwa makosa hayo mawili likiwemo la kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Nance Nyalusi kama zawadi baada ya kupata zabuni ya kukusanya ushuru stendi kuu ya mabasi mjini Iringa .Kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo kinyume na sheria kwa meya kuomba zawadi hiyo kutoka kwa mzabuni huyo .

Wakati shitaka la pili ni mshitakiwa amefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la kupokea rushwa kutoka kwa Nance Nyalusi .Hata hivyo mshitakiwa huyo aliweza kukana makosa yote yanayomkabili kuwa si ya kweli na kwa kuwa upande wa wakili wa jamhuri katika kesi hiyo uliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi bado haujakamilika na hauna pingamizi juu ya dhamana ya mshitakiwa .

Hakimu wa mahakama hiyo Liad Chamshana alisema hamaka yake inamtaka mshitakiwa kusaini dhamana ya maadishi ya shilingi milioni 10 pamoja na kuwa na wadhamini wawili mashariti ambayo yalitekelezwa na mshitakiwa kuachiwa kwa dhamana .

Akizungumza nje ya mahakama na waandishi wa habari wakili anayemtetea Kimbe Lutebuka Samson Antony alisema kuwa kosa la kwanza linalomkabili mtaja wake ni kudhaniwa kuomba rushwa huku kosa la pili ni la kudhaniwa kupokea rushwa kesi hiyo itatajwa tena Desemba 5 mwaka huu .
Kimbe akiwashukuru waliofika Mahakamani leo.
 Meya Alex Kimbe akifikishwa Mahakamani na Maofisa wa TAKUKURU leo
Meya Alex Kimbe akiwa Mahakamani leo 

No comments: