Thursday, November 15, 2018

MENEJA DAWASA BAGAMOYO AAHIDI KUPOKEA MRADI WA MAJI VIKAWE

NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 
MENEJA wa mkoa wa mamlaka ya maji safi na salama ( DAWASA)wilayani Bagamoyo  ,mkoani Pwani, Alex Ngw'andu ameahidi kuwa wataupokea mradi wa maji kutoka Ruvu Chini -Vikawe Shuleni  -Miwale Kibaha Mjini , ifikapo novemba  30 mwaka huu. 

Ametoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kuunda kamati ya watu sita wiki iliyopita, kwenda kwake kufuatilia suala hilo ili kuondoa kero ya kipindi kirefu ya ukosefu wa maji kwa wakazi wa Vikawe. 

Ngw 'andu alisema ,kamati hiyo imefika ofisi kwake kwa nia ya kujua kama DAWASA itauchukua mradi wa Vikawe  kutokana na halmashauri ya Mji huo kuonekana kushindwa kuuendesha mradi ipasavyo.
Alieleza, tayari Bagamoyo wameshaupitia mradi na wahandisi wameshapata michoro na taarifa za uendeshaji na sasa wanajiaandaa kuufufua kwa maana kuweka umeme wa uhakika ili pampu za kusukuma maji zifanye kazi masaa angalau16 kwa siku.

"Kufufua vizimba (DP) vilivyopo na kuanza house connections (kusambaza majumbani) kwa wateja ifikapo January 2019 "

"Kwa ufupi ni kwamba mradi utapokelewa end of this month, maji na huduma iliyokuwa inatolewa awali itakuwa restored, ikiwa ni pamoja na maboresho ya kipindi cha upatikanaji maji",alifafanua Ngw'andu.

Alieleza, wamekubaliana na kamati hiyo maalumu ya mbunge Koka yenye diwani wa eneo la Pangani,  wahandisi na msaidizi wa mbunge kuwa DAWASA pia itakwenda kutembelea eneo la huduma Vikawe jumamosi ijayo.

Kwa upande wake ,katibu wa mbunge Method Mselewa alimshukuru meneja huyo kwa kushughulikia kero za wananchi. 

Mselewa alisema, kwa hakika DAWASA ya sasa inakwenda kujibu kero ya ukosefu wa maji Vikawe ambayo ilikuwa ikisababisha wakazi wa eneo hilo kutumia maji ya visima licha ya kuwa mjini.  

No comments: