*Biteko asema wachimbaji sasa kuchimba kwa uhakika
Na Asteria Muhozya, Dodoma
Taasisi
ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetakiwa kuandaa
ramani zinazoonyesha madini mbalimbali katika ngazi ya Mikoa na Wilaya
ili kuwapa nafuu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini
nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko baada ya kupokea
taarifa ya Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo
(Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika nchi nzima
kwa ushirikiano kati ya GST na Taasisi ya Jiolojia ya China.
Naibu
Waziri Doto pia, ameitaka taasisi hiyo kuelekeza nguvu katika kuisaidia
serikali katika kupata matokeo chanya katika shughuli za madini huku
ikiongeza thamani ya kazi kutokana na utafiti huo na kuongeza kuwa, GST
inaweza kutumia utafiti huo mkubwa kuandaa ramani za madini katika ngazi
za Mikoa na Wilaya.
Akizungumzia
manufaa ya tafiti huo kwa Tanzania, amesema baada ya muda si mrefu
watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji watahamia katika uchimbaji
wa uhakika na siyo wa kubahatisha kwa kuwa utafiti huo unaonesha mahali
sahihi ambapo shughuli hizo zinaweza kufanywa.
Amesema
mbali na shughuli za madini, utafiti huo pia unaweza kutumika katika
sekta za kilimo, maji na ujenzi wa barabara kwa kuwa unawezesha kutambua
aina ya udongo unaofaa kwa shughuli hizo.
Kutokana
na umuhimu wa utafiti na kazi iliyofanywa na taasisi hizo mbili, Naibu
Waziri Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuitumia taasisi ya GST katika
shughuli za kitaalam ikiwemo kupata taarifa za utafiti zinazohusu sekta
ya madini na kuongeza kuwa, sekta hiyo inao uwezo mkubwa wa kutekeleza
wajibu wake.Aidha,
Naibu Waziri Doto ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China
kutokana na ushirikiano huo iliyoutoa katika kutekeleza utafiti huo
ambao umegarimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 4 na Laki Tano
Kwa
upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jilojia ya China, Profesa Sun
Xiaoming amesema kuwa taarifa ya utafiti iliyowasilishwa ni ya nchi
nzima ya Tanzania na eneo la Mkoa wa Mbeya.Amesema
utafiti huo umetoa matokeo ya jiokemia ya sampuli 71 nchini kote na
sampuli 39 katika mkoa wa Mbeya na kuongeza kuwa utafiti huo utasaidia
katika utekelezaji maendeleo ya shughuli za madini, kilimo na mazingira
nchini.
Awali,
akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Mathias Abisai amesema kusudio la ujumbe huo ilikuwa ni kuhakiki kazi
iliyofanyika na kuwasilisha ripoti. Ameongeza kuwa, ripoti hiyo
itasaidia kwenye tafiti nyingine za madini ikiwemo maji na mazingira.
Ameongeza
kuwa, mnamo Mwaka 2009 serikali ya China na Tanzania kwa kutumia
taasisi zake za Jiolojia zilisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa lengo
la kuanzisha mradi huo wa miaka mitano ambapo kazi rasmi ya mradi
ilianza mwaka 2013 na kukamilishwa mwaka 2018.
Naye,
Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Yokobeth Myumbilwa akileza malengo ya
utafiti huo amesema kuwa ni kupata taarifa za utafiti wa jiokemia kwa
ajili ya kuandaa kanzidata ambayo itaainisha uwepo wa taarifa zinazo
ainisha uwepo wa aina mbalimbali za madini ,upangaji miji ,pamoja na
taarifa hizo kuweza kutumika katika shughuli mbalimbali katika sekta za
kilimo na mazingira.
Naibu
Waziri wa Madini Doto Biteko, akionesha taarifa ya utafiti wa jiokemia
uliofanywa nchi mzima na Taasisi ya Jiolojia ya Madini Tanzania (GST)
kwa kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia ya China. Kulia ni Mtendaji Mkuu
wa Taasisi ya Jiolojia ya China Profesa Sun Xiaoming na Kushoto ni
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mathias Absai.
Naibu
Waziri wa Madini Doto Biteko katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka
Taasisi ya Jilojia ya China, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini
Tanzania (GST), na Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.
Naibu
Waziri Doto Biteko akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya
China, Profesa Sun Xiaoming Cheti cha kutambua mchango wake na
kukamilika kwa utafiti wa Jiokemia uliofanywa nchini.
Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming (kulia)
akitoa taarifa ya utafiti huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Madini Doto
Biteko na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Mathias Abisai.
Sehemu
ya Wataalam kutoka Taasisi ya Jiolojia ya China, Wizara, Taasisi ya
Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Tume ya Madini
wakifuatilia kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa GST, Yokobeth Myumbilwa akizungumza jambo katika kikao hicho.
Naibu
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo (katikati). Kulia ni
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming na
kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Mathias Abisai.
Naibu
Waziri wa Madini Doto Biteko akionesha Taarifa ya Utafiti wa Jiokemia
iliyofanywa katika Mkoa wa Mbeya. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu
Mathias Abisai.
No comments:
Post a Comment