MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Freeman Mbowe anayekabiliwa na kesi ya Uchochezi namba 112 ya mwaka huu amesafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini akiwa mahututi kwa ajili ya matibabu ya moyo na shinikizo la damu.
Hayo yameelezwe leo Novemba Mosi mwaka huu na Wakili Peter Kibatala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali, (PH).
Wakili Kibatala ameieleza Mahakama kuwa alimuhoji mdhamini wa Mbowe, Grays Celestine na akamueleza kuwa Mbowe amesafirishwa jana jioni akiwa mahututi kuelekea Afrika Kusini na nyaraka za usafiri na matibabu zitawasilishwa kwa barua mahakamani.
Kibatala alieleza kuwa Mbowe amekuwa akifika mahakamani mara kadhaa bila kukosa, hivyo adhabu kwamba kueleza anaidharau mahakama kwani hata kitendo cha kumtuma mdhamini wake si jambo la dharau.Kutokana na taarifa hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi ameiomba Mahakama itoe amri ya kumkamata mara moja Mbowe ili ajieleze kwani dhamana aliyopewa na mahakama isifutwe kwa kushindwa kuiheshimu.
Baada ya mdhamini huyo kueleza hayo, Hakimu Mashauri alimuuliza kama ana nyaraka ya kuithibitishia mahakama kuwa Mbowe amesafiri nje ya nchi kwa Matibabu lakini mdhamini huyo alidai kuwa hana na kwamba mshtakiwa akirejea atawasilisha nyaraka za safari na Matibabu kwa mahakama na upande wa mashtaka.
Pia anaendelea kufanya mawasiliano ili aweze kutumia kwa Fax.Hata hivyo wakili Nchimbi alidai, kutokana na taarifa hizo bado analazimika kueleza mdhamini hajaonesha uzito wowote kwa kuwa tunata kujua ameenda nje kwa matibabu, lini, katika taasisi gani na nchi gani.Ameongeza labda aliondoka akiwa mahututi lakini waliomsindikiza wangeweza mdhamini, hivyo hao wao upande wa mashtaka hayo wanaona ni muendelezo wa dharau ya mshtakiwa kwa kuwa alikwisha pewa onyo mara mbili.
Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Mashauri amekubaliana na hoja hizo za upande wa mashtaka na kwamba mshtakiwa huyo anapaswa kuja mahakamani kueleza kwa nini dhamana yake isifutwe.Hata hivyo Hakimu Mashauri amesema iwapo mshtakiwa hatopeleka vielelezo atatoa amri ya kukamatwa ili ajieleze kwani ni asifutiwe dhamana kwa kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa na mahakama.
Mbali na Mbowe, Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo, wanatetewa na wakili Peter Kibatala ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa bunda, Esther Bulaya, Mbunge wa
Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Vincent Mashinji. Huku Peter Msigwa anatetewa na wakili Jamuhuri
Johnson.Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment