Waziri
Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi
wa albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi,
utakaofanyika Disemba 2, 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli
Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi ambaye atazindua albamu yake skiku ya tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka huu
Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi
wa albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi,
utakaofanyika Disemba 2, 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli
Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini Dar es Salaam.
Mbali
na Lowassa, waimbaji watakaosindikiza uzinduzi wa albamu hiyo inayoitwa
‘Hakimu wa Haki’ ni Bahati Bukuku, Dk Tumaini Msowoya, Tumaini Njole,
Tumaini Mbembela, Madamu Ruth ,Iren Mwamfupe, Bony Mwaitege, Margie
Muliri, Juvenalista Mabuma Edson Mwasabwite.
Akizungumza
na Mwananchi, Mariam alisema amemualika Lowassa kwa sababu ndiyo
aliyeanza kuibu kipaji chake, alipompa nafasi ya kuimba siku ya sherehe
yake ya kuzaliwa.
“Lowassa
ni baba yangu, aliibua kipaji change ndio maana nikatamani awe mgeni
rasmi na amekubali, namshukuru sana Mungu kwa sababu hii,” alisema.
Alitaja
nyimbo zilizo kwenye albamu yake kuwa ni Hakimu wa Haki, Pam Pam
tukuza, Natafuta Mshauri, Chereko leo, Nasikia Kuitwa, Agano Langu,
Ushindi Lazima na Mapambazuko.
“Nasikia
kuitwa ndio wimbo ambao niliimba wakati nikianza mbele ya baba Lowassa,
kwa hiyo ilipofika hatua ya kuandaa albamu yangu niliuweka na huo kwa
sababu ndio ulionifungulia njia,” alisema.
Akizungumzia
changamoto alizokutana nazo kwenye muziki huo, Mariam alisema ni
gharama kubwa ya uandaaji wa muziki pamoja na kusambaza kazi hiyo.
“Naimba
muziki kwa sababu nasikia kuitwa kwa ajili ya kazi hiyo, kusema kweli
gharama za uandaaji wa kazi nzuri ni kubwa hata hivyo namshukuru Mungu
kwa sababu nimeshakamilisha hatua ya kwanza,” alisisitiza.
Hata
hivyo alisema, imekuwa rahisi kwake kufikia ndoto ya mafanikio kwa
sababu ya sapoti kubwa kutoka kwa waimbaji waliotangulia.
Mariam amesema tayari tiem ya wacheza show ‘dancers’ imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya siku hiyo.
“Mara
nyingi waimbaji wa muziki wa injili huwa tunapuuzia wacheza shoe lakini
ni watu muhimu na hawa ndio huwa wanafanya watu wafurahie matamasha,
kwa hiyo tayari nimeshawaingiza kambini,” alisema.
Akizungumzia
uzinduzi huo, mwimbaji Jesca Gazuko anayetamba na wimbo wa ‘Bwana
Amefanya’ alisema ujio wa Lowassa unaonyesha namba ambavyo viongozi
wamekuwa wakisapoti kazi za waimbaji wanaochipukia.
No comments:
Post a Comment