Tuesday, November 6, 2018

KUMEKUCHA NAMTUMBO MARATHON, MAMIA WAJITOKEZA KUJIANDIKISHA

Wanariadha kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki Namtumbo Marathon inayotarajiwa kutimua vumbi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma ambapo maelfu ya wakazi wa wilaya hiyo na vitongoji vyake wamekuwa wakizitazamia mbio hizo kuanza wakati wowote ili nao wapate fursa mbalimbali za kushiriki katika mbio hizo.

Akizungumzia usajili unaoendelea katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo, Dokta Chihoma amesema watu wengi wameitikia wito na wamejitokeza kwa wingi wao kujiandikisha tayari kwaajili ya kushriki mbio hizo ambazo zilianzishwa rasmi mwaka 2017 kwa malengo mengi lakini kubwa likiwa ni kuchangisha fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambayo imefanikia kuanza kwa kiasi kikubwa. 

Aidha Chihoma ameongeza kuwa nafasi bado zipo wazi kwaajili washiriki watakaojitokeza kujiandika kwaajili ya bio hizo. 

Kwa upande wao wadhamini wa na waandaaji wa mbio hizo Mantra Tanzania au Uranium one wamesema kila kitu kipo sawasawa na kuwataka watanzania na wageni kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo zinalenga kuleta maendeleo ya kiafya katika eneo la Namtumbo na vitongoji vyake. 

Mwakilishi wa Mantra Tanzania Bi. Khadija Pallangyo Kawawa amaesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba watanzania watafurahia mbio za mwaka huu kutokana na jinsi zilivyopata hamasa kubwa katika maeneo mbalimbali “Nawaomba sana watanzania wajitokeze kwa wingi waje washiriki nasi katika kufanikisha awamu ya pili ya Namtumbo Marathon” 

Alisema Khadija huku akiwaomba wana Namtumbo, Songea Ruvuma na vitongoji vyake hasa wafanya biashara na wenye makampuni katika maeneo mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi kuuchangia ujenzi wa hospitali ya wila ya Namtumbo akiitaja hospitali hiyo kuwa itakuwa msaada mkubwa wenye kuleta mafanikio na maendeleo katika eneo lote linalopakana na wilaya hiyo. 

Nao waratibu na wasimamizi wa tukio zima Corporate Info Limited ya jiji Dar Es Salaam wamesema mbio hizo zinaandandaliwa kuja kuwa moja kati yam bio kubwa kabisa nchini huku wakijivunia kuwa wasimamizi wa mbio hizo kwa mara nyingine. 

Wilaya ya Namtumbo imezungukwa na vivutio mbalimbali vya kiasili mojawapo ikiwa mbuga kubwa ya wanya ya Sloue ambayo imekuwa kivutio kikubwa sana kwa watalii kutoka mataifa mbalimbali na ndani nchi hivyo kufanyika kwa mbio hizo itakuwa sehemu mojawapo ya kuitangaza mbuga hiyo pamoja na vursa zingine kama madini aina ya Uranium ambayo yanapatikana kwa wingi wilaya Namtumbo. 

No comments: