Thursday, November 29, 2018

KAZI INAKWENDA VIZURI MRADI WA RELI YA KISASA KUTOKA DAR MPAKA SINGIDA MAKUTUPORA


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Dodoma

Kazi inakwenda vizuri. Ndivyo unavyoweza sema juu ya mradi wa reli ya kisasa marufu ya Standard Gauge kutokana na Shirika la Reli(TRC) kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kumsimamia mkandarasi Yepi Merkezi kwa ukaribu mkubwa.

Michuzi Blog imetembelea mradi huo, kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora, ambako kuna vipande viwili vya mradi huo vinavyotekelezwa na mkandarasi huyo, kujionea kuna mabadiliko makubwa juu ya ujenzi huo tofauti na watu wanavyozungumza katika Mitandao ya Kijamii na Vijiweni.

Hii inatokana na kuwepo kwa madai ya kuwa hakuna kazi inayofanyika, ambapo kumefichuka kuwa kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kazi imefanyika kwa zaidi ya asilimia 36, ambapo sehemu zilizobakia ni ndogo na zinazowezwa kufanya kazi kwa uharaka na mkandarasi.

Pia, inaelezwa hata baadhi ya malighafi nyingi zinapatikana kwenye eneo la mradi iwe kipande cha Morogoro hadi Makutupora au Dar es Salaam hadi Morogoro, ambapo imerahisisha upataji wa marighafi.Akizungumza na Michuzi Blog Meneja mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC), Injinia Masanja Machibya, amesema hakuna malighafi yeyote inayozalishwa nje, bali mahitaji yote muhimu yanapatikana kwenye eneo la mradi.

Amesema kwa upande wa kipande anachokisimamia cha Dar es Salaam hadi Morogoro, malighafi zote zinapatikana ikiwemo kuwa na kiwanda cha kokoto chenye uwezo mkubwa wa uzalishaji wa kokoto na kuondoa kabisa tatizo la kuagiza kokoto.

amesema kuna kiwanda cha kutengeneza mataluma, ambapo mataluma 1080 yanazalishwa kwa siku na kazi yote inafanywa na vijana wa kitanzania, Mataluma hayo yanatengenezwa kwa kutumia Nondo, Saruji, Kokoto, Mchanga na Maji ambavyo vyote vinapatikana nchini.Amesema wameweza hata kutandaza nyaya za mawasiliano ili kuwasaidia waongoza treni pindi itakapoanza. hivyo ana matumaini makubwa mradi huo unakwenda kufanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na vitu vinavyofanyika.

Akizungumza naye na Michuzi Media, Injinia Faustine Kataraia, ambaye ni msimamizi wa mradi wa SGR kwa upande wa Morogoro hadi Makutupora, amesema sasa wamemaliza kujenga kiwanda cha kokoto eneo la Morogoro, ambazo zitatumika kwenye kipande hicho na mradi utakapomalizika kiwanda kitaendelea kuwepo.

"Huu si mradi pekee kiwanda tulichojenga hapa Morogoro tunaweza kuuza hata kwenye miradi mingine ya barabara au kwa watu binafsi, hapa tunaweza kusema tumeunga mkono jitihada ya rais Dk.John Magufuli ya viwanda," amesema.

Amesema kila kitu kinakwenda vizuri hasa upande wa Morogoro hadi Makutupora, hivyo hadi ifikapo 2021 mambo yatakuwa mazuri na mradi utakuwa bora kwa kuwa kwa miundombinu iliopo itasaidia hata mwendesha treni alioko Dar es Salaam kuona kila kitu kinachofanyika

Meneja mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC), Injinia Masanja Machibya, akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu mradi huo unavyoendelea katika Lot 1 inayotoka Dar es Salaam mpaka Morogoro.
Meneja mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini (TRC), Injinia Masanja Machibya,akiwaonesha Wanndishi wa Habari mfano wa Reli ya SGR itakavyokuwa katika kiwanda cha kuzalisha Mataluma ya Reli hiyo.
Mafundi Wakiendelea na Ujenzi wa Madaraja na karavati katika eneo la mradi wa SGR eneo la Lot 1 Kisarawe.

Mataluma ya Reli yakiwa yameweka kwa ajili ya kutandikwa juu ili kujenga mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC),
Sehemu ya Wakandarasi wakiendelea na upandaji nyasi kwa ajili ya kuzuia Mmomonyoko wa udongo  kwenye tuta la kukatisha reli ya SGR.
Mafundi chuma wa mradi wa SGR Kutoka Yap Markenz wakiendelea na kazi katika yard ya Shaurimoyo Jijini Dar es Salaam.
Mafundi chuma wa mradi wa SGR Kutoka Yap Markenz wakiendelea na kazi ya kujenga Madaraja ya kupachika katika yard ya Shaurimoyo Jijini Dar es Salaam.
Moja ya kituo cha Mfano kikiwa katika picha ya mfumo wa 3d na kikionesha namna ya kituo cha Pugu Station kitakavyokuwa. 

No comments: